jkuWiki hii mwanasiasa aliyevuma zaidi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania,Jakaya Mrisho Kikwete.Kama umefuatilia vizuri kwenye vyombo mbalimbali vya habari,habari kubwa ilikuwa kuhusu utaratibu mpya aliouanzisha Rais Kikwete wa kuongea na wananchi na pia kuwapa nafasi ya kuuliza maswali ya papo kwa hapo.

Ingawa wananchi wengi wakiwemo pia viongozi wa vyama vya upinzani kama vile Mhe.Dr.Slaa,wanasema Rais Kikwete alipinga chenga au kujibu juu juu sana maswali ya wananchi,mimi nampongeza kwa kuanzisha utaratibu huu. Kama utadumu na kama utakuwa huru(kunawezwa wekwa mamluki wa kuuliza maswali;hakuna linaloshindikana karne hii),naamini ni njia nzuri ya Rais kuwasiliana na wananchi na japo kujua kwa mbali,yanayowakera.Hongera JK! Bado tu kufungua blog na account za twitter,facebook na myspace.Watanzania wengi sana siku hizi wanatumia zana hizo za mawasiliano.Obama yeye anazo zote tayari.

Pamoja na sifa hizo,kuna kitu ambacho kinanifanya nigune kidogo.Kwanini Mheshimiwa Rais amesubiri mpaka umebakia mwaka mmoja kabla ya uchaguzi ndio aanzishe utaratibu huu?Nia ni kusikia kweli hoja na maswali ya wananchi au ndio “kujiweka sawa” kabla ya uchaguzi?

Nini maoni yako kuhusiana na utaratibu huu mpya wa Rais Kikwete?Na je kama uliangalia zoezi zima la hotuba,maswali na majibu,unasemaje?Unampa alama gani Mheshimiwa Rais?A,B,C,D au…?

Feedback / Comments

6 Responses to “MWANASIASA WA WIKI:JAKAYA MRISHO KIKWETE”

  1. Comment by Flora on September 14th, 2009 6:46 am

    I don’t know how longer it takes the Leaders specifically (PRESIDENT) to address the public. May be that were Kikwete’s strategy to put his people as second priority and give fellow leaders first chance. That’s why he is talking to the public now?

    I am sorry I cannot accept to be your second priorities just continue campaigning for the second term Mr. Kikwete, this time I won’t waste my time to stand on the long queue and vote for you. I did not get anything that you promised to do during your first term campaign.Obviously if you will be given another term I don’t expect any changes apart from continuing being fooled by corrupted CCM with their empty promises to much talking zero action.

    I don’t know who is fooling who and until when?

    We are friends when you need something from me after getting what you want you become my enemy.

    No way! Not anymore we need good governance and transparency government.

    Stay blessed!

  2. Comment by Dinah on September 14th, 2009 3:06 pm

    Alivyoanza alikuwa na website ambapo mwananchi ulikuwa huru kuwasiliana nae kwa njia ya Mail, ni vema kapiga hatua ya ujumbe mfupii wa siku.

    Angefanya hivi mara tu baada ya kuchukua majukumu kama Rais ingekuwa vema zaidi, kwa sasa hata mimi nashindwa kujizuia kudhania kuwa ni njia moja wapo ya “kushinda” kura ili aendelee kuwepo kipindi cha pili.

    Kila Rais aliyepita alichukua majukumu ktk wakati mgumu hali kadhalika Kikwete alichukua nchi ikiwa ktk wakati mgumu na anajitahidi kadri ya uwezo wake kuweka mambo sawa, yeye kama mwanadamu hawezi kufanya kila kitu tunachokitaka ndani ya miaka kumi.

    Itachukua muda mrefu sana kusafisha makosa yaliyoachwa na viogozi waliopita, hasa ukizingatia kuwa bado kuna utaratibu wa kulindana.

    Kikwete unajitahidi, lakini je tukupe nafasi ya 2ili umalizie kazi uliyokwisha ianza?
    Kila la kheri!

  3. Comment by Dinah on September 14th, 2009 3:07 pm

    ujumbe mfupi wa simu*

  4. Comment by mwamuzi on September 15th, 2009 7:55 am

    mim nathani CCm kuanguka katika uchaguzi ujao utaisaid wananchi kuamka na nchi nzima kukua na kuamini inawezakana.maana hata viongozi wataogopa,na utendaji kazi wake utakuwa ni mkubwa.rais umeweka watu wengi katika nyathifa hambazo hawaziwezi,yaani ni kujuana tu.udini,uswahli tu.kuna watu kibao waliochini hawajulikani lakni wanafanya kazi zaid ya hao mabos wako na wanauchungu na nchi hii.
    Mimi sikuchukii ila naomba Mungu usipite hata kidogo.kwa niaa njema tu .TUkuwe!

  5. Comment by benne on September 22nd, 2009 6:07 am

    Juu ya mafanikio Tanzania ni neno la Mungu tu litawatoa hapo. Mtachagua mpaka karne ziiishe ila msipoisoma biblia na kuona wafalme wa enzi hizo walifanya nini hambandui hapo.

  6. Comment by Geoffrey on September 26th, 2009 7:25 pm

    Binafsi naona JK kajitahidi sana hasa kwenye swala la ufisadi, it was a dream for something like this to happen, he made it a reality. The problem he’s against all these powerful mafisadi. its a tough battle. Many people expected JK to be easy going and people/leaders thought they could have a walk in a park!.

    I still feel vyama vya upinzani they are still amatures. They seem unstable even before getting full ruling powers. Mimi naona bado upinzania hawapo tayari kushika uongozi, waendelee tuu kwa sasa kuikosoa CCM ili ijirekebishe na wametoa mchango mkubwa sana kwa maendeleo hasa vita ya ufisadi, lakini hiyo sioni ni ticket ya wao kushika nchi. Jamani lazima tukubali kuongoza nchi tena kubwa kama TZ si kazi ndogo, na wananchi in most case huwa tunalaumu tu viongozi.

    “Watanzania, fanyeni kazi kwa bidii, siyo kulalamika na kutemea mimi Rais nifanye kila kitu, ni jukumu la kila mtanzania kujenga Taifa ” – words from President Benjamin W. Mkapa.

    Tayari huko visiwani hali sii nzuri(wapinzani). ni bora nichague CCM ila niwe naamani. Hata wapinzani wakishika madaraka, bado itabidi waongoze serikali, sasa sioni miujiza yoyote watakayo fanya over night nchi iwe na mabadiliko kama wananchi wanavyotarajia. end of the day all these are politics and they can never fulfill everyones demands.

    CCM should work harder, otherwise wananchi watakuwa wamewachoka and the will not care anymore what comes ahead, watataka tu mtoke, so yeyote sasa atashika nchi na hii yaweza leta matatizo kama wapinzani watakuwa hawako tayari kikamilifu kishika nchi, tunaweza kuyumba vibaya zaidi.

    Those are my opinions.

Leave a Reply