baby-powder

Kila kukicha,watanzania mbalimbali waliotapakaa ulimwenguni kote wanazidi kuwa wabunifu na watu wanaothubutu kufanya mambo fulani fulani ambayo sio tu yanazidi kuiweka Tanzania mahali inapostahili katika ramani ya dunia ,bali pia kuongeza ujuzi,kuingiza vipato halali na zaidi to make us proud!

Hayo yanatokea katika nyanja mbalimbali ikiwemo ya filamu!Bila shaka ulifuatilia filamu za Kibira za Bongoland.Ukipenda unaweza kusema ule ulikuwa ni mwanzo tu.Wengine wamefuata nyayo hizo na wanakuja na filamu inayokwenda kwa jina la BABY POWDER. Ni watanzania wanaoishi jijini Atlanta,GA.

Filamu hii inatarajiwa kuonekana kwa mara ya kwanza kabisa ndani ya jiji la Atlanta lililopo jimboni Georgia nchini Marekani tarehe 14 November,2009.Baada ya hapo itaonyeshwa jijini Houston huko Texas tarehe 26 November,2009 na kisha jijini Washington,DC tarehe 5 December 2009. Baada ya hapo itakuwa zamu ya watu wa Minnesota kuiona tarehe 19 December 2009 kabla ya tour ya Europe na Africa haijaanza tarehe 25 December 2009. Tarehe na miji itakapoonyeshwa filamu hiyo zitatangazwa baadaye.

BABY POWDER ni filamu inayogusa maisha ya kweli . PHILIP NKASA (Lambert “LBT” Tibaigana) ni kijana wa kitanzania ambaye anakwenda Marekani kwa matumaini ya kupata elimu ili kuweza kuboresha maisha yake na ya familia yake nyumbani. Philip ananzaa maisha yake ndani ya Marekani katika mji mdogo wa Wichita,KS na baada ya kumaliza shule na kushindwa kupata kazi ,Philip anakata shauri kwenda kujaribu bahati yake katika jiji la Atlanta, GA.

Mambo hayawi kama Philip alivyotegemea.Upatikanaji wa kazi jijini Atlanta unakua wa shida.Ili kuendesha maisha Philip anachukua kazi ya malipo kidogo pamoja na kuwa tayari ni msomi mwenye shahada ya kwanza(degree)Hali ya maisha ya wazee wake inaendela kuwa mbaya kutokana na mapato yake kuwa kidogo na hivyo kushindwa kuwasaidia.

Tizama Trailer hapa;

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Baada ya kugundua mfanyakazi mwenzake Mamdo (Albert Levasseur) anafanya biashara haramu, Philip anaona hiyo ndio nafasi ya kutatua matatizo yake.Baada ya kuonja asali anachonga mzinga. Anaingia katika biashara  haramu kwa nguvu zote.

Kutokana na kukua kwa biashara yake, Philip anaongeza msaada kutoka kwa vijana wenzake Tizo ( Carlos Mwaibulla) Chuma (Ulimboka GWAII Mwanjabala) na Wesi (Hadji Saidia).Penye wengi hapaharibiki jambo.Lakini kundi hili linaubadilisha msemo huo….( mengi yanaharibika)

Philip anaingia mapenzi na mrembo kutoka Kenya WARIDI (Tuni Ngigi) ambaye anashindwa kumwambia ukweli kuhusu biashara zake. Za mwizi arobaini.Waridi anakuja kugundua.

Majina ya waigizaji

Lambert Tibaigana-         PHILIP NKASA

Tuni Ngigi                      WARIDI

Carlos Mwaibulla            TIZO

Ulimboka Mwanjabala      CHUMA

Hadji Saidia                    WESI

Lydia Mbuah                   JOSELYNE

Warda Hassan                JACKEY

Dynamic                        DULAH

Albert Levasser               MAMADO

Babu sikare                     KAI

na wengine wengi….

BABY POWDER ni filamu inayo elimisha, sikitisha ,furahisha,na kutia moyo.Ni mkasa wa kuburudisha…

Filamu hii haita toka kwenye DVD mpaka mkatikati ya mwaka 2010 nafasi pekee ya kuiona filamu hii ni wakati wa uzinduzi rasimi katika sehemu mbali mbali

Kwa habari zaidi tembelea www.jake-productions.com

Feedback / Comments

15 Responses to “COMING SOON…BABY POWDER!”

  1. Comment by Harold on September 11th, 2009 12:06 pm

    Guys this is cool, you really tried to come out cooly, Man i cant wait till mid next year!! When is the lauch and where?

    Two thumbs up!!

  2. Comment by Geoffrey on September 11th, 2009 1:19 pm

    hii kitu imetulia sana, aisee!, much respect. the audio quality, image quality, dialogue, action it all sums up to ONE BIG MOVIE not to be missed. I cant wait to see it.

  3. Comment by mare on September 11th, 2009 3:08 pm

    lakini mbona cover yake haivutii, japokua wanasema dont judge the book by its cover.

  4. Comment by Dinah on September 11th, 2009 4:36 pm

    Safi sana!
    Inapendeza.

  5. Comment by Vyne on September 11th, 2009 4:45 pm

    Trailer haina ulemsisimuo wa mtu kutaka ona unless uwe wapenda kuna wanawake na vichupi au wanaume bila mashati.I don’t hate but not sure abt this.

  6. Comment by Riziki Romwald on September 11th, 2009 7:48 pm

    Excellent contents,better than Kanumba’s saga.Conversely,you need to do more work on the cover.the message it potray is quite different message from the theme of the movie.Beside,it is not attractive by all criterion.

    Can you find something else will be more appealling to the audience please?.Overall,it is a good start and a good movie to watch.Foks! Everybody needs to have a dream”.I like your dream.

  7. Comment by Riziki Romwald on September 11th, 2009 7:51 pm

    Excellent contents,better than Kanumba’s saga.Conversely,you need to do more work on the cover.the message it potray is quite different from the theme of the movie.Beside,it is not attractive by all criterion.

    Can you find something else more appealling to the audience please?.Overall,it is a good start and a good movie to watch.Foks! Everybody needs to have a dream”.I like your dream.

  8. Comment by kamanzi on September 12th, 2009 3:22 am

    Lambert Tibaigana. Nilisoma na huyu dogo pale Tambaza miaka hiyo. Clips zinaonyesha pengine kwa mara ya kwanza kutakuwa na filamu ya ukweli Tanzania na ukisikiliza lafudhi ya waigizaji unakubali wakitumia title ya kizungu. Inanichefua pale unapoita filamu jina la kizungu halafu waigizaji akina KANUMBA. Utumbo mtupu. Ingawa lazima tukubali kwamba kwa namna moja au nyingine wazembe hawa tunaowaponda ndio walioanzisha filamu bongo ingawa ni kwa kukopi wanigeria.

  9. Comment by MAKULILO, Jr. on September 12th, 2009 3:48 am

    Hongereni sana kwa kuandaa filamu yenye kuonesha maisha ya kweli ya ughaibuni. Binafsi naamini yatatoa picha halisi ya mtu anapotaka kuja kusoma au kikazi ughaibuni kupata mwanga wa nini afanye kabla na wakati akiwepo ughaibuni.

    Nawapongezeni kwa kazi nzuri, japo trailer ni fupi naamini nitaweza kuiona full movie yenyewe na kupata mafundisho yaliyomo.

    MAKULILO, Jr.
    San Diego, California
    http://www.makulilo.blogspot.com

  10. Comment by Geoffrey on September 12th, 2009 6:29 am

    @Mare, mimi naona hiyo cover/poster iko sawa kwa upande wangu, imebeba ujumbe kuhusu Philip/LMT, amekuwa ni mtu anayebeba uzito kila mahali, yupo shuleni na kwenye mihangaiko mingine maishani, utaona kashika vitabu, babypower, kavaa kofi ya degree, na kama ganster…I think its cool.(my opinion)

  11. Comment by tabitha on September 12th, 2009 11:29 am

    Well mi kivyangu ni kazi nzuri sana,i cant wait watching the movie na nakususapport sana kaka geoffrey,cover iko sawa sawa na theme ya movie lbt ni mhangaikaji so shule tuko na mtaani pia,ni ubunifu mkubwa,sio lazima kazi nzima ionekane kwenye cover kama tulivyozoea watanzania we nid a change jamani.Im proud of u brothers mnawakilisha n all the best.

  12. Comment by george on September 17th, 2009 7:23 am

    its a movement,i must watch this movie.

  13. Comment by jakeProductions on November 12th, 2009 12:15 am

    Thank you so much for all your comments. Its always positve knowing that you all took the time to write your views… please keep them coming.

  14. Comment by Mwanaisha on November 12th, 2009 12:36 am

    @ Kamazani mimi nashindwa kuelewa kua umependa hiyo movement au haupendi? Ukitaka kuuza Cinema katika soko la dunia, inabidi uchague jina litalo tambuliwa ulimwenguni.nikisema hivyo simaanishi kama kiswahili ni kibaya la hasha bali soko la ulimwengu limetekwa na lugha ya kiingereza hivyo naweza kusema pmoja nakuwa picha inaelimisha inafundisha inaburudisha lakini pia tupo kibiashara zaidi…

  15. Comment by Rukia masawe on November 12th, 2009 7:59 pm

    Hakuna chochote Mwanaisha, huoniupumbavu wa hali ya juu. Naona umelemazwa na kutekwa kimawazo. In other words you are a slave to the whites. Be proud and make Swahili be competitive.

Leave a Reply