Hii ni collaboration ya Kenya na Tanzania.Wimbo unaitwa Nimetoka Mbali.Ni kutoka kwa msanii Jaguar kutoka nchini Kenya akiwa amemshirikisha wa kwetu wenyewe,AY.Ni mojawapo ya track mpya mpya zinazotamba kwenye vituo vya radio,televisheni bila kusahau katika kumbi mbalimbali za raha.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Feedback / Comments

3 Responses to ““NIMETOKA MBALI”-JAGUAR FT AY”

  1. Comment by Riziki Romwald on September 23rd, 2009 3:39 pm

    Kwa kweli kitu kimetulia.Hizi ndizo kazi tunazotaka,kazi inaonekana imeenda shule.Kuna watu walikaa chini,wakaumiza vichwa,wakajitoa mhanga (fedha)ili kitu kitoke swafi.Hakuna kizuri pasipo ghalama,pasipo maumivu.

    Rangi,sauti (FLOW),mtiririko wa picha na beats vimenatana.Labda logic ya wimbo (UJUMBE) na picha (MATUKIO) kidogo sijaipata ila over all ngoma iko juu.

    Tunataka watu wakae chini, waumize vichwa.Huwezi kila mwezi kutoa single au video (MOVIE) kama rafiki yangu Kanumba,itakuwa poor quality tu lazima.Tujifunze kutulia na kuumiza vichwa.Ubunifu ukiwa juu.

    Nimependa mbali ya kutumia magari ya anasa,wameshoo kwenye mazingira ya kawaida,kutoa picha halisi,sio kujifanya eti mnashootia moven pick ili muonekane mko ulaya.Toa ngoma inayowakilisha mazingira halisia.

    Nawapa Hongera kwa ushirikiano huo,ndiyo mambo tunayotaka haya.Ukiunganisha talents unazaa kitu bora.

  2. Comment by marknigga salamba on September 24th, 2009 12:58 pm

    aya wenye kuimba imbeni.sisi yetu masikio,yes VIJANA TWASONGA MBELE.MABRUK AU HONGERA.makinigga australai

  3. Comment by Pat-Magazeti on October 4th, 2009 10:12 pm

    Great sound track and video.

Leave a Reply