MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

abramomich-kilimanjararo-059

Hivi karibuni,tajiri bilionea mmiliki wa timu maarufu ya soka ya Chelsea FC ya nchini Uingereza, Roman Abramovich, alitinga nchini Tanzania na akiwa na nia ya kutalii na kuupanda mlima mrefu kupita yote barani Afrika yaani Mlima Kilimanjaro.

Safari ya Bilionea Abramovich kuja kupanda Mlima Kilimanjaro ilikuwa ni habari kubwa iliyoripotiwa na vyombo lukuki vya habari hususani nchini Tanzania na Uingereza.Kilichoifanya habari hiyo kuwa kubwa hakutokani tu na ukweli kwamba Abramovich ni miongoni mwa watu matajiri sana ulimwenguni bali pia ni ule uhusiano uliopo miongoni mwa mchezo wa soka ulimwenguni huku mashabiki wa timu ya Chelsea anayoimiliki Abramovich ya Chelsea ikiwa na mashabiki kibao ulimwenguni wakiwemo pia wale wanaoishi na kuitazama timu hiyo kutokea Tanzania.

Ingawa Roman Abramovich hakufika kileleni, ni wazi kwamba,kwa namna moja au nyingine,amesaidia kuinua soko la utalii la Tanzania na hususani upandaji wa Mlima Kilimanjaro.

Lakini ni nani aliyemuongoza njia Roman Abramovich? Kuna wadadisi wameuliza swali hili na tuna furahi kwamba jibu lake tumelipata. Aliyekuwa guide wa Roman na rafiki zake anaitwa Isaac Kitindi(pichani juu ndiye anayeonekana kushoto akiwa na Roman.

Isaac ni Mhitimu wa Advanced Diploma katika masuala ya Wildlife Management kutoka Chuo cha Elimu na Utawala wa Wanyamapori cha Mweka kilichopo Moshi,Kilimanjaro. Isaac alikuja Tanzania maalumu kwa shughuli ya kumsindikiza Roman Abramovich mlimani kwani hivi sasa anasomea masuala ya Huduma ya Kwanza (First Aid Training) katika chuo kikuu maarufu cha Havard nchini Marekani.

Isaac Kitindi ambaye wenzake hupenda kumuita Mountain Madness kutokana na umahiri wake wa kuupanda Mlima Kilimanjaro hivi sasa yupo njiani kurejea Havard huku kukiwa na habari kwamba atapitia nchini Uingereza ambapo ataonana tena na Roman Abramovich kwa mazungumzo ya kuileta Tanzania timu ya Chelsea FC hapo mwakani.

Ukitaka kujua ilikuwaje mpaka Roman Abramovich akashindwa kufika kileleni,bonyeza hapa.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

6 Responses to “REMEMBER ROMAN ABRAMOVICH?NOW MEET THE GUIDE”

  1. Comment by Kichwa Bakora on September 19th, 2009 12:25 am

    Hii kali, nampa hongera huyo jamaa kwa kuwa karibu na Roman! Kitu kilichonisukuma kuwasiliana na nyie ni hiyo elimu mnayosema huyo jamaa anasomea pale Harvard! First Aid Training? Huku First Aid wanaitwa First responders or CPR kwa issue kama pressure na vingine na ni course ya few hours tu, saa mawili tu unapewa certificate, huyo mshikaji anadanganya! For one Harvard is expensive, very expensive! It doesnt make any sense kwa jamaa kwenda pale kuchukua course mbuzi kama hiyo ambayo angeweza kuipta in a a community coleges at a cheaper deal!!

  2. Comment by chapombe on September 22nd, 2009 7:41 am

    kazi imeanza

  3. Comment by veyonclate on September 23rd, 2009 1:42 pm

    hahaha…unajua huo ni ukweli lakini…yap big up kwa huyo kaka…but hiyo first aid in harvard..?????..mmhhh…jamani,kamba za miguu hizo…!!!!

  4. Comment by watu on September 25th, 2009 10:00 am

    tatizo letu wengi tunapenda kukosoa na kuelezea vile tujuavyo sisi. kwanza kabisa hilo jina la mountain madness ni jina la kampuni na hawa jamaa kusomea first aid havard ni kitu cha kawaida kwao, coz wanalipiwa na kampuni hivyo watu msije na criticism zenu ambazo hamjazifanyia kazi. huyo wala sio wa kwanza kusomea first aid havard. Na kama kuna watu wanaolipwa hela nzuri bongo ni hao guides

  5. Comment by Fathiyah on October 6th, 2009 2:07 pm

    Jt love roman abramovich dah unaraha u wer near him!!<3<3

  6. Comment by mgalatia on December 20th, 2009 7:57 am

    hizo ni fix nathani hizi ni computer pictures mimi nilikuwa nae kilimanjaro

Leave a Reply