Hatimaye Mfalme wa Pop,Michael Jackson,anatarajiwa kuzikwa leo huko Forest Lawn-Glendale,California katika makaburi yajulikanayo kama Holly Terrace.Mazishi yanatarajiwa kuanza saa moja usiku kwa saa za California.
Kwa mujibu wa taarifa kuhusu mazishi hayo,yatakuwa ni mazishi “private” na hivyo ni ndugu,jamaa na marafiki wa karibu pekee watakaoweza kuhudhuria.
Mazishi haya yanafuatia mlolongo wa matukio tangu alipofariki mwanamuziki huyo ikiwemo uchunguzi wa kipolisi kuhusiana na kifo chake na pia kupingana kwa ndugu na wanafamilia yake kuhusiana na swala la wapi azikwe. Mengine yaliyoibuka tangu afariki dunia ni pamoja na habari za matumizi mabaya ya madawa ya kutuliza maumivu na kulaza aliyokuwa nayo Michael Jackson.
Hivi karibuni Mchunguzi wa vifo wa California,alithibitisha kwamba Michael Jackson alifariki dunia kutokana na kuchomwa sindano ya kupunguza maumivu ambayo ilikuwa na dozi kubwa kuliko kawaida. Daktari aliyekuwa naye siku hiyo,Dr.Murray, ndiye anatupiwa lawama zote ingawa mpaka leo hakuna mashtaka rasmi kuhusiana na kifo cha mwanamuziki huyo.
Pumzika Salama Michael.
Feedback / Comments
18 Responses to “MJ KUZIKWA LEO”
Leave a Reply


sending...
bado sijaamini kama kweli michael hatunaye
i love you michael love, love, love you milele nitakupenda pumuzika kipenzi chetu
ww RITTA utapenda wangapi? ulionao tu wanakushindwa sasa huyu MJ unampenda akiwa ameshakufa??? na sio PUMUZIKA ni PUMZIKA.
Sasa hata kuandika hujui huyu MJ mlijuanaje hadi utokee kumpenda kiivyo.
JITAHIDI KUPUNGUZA SHOBO .
wewe micharuko aliyekuambia kujuwa kiswahili ni deal nani? of couse nampenda na nitampenda milele,
eti sijuwi kuandika nimemjuwa wapi kweli wewe mswahili
sasa aliyekuambia mtu akifa hapendwi nani?
kabla hujanikosoa nenda kapige mswaki ndiyo uje kukosoa maoni yangu
kweli wewe micharuko pole sana kwa uswahili
micharuko kwa kukusaidia mimi sio mswahili mwenzio na pia ukitaka kujua jaribu kuangalia maoni yangu nimeyatoa saa ngapi za huko kwenu ili ujuwe,
si wote tutajuwa kiswahili na si deal kwa sisi wengine labda wewe.
Kwako Micharuko
Mi namjua Ritta ana maradhi ya kupenda!!!!
yaaaaani we acha tu!!!!!!
kuna watu washamba mpaka wanachefua hata akijua kuwa unakaa wapi ndio nini na wewe inakuongezea nini au inapunguza kubaguliwa huko ulipo lo!jivunie chako ndio maana wampenda huyo mwenzio ndio walewale wa kukataa asili yao,mshindwe na mlegee sehemu zenu muhimu.
wewe sonia acha korosho nani kakwambia tulioko majuu tunabaguliwa? au umedata? wewe ndiye mshamba halafu unasema wenzio wewe kavu kweli nafasi ya ritta ukiipata je utaiacha????????????????????????
tena kwa taarifa yako we chuma cha pua mie siishi kama digidigi kama wewe ambae hata hao unaowaabudu wakikufanyia ujinga unakula kona unaogopa polisi,sasa kati yangu mimi na wewe nani kadata?
ritta + mcharuko = romance
he he he heeeeeeeeee!! Papai umenichekesha saana….sina mbavu hapa nilipo….wee acha tuu…!! Inatia raha lol
sonia wewe kama hubaguliwi inakusaidia nini wakati jirani yako albino anawindwa kuuliwa?
wewe hata mshipa wa noma huna kutucheka sisi tunaoishi ulimwengu wa kwanza haki za binadamu zimeanzia huku sema kipande hiki unakitamani na hutokipata utaishia kukasirika tu,
tena kaa ukijuwa kuwa hayo mambo unayoyasema mimi sijawahi kuona.HUKU KWETU MTU AKIKUBAGUA SIANATAFUTA KUKURIPA EURO ZA KUTOSHA. sasa wewe aliyokupa hadidhi hiyo hataki uje uone ulimwengu wa kwanza hivyo oza hukohuko
wewe sonia toka unyimwe visa umekasirikia kila mtu
DUUU!!!!!!!!!!1 KWELI HILI PAPAI BADO BICHI!!!
hivi nyie mnafikiri kila mtu anasubiri kuhadithiwa maisha mnayoishi nyie huko mliko,siku zote mtabaki kuwa duni na watu wa daraja la pili huko mlipo kubali,kataa nafsi inakusuta na kamwe usiotee nilipo ni vitu ninavyoviona,na naongea ninachokijua na kuhusu kunyimwa visa kwangu sahau nina mkoba begani au nikupe mwaliko.
ninyi wa tanzania mdomo mdomo kila mahali, yani huwezi kusema neno bila mweginf kujibu. show off kama uko ni nini si wote ni watu tuna pumua 02 na kila mahali kuna shida mbalimbali.
Kha jamani kweli kusoma kitu kingine na kuelewa ni kitu kingine. Issue hapa ilikuwa ni mazishi ya MJ sasa mambo ya kuishi ulimwengu wa kwanza na visa yametoka wapi??? Mbona mnajishaua bila sababu??? Maisha popote jamani!! Wapo watu wanaishi hapa TZ wanakula bata na kutesa kuliko waliko huko mnakokuita ulimwengu wa kwanza. Tumewaona watu waliopoteza muda wa maisha yao kufanya kazi za ovyo Ulaya na hata wanatamani kurudi bongo ila wanakosa nauli. Teh teh zungumzieni mambo ya MJ na si mashauzi. Mtu pale alipo ndo bora. HATA HIVYO KUMBUKENI MTU KWAO BWANA WEEE
wewe miriam john kama wewe unaelewa kusoma aliyeharibu mazungumzo hapo nani?? bongo utatesa au utateseka???