gaddafiKatika anga za siasa wiki hii tunayoimaliza,ilitawaliwa na viongozi wa dunia kupigana vijembe,kufanyiana dhihaka,kuonyesha hasira zao nk kupitia hotuba walizozitoa katika mkutano wa Baraza la Umoja wa Mataifa. Miongoni mwa wanasiasa hao,yawezekana kabisa kukawa hakuna mwanasiasa aliyeongelewa,kujadiliwa na kuzua mijadala mikali zaidi ya Rais wa Libya,Muammar Gaddafi kufuatia hotuba aliyoitoa katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko jijini New York. Ni kwa sababu hiyo ndio maana leo tunavuka mipaka katika ukurasa huu wa “Mwanasiasa wa Wiki” na kumweka Gaddafi.Rais wetu,Jakaya Mrisho Kikwete,naye alihudhuria kikao hicho na alihutubia.

Kwanini “Mwasiasa wa Wiki” hapa BC awe Kanali Gaddaffi? Sababu ni nyingi.Lakini kwa uchache,Muammar Gaddafi ni mwafrika.Hivi sasa anashikilia cheo cha Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika.Kwa hiyo,kwa mapana na marefu,alikuwa akituwakilisha waafrika.Hii ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na mara yake ya kwanza kutembelea/kufika  Marekani.

Safari ya Gaddafi ya kuelekea New York ilikumbana na vikwazo vingi.Kwanza alikataliwa sehemu kadhaa kuweka hema lake ambalo amekuwa akisafiri nalo kila mahali anapokwenda.Huwa hafikii hotelini.Anachohitaji yeye ni sehemu ya kuwekeza hema lake.Ulinzi wake huwa ni wa ma-bodyguard wanawake watupu.Maandamano kadhaa kutoka jumuiya mbalimbali yakipinga Gaddafi kupewa ruhusa ya kuweka hema yalifanyika.”Hatumtaki katika mji wetu wala mtaa wetu” Gaddafi ni dikteta.Mabango kadhaa yaliweka wazi sababu za kumkatalia “mgeni”Ilibidi afikie katika “ofisi” ya kidiplomasia ya Libya.

Yote tisa.Kumi ni pale alipolikwaa jukwaa la Umoja wa Mataifa na kuanza kuhutubia.Gaddafi alihutubia muda mfupi tu baada ya Rais wa Marekani,Barack Obama, ambaye naye ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuhutubia baraza hilo.Gaddafi alikuwa ametengewa dakika 15 za kuhutubia.Alihutubia kwa zaidi ya dakika 90! Wengine walidhani alikuwa akielekea kuweka rekodi ya dunia.Hakuweza kwani mpaka leo mtu ambaye anashikilia rekodi ya kuhutubia Baraza la Umoja wa Mataifa kwa muda mrefu zaidi ni aliyekuwa Rais wa Cuba,Fidel mwana wa Castro.Alihutubia kwa zaidi ya masaa manne(4).

Baada ya hotuba ya Gaddafi,swali kubwa lililobakia miongoni mwa wafuatiliaji wengi wa mambo ya siasa ni “What was he talking about?”. Wengi hawakumuelewa alipotaka,kwa mfano,uchunguzi wa kina ufanyike kutokana na vifo vya aliyekuwa Rais wa Marekani,John F.Keneddy na mwanaharakati maarufu Mchungaji Martin Luther King.Uchunguzi leo hii? Gaddafi alionekana kutokuwa na maandalizi ya kile alichotaka kukiongelea.Hili hata mimi nililiona.Alipanda na vipande chungu mbovu vya makaratasi na mara kadhaa alionekana kusahau alichotaka kusema au alikiandika kwenye kipande gani cha karatasi.Mara kadhaa alijichanganya hususani alipokuwa anaongelea homa ya mafua ya nguruwe ya Swine Flu.

Pamoja na “hitilafu” hizo,yapo mambo ya msingi ambayo Kanali Muammar Gaddafi aliyaongelea.Kwa mfano ni kweli kwamba nchi nyingi wanachama wa UN hivi leo,hazikuwa wanachama wakati umoja huo unaanzishwa.Kwa hiyo,kuna haja ya kuangalia upya muundo mzima wa umoja huo yakiwemo mambo kama vile kura ya Veto.Gaddafi pia aliongelea jinsi ambavyo madhumuni ya kuanzishwa kwa umoja huo yameshindwa.Alisema,kwa mfano,vita zaidi ya 65 vimetokea na vinaendelea kutokea huku umoja huo ambao ulianzishwa ili kuzuia kutokea kwa vitu kama vita,ukiangalia tu.Ukitaka kusoma hotuba na kusikiliza hotuba nzima ya Muammar Gaddafi,bonyeza hapa.

Je ulipata muda wa kuiangalia hotuba ya Gaddafi?Unasemaje kuhusu hotuba hiyo? Gaddafi alitoa uwakilishi ulioutegemea kwa bara la Afrika? Unakubaliana na wanaosema Gaddafi ni mzigo kwa bara la Afrika na sababu nyingine ya kudharauliwa?

Viongozi wengine waliohutubia na kuzua gumzo ni Rais wa Iran,Mahmoud Ahmadenijad ,Rais wa Zimbwabwe,Comrade Robert Gabriel Mugabe na kama kawaida Rais wa Venezuela Hugo Chavez aliyeanza kwa kuomba wasikilizaji wake wasije wakamrushia kiatu ikiwa ni dongo la moja kwa moja kwa Rais wa 43 wa Marekani,George Bush iliyembidi akwepe viatu vya mwandishi wa habari wa Iraq alipokuwa madarakani.

Feedback / Comments

31 Responses to “MWANASIASA WA WIKI:MUAMMAR GADDAFI”

  1. Comment by hombiz on September 28th, 2009 1:47 am

    Huyu Gadafi ni dicteta wa kutupa!
    Inakuwaje dictator kama huyu anachakuliwa kuwa mwenyekiti wa moja wa nchi za Afrika!
    Gadaffi anatwala Libya tangu alipopindua utawala wa ki-falme mwaka 1969.

    Gadaffi amekuwa mfadhili mkubwa wa vitendo vya kigidi kwa muda mrefu sana kw nchi kama Syria, Parestina, Iran, Iraq,Parestine, na Uganda. Ktk swala hili la Uganda, Gadaffi alimsaidia sana dictata mwenzake Iddi Amini, ktk vita vya Tanzania na Uganda. Kwa bahati nzuri jeshi la wanachi wa Tanzania (JWTZ) liliwazidi nguvu na kuwaadhibu vibaya na kama sikosei vikosi vya gadaffi vilitekwa na Tanzania.
    Kama Iddi Amini alivyofukuza wahindi uganda, Gadafi nae alifukuza wayahudi na waitaliano nchini Libya na kutaifisha mali zao.
    Huyu huyu Gadaffi aliandika “Green Book” na kuifanya ndio katiba ya Libya inayolinda maslahi yake.

    Hivi sasa huyu Gadaffi, anamuandaa mwanae Saif Al-Islam kumrithi kiti cha utawala.

    Hivi mtu kama huyu anawezaje kuwa mwenyekiti wa Umoja wa nchi za Afrika!? Sifa za mwenyekiti wa umoja huu zinatakiwa ziwe ni zipi!?

    Kwa mtazamo huu, mimi naamini kuwa demokrasia haina nafasi Afrika. Kinchoendelea Afrika ni siasa za kifisadi, ukandamizaji, rushwa, uhujumu, kulindana na kutothamini utaifa au uafrika kwa viongozi wa nchi hizi za afrika walioko madarakani. Na sitashanaa mwakani nikisikia kuwa Mugabe ni mwenyekiti wa umoja huo.

    Hotuba aliyoitoa Gadaffi ktk UN ni ugoro mtupu usiomsaidia mwafrika kwa lolote. Kiongozi wa kweli mwenye uchungu na Afrika angeongelea:

    1. Afrika inavyojipanga kupambana na matizo sugu la umasikini, njaa, ujinga, na maradhi na mbinu za kuanza kutatua matatizo hayo bila kutegemea misaada zaidi kutoka nchi za magharibi.

    2. Angelaani vitendo vya kinyonyaji vinavyofanywa na mashirika ya fedha ya kimataifa na jinsi Afrika kupitia umoja wake inavyojipanga kukabiliana na dhahama hiyo.

    3. Angependekeza utawala bora wa sheria na ukuzaji wa demokrasia kwa nchi za Afrika na waafrika wote kwa ujumla.

    4. Angezungumzia kuundwa kwa soko moja la Afrika ambalo lingesimamia ununuaji na uuzaji wa bidhaa za kutoka na kuingia Afrika kwa maslahi ya Afrika.

    Hawa viongozi wa Afrika hawako madarakani kwa kuzitakia nchi zao mambo mema kwa kuwajali wanyonge. Badala yake wamegubikwa na tamaa ya mali na maslahi binafsi huku wakilewa sifa na madaraka kwa kusahau sifa za kiongozi wa kweli.

    Hayati, mwalimu Nyerere na Kwame Nkurumah, walipokuwa wakiongea, dunia alisikiliza kwa makini. Kwani walijua kinachoongelewa si pumba. Lakini upuuzi wa hawa mafisadi wa siku hizi, hakuna anayetaka kusikiliza.

    Huyu mjinga Gadaffi alitaka kupeleka mahema marekani badala ya uleta point za maana.

    I hate this dishonest leaders and dictators!

  2. Comment by hombiz on September 28th, 2009 1:53 am

    Imeant i hate these dishonest leaders and dictators. Afrika ikipata viongozi wa kweli, itaendelea kwa kasi kubwa sana tena kwa muda mfupi!

  3. Comment by duu. on September 28th, 2009 7:53 am

    bwana wewe mbona Gadaf alieleweka vizuri tu eeh.
    Ama ndo desturi yetu tena watanzania kuangalia mapungufu badala ya mantiki inakuaje hii jamani eeh.
    Link ya UN imetoa summary nzuri tu ya jinsi Gadaf alivyoongea mbona hivyo jamani eeh.

    Tuangalieni mantiki ya mtu ana maanisha nini badala ya kuangalia mapungufu ya mtu jamani watanzania wenzangu inakuaje hii haijakaa sawa jamani

  4. Comment by mwaipopo on September 28th, 2009 8:36 am

    how did this african dictator creep into ‘bongo’(tanzania) celebrity blog?

  5. Comment by muhogo mchungu on September 28th, 2009 11:23 am

    Wewe Hombiz,

    Umelishwa sumu na media ya west hasa hasa Marekani, Gadaffi ni kati ya viongozi wazuri Africa ambaye ni mtu wa ,msimamo bila kuyumba,

    Kiongozi yeyote wa Africa hasiye kubali kuburuzwa na Marekani huwa anaitwa Dictator. Mugabe na Gadaffi ni viongozi wazuri lakini uwezi kuona maana umepofushwa na media ya wazungu, wenye macho hawawezi kuona na wanyemasikio hawawezi kusikia

    Hongera Gadaffi, Kiongozi Gaidi wa Marekani yaani George Bushi apelekwe mahakama ya Kimataifa , Bushi ni Gaidi

  6. Comment by shekallaghe on September 28th, 2009 9:52 pm

    inavyoonekana muheshimiwa wa bc una kaudini kidogo kwa kuwa watu uliowataja ama ni waislam au ni watu wanaochukiwa na wakristo(marekani).sioni kama rais wa irani alichemka kwa kuwa huo ni mtazamo wake na hata gadafi ni mtazamo wake labda unaogopa kwamba africa hatutapewa misaada kutokana na gadafi kuwa kiongoza na ni muislam lkn si kwakuwa aliongea pumba no no non.

  7. Comment by BLACKMANNEN on September 28th, 2009 11:12 pm

    Msitufanye sisi Waafrika kuwa hatuna akili. Gaddafi na Mugabe ni Viongozi wetu wa Afrika.

    Msiwafanye viongozi wa Afrika kuwa hawana akili kwa kumweka Gaddafi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika.

    Wala msidhani kuwa viongozi wengi wa Afrika hawana akili kwa kumwunga mkono Mugabe katika kuchukua mashamba ya wazungu na kuwagawia Wazawa hata kama ni pamoja na kumgawia mkewe mashamba hayo, na yeye ni Mzawa vile vile.

    Ni kitu cha kuchekesha sana ninapowaona watu (makabwela wenzangu, waliotoka Afrika) wanauvaa Umarekani, wakati Wamarekani wenyewe hawawathamini.

    Kiongozi yeyote duniani anapowatolea uvivu Wamarekani na washirika wake. Watu wanaanza kuwanyoshea vidole hata makabwela wenzangu wanakubali kuwa vibaraka wao kwa kuwatukana hadi viongozi wao wa Afrika.

    Marais wa Iran na Venezuela kama ilivyo kwa Gaddafi na Mugabe wanaonekana kuwa ni viongozi madikteta na magaidi. Mbele ya macho ya Wamarekani na washirika wake ikiwa ni pamoja na vijibwa vyao pembeni vinabweka.

    Je, ni Gaddafi au Hugo Chavez au Mugabe au Ahmednajad waliyemtengeneza kiongozi wa Al-Qaidar “Mzee Osama?”.

    Je, ni Gaddafi au Mugabe wanayeendeleza kuwatesa watu wa Iraq na Afghanistan?

    Najua sisi wengine tunajikuta tunaikumbatia Marekani na Washirika wake, ili tupate makaratasi ya kuishi huko. Tunafikia hadi kujitukana wenyewe.

    Hapa nilipo najiuliza kuwa, kama wenzangu na miye hawa, wanaowaona hadi Viongozi wetu wa Afrika hawana akili na hawafai kuongoza nchi.

    Kwanini wao wasichukue Uongozi wa nchi hizo (Walizotoka huko Afrika), badala yake nawaona wanazurura katika nchi za wenzao na kujikita kujipendekeza kwa kuwasifia Viongozi wa nchi hizo?????

    Usidharau kwenu hata kama ni kubaya. Waafrika bado tunayo safari ndefu sana ya maendeleo na ili tufanikiwe kuifupisha, ni muhimu tupendane na tushirikiane sisi wenyewe kwanza.

    Tusikubali kuchaguliwa Viongozi wetu na watu wengine. Viongozi tunaowachagua sisi ndiyo tunaowataka na tunawapenda na kuwaheshimu.

    Viongozi wetu hawa waheshimiwe pia wanapokwenda katika nchi zingine kama vile Amerika na Washirika wake.

    Sio nchi nyingine inawatumia barua za vitisho vya kuwazuia kuingia katika nchi zao, wakati Viongozi hao wala hawajaomba kwenda huko.

    It’s Great To Be Black=Blackmannen

  8. Comment by mr degree on September 29th, 2009 10:05 am

    hombiz!mimi nilibahatika kuangalia hotuba yake na ingawa haikuwa katika mpangilio mzuri lakini hisia zake kwa mataifa kandamizi zilieleweka kabisa. alizungumzia uwepo wa kura ya veto katika securuty council na alizungumzia pia vitendo vya kinyonyaji vinavyofanywa na mashirika ya fedha ya kimataifa.hapa kosa lipo wapi? veto ndio iliyomkosesha mtanzania salim ahmed salim kuongoza UNO,na mashirika ya fedha ndio hayo yanayotukopesha kila siku na tunalipa kwa riba inayotuelemea! hayo yote aliyaongea! tatizo la waafrika wanataka ufundi wa kusoma hotuba na ndio maana kila siku tunaibiwa tuu na wanasiasa! hombiz badala ya kuchanganua contents ya hotuba yake wewe unazungumzia hisia zako juu ya gadafi na mugabe! hivi uliifuatilia hotuba yake? leo hii ukitaka vyombo vya magharibi vikuone mbaya basi pingana nao na ndio maana hata mugabe na gadafi wanaonekana hovyo, na mbaya zaidi hata waafrika wenyewe kina hombiz wamekuwa vibaraka wazungu na kuita viongozi wetu wanaothubutu kukemea wazungu wanaongea UGORO! mimi naomba BC uweke na mahojiano ya Mugabe na Cristian amanpour ya wiki iliyopita tuione halafu wapuuzi wengine ndio watafunguka macho!

  9. Comment by hombiz on September 30th, 2009 2:20 am

    Nyinyi critics hapo juu hebu ondoeni uzarendo usiokuwa na maana ktk wanja hili la BC. Ni nani dunia hii, “hata bila ya western Media”, asiyefahamu kuwa Gadafi ni dicteta? Kusema kwake ovyo ndani ya UN hakumpi credits za yeye kuitwa kiongozi bora Afrika hata sekunde moja. Tittle yake ya kuwa dicteta atabaki nayo mpaka kufa.

    Hili jitu limejisimika madaraka nchini kwake tangu mwaka 1969 mpaka sasa na linanyonya wananchi wake kama halina akili nzuri. Mbali na hapo, limekuwa likiendesha ugaidi wa kuuwa watu wasio na hatia kwa miaka mingi halafu nyinyi mnaliita zalendo! Mbali na hapa wazembe nyie mnataka tusilikemee kisa tutaonekana vibaraka ikiwa tutafanya hivyo. Are you serious! You guys really need to go sit down somewhere and shot the hell up!

    Dictator ni dicteta tuu. Awe ametokea Ujerumani kama Hitler au Libya kama Gadaffi, dictator lazima apewe tittle yake.

    Mbona huyu mtu alipokuwa akimsaidia Iddi Amini katika vita kati ya Tanzaia na Uganda hamkujitokeza na kumuita ni shujaa wa Afrika kama kweli hivyo ndivyo mnavyoamini!? Suppose alipomsadia Amini, Amini angeshinda vita ile ninyi mngekuwa wapi na mkiwa na mitazamo gani hivi sasa!? Huyu Gadafi ana faida gani kwa Afrika tangu alipopindua nchi mwaka 1969 zaidi ya ugaidi, kuiba na kujilimbikizia mali! Come on people, you need to think constructively. Hizi propaganda za kisiasa za viongozi wa Afrika ndizo zinazofanya umoja wa nchi za Afrika uwe hauna meno.

    Kila ninapowaambia waafrika wenzangu ukweli, mnakimbilia kuniita eti kibaraka wa wazungu au nimekuwa brainwashed na western media. Msichokielewa juu yangu ni kwamba mimi ni mtanzania mwenye machugu ya kweli na nchi yangu na sio bla bla zenu zisizo litakia bara la Afrika mambo mema yenye neema kwa mamilioni ya watu wake ambao wanaishi ktk dimbwi kubwa la umasikini kutokana na tamaa za viongozi wake waliokamata usukani.

    Watanzania na waafrika wanzangu wenye mapenzi mema na bara hili la Afrika, mnapaswa mtambue kuwa maendeleo ya Afrika yataletwa na sisi waafrika wenyewe na si mataifa yaliyoendelea. Misaada ya wafadhili haiwezi kutukwamua ktk umasikini hata siku moja. Badala yake, itatufanya tuzidi kudharauliwa na nchi zilizoendelea, na kuwa tegemezi zaidi.

    Mwalimu Nyerere alipotuhimiza juu ya sera za ujamaa na kujitegemea, tungemsikiliza kwa vitendo, leo hii tungekuwa mbali saaana. Palipo na ujamaa, hakuna unyonyaji, ufisadi, uhujumu, matabaka ya watu(matajiri na masikini) na hata udini. Penye ujamaa watu huishi pamoja na kuheshimiana, kusaidiana na kupendana kwani umoja ni nguvu utengano ni udhaifu. Kungekuwa na ujamaa wa kweli wa waafrika, viongozi vibaraka wa nchi za Afrika wasingeweza kujitokeza. Nchi za kibepari zingeshindwa kupandikiza viongozi vibaraka sababu ya ujamaa uliokomaa. Kungekuwa na umoja wa waafrika, waafrika wasingekubali kupokea siraha toka kwa nchi zilizoendelea na kuuwana wao kwa wao huko Rwanda, Burundi, Somalia, Uganda na kwingineko.

    Na kwakujitegemea, kila mtu angefanya kazi yake kwa juhudi na maarifa kwa maslahi ya Afrika. Walimu wangefundisha kwa juhudi na maarifa, madaktari wangetibia kwa juhudi na maarifa. Viongozi wangeongoza kwa juhudi na maarifa. Kila mtu angewajibika kiufasaha kulingana na nafasi yake na hatimaye Afrika ingeushangaza ulimwengu.

    Lakini kwa kuwa Afrika hakuna ujamaa na badala yake umimi na ubinafsi, ndio maana Gadaffi na Mugabe wanaonekana mashujaa. Kwakuwa Afrika kujitegemea bado ni msamiati, basi kuombaomba toka nchi zilizoendelea kunabaki kuwa ni jadi.

    Tufumbue mamcho na akili pia!

  10. Comment by shekallaghe on September 30th, 2009 12:02 pm

    nadhani bado sitakosea kama nitasema ww hombiz una chuki uliyorithishwa ama na wazazi wako au viongozi wako unajua mambo ya unayooyaita demokrasi ama vyama vingi yameletwa na hayo mataifa ya magharibi?.sheria za utawala za nchi za kiarabu ni tofauti na nchi za kimagharibu basi kwa mtazamo wangu hata baba yetu wa taifa alifaaa kuitwa dicteta kwa kuwa aliongoza kunzia 61 mpaka alipong’atuka zaidi ya miaka 20.je hulioni hilo?.waarabu wana tawala zao za kifalme na hawawezi kufuata sheria za nchi za magharibi.ila hayo ni maoni yako lkn kwa mtu asiyekuwa mtumwa wa kimawazo anautambua ukweli uko wapi.

  11. Comment by mr degree on September 30th, 2009 1:04 pm

    hombiz hana uwezo wa kuchanganua mambo kwa kutumia akili yake! naona anaamini kila kinachoonyeshwa kwenye TV na kilichoandikwa kwenye vitabu. kwa hiyo waki mis lead naye amekwenda na maji.inawezekana hafahamu kuwa wazungu waliitawala zimbabwe mpaka kwenye miaka ya 80 na haelewi chochote kuhusu lancaster house! kazi ipo!na sidhani kama anakumbuka wale wazungu waliowapandikizia kwa makusudi virusi vya ukimwi watoto wadogo wa Libya!nadhani hombiz ndio wale wanaoamini kuwa Gaidi ni mwarabu na mzungu si gaidi!sio vizuri sana kumlaumu kwa kuwa upeo wake ndio umekomea hapo!

  12. Comment by shekallaghe on September 30th, 2009 5:42 pm

    NAJUA HUTAKI KUTOA MAONI YANGU LKN UKWELI NDO HUO NAJUA UMESHASOMA NA KUELEWA.

  13. Comment by hombiz on October 1st, 2009 1:31 am

    Wewe Shekallage ndio hamnazo kabisa! Hivi haufahamu kuwa mfumo wa elimu wa Tanzania, mfumo wa bunge, na serikali ya Tanzania vimetengenezwa kwa kufuata tuiga toka kwa Wazungu hao hao unaowakataa wewe!. Hao viongozi wa nchi yako wamesomea wapi!? Arabuni au ulaya na marekani! Hivyo vitabu vinavyotumika vyuo vikuu kwa taaluma mbalimbali vimeandikwa na nani!? Babu yako, waarabu au wazungu wa maghalibi!?

    Kwa upande mwingine, mwalimu Nyerere naamini aliona mbali ndio maana akaamua kung`atuka baada ya kutawala kwa muda huo mrefu na kuamua kuruhusu mfumo huo wa vyama vingi na wa kidemokrasia ulioletwa na mapinduzi ya kidemokrasia hasa baada ya cold war kusambaratishwa na Taifa la marekani.

  14. Comment by hombiz on October 1st, 2009 2:35 am

    Mr. Degree wewe degree yako ni ya kufuka! Hakuna asiyekufahamu toka awali. Mimi napembua mambo kiyakinifu na sio kidhanifu kama wewe!

    Wewe Mr. Degree, wazungu walitawala zimbabwe kwa muda mrefu kwa njia ya mabavu. Lakini hatimaye utawala wa Zimbabwe huru ulipatikana chini ya Mugabe ambaye baada ya kulewa madaraka hapo baadaye, akageuka mwehu na ku-abuse office na kuwa dictator.

    Pamoja na u-dikteta wake, mimi ningemuna Mugabe kuwa ametumia elimu yake vizuri kidogo kama angewaelimisha wazawa wake juu ya elimu ya kilimo bora kabla hajawanyang`anya wazungu hayo mshamba na kuwapa wao wazawa wake. Kwakuwa alifanya kinyume chake, matokeo yake sasa wazawa wameshindwa kuyaendeleza mashamba ipasavyo na hivi sasa watu wanakufa kwa utapiamlo. Nchi kama Zimbabwe ni nchi ya mtu kufa na njaa kweli kutokana na neema ya ardhi bora iiyobalikiwa!?

    Pia wewe Mr Degree ni lazima ufahamu wazungu wengi waliingia huko Zimbabwe miaka mingi sana. Wengi wao wamezaliwa Zimbabwe na kwa hiyo nao ni wa-zimbabwe. Ingekuwa kila kiongozi ana mtazamo mbovu kama wako, basi hata Nyerere angewatimua watanzania woote wenye asili ya nchi za Magharibi na Asia, na uarabu. Unataka kuniambia kuwa Watanzania wenye asili ya Sultan Sayyid Said mtawala wa Oman na Zanzibar wanapaswa kutimuliwa Tanzania? Huyu sultan si alifanya biashara ya kununua na kuuza watu kama bidhaa! Mbona Mwl Nyerere hakutumua kizazi chake toka Tanzania!? Si nao wana mlighafi kibao tu wanazomiliki Tanzania!?

    Hebu nyinyi watanzania wachache wenye mawazo ya kimasikini, kibinafsi, na kijinga amkeni na mtoe comments za maana zilizolenga kujenga Tanzania na Afrika yote kwa ujumla, badaya ya kuleta bla bla za kibwege hapa!

    Mugabe na Gadaffi ni Ma-dictator!. They`re not valuable for Africa!

  15. Comment by raphkim on October 1st, 2009 6:25 am

    mmmh kiuakika huyu ni mwafrika aasilia,wanaodai ni dicteta ni mafisadi na watu wabaya kwa afrika ya leo.jamani Africa bila huo tunaouita udicteta haiendi maana democrasia imelea mafisadi na wezi wa haki za wanyonge.udicteta wenye lengo la maendeleo ni mzuri kwa bara hili tajiri linaloishi umaskini uliopitiliza.jamani Africa ni yetu tuwe na mtazamo chanya wenye kulenga ukweli hata kama tutaonekana madicteta.Gadaphi ni mfano mzuri tu kwetu tuangalie malengo yake na mazuri mengi aliyofanya kwa Libya .kila la kheri mwana Africa.

  16. Comment by Geoffrey on October 1st, 2009 10:49 pm

    jamani ghadafi hazeeki huyu jamaa, yupo hivi hivi miaka yote.

  17. Comment by shekallaghe on October 2nd, 2009 11:12 pm

    hivi ww hombiz kwa akili yako unajua nchi z kimagharibi ndo kila kitu au wazungu ndo wakunyenyekewa?.lkn si makosa yako ni ulimbukeni,utanambia nn nchi kama china,japan,france,korea,urusi irani, israel na nyenginezo ambazo ni super power ambazo zina kila kitu chao kuanzia lugha mashuleni wanatumia lugha za kwao,ni hao wazungu waliokuja africa kwa muamvuli wa dini kwa kutupumbaza kisha wakutuchukulia ardhi yetu.hata kama wasingekuja wazungu watu pia wazee wetu wengesoma kwa kuwa wazungu elimu waliokuwa nayo pia wameiga kwa watu wa vitabu.utaniambiaje kuhusu ivory coast,burkina faso na mali ambazo lugha zao ni kifaransa kwa hiyo hawa ni mataahira kwa kuwa hawakusoma kizungu?.acha chuki uliorisishwa na wazazi wako pamoja na viongozi wako ambao ni mafinyu wa akili.

  18. Comment by shekallaghe on October 3rd, 2009 1:07 pm

    imejionesha dhahiri kwamba ww chuki zako ni waarabu na sio gadafi.kwa kuwa tuu baba yako na baba yako wa taifa wamesomeshwa na wazungu.lkn nataka tena ujue kwamba wazungu si kila kila kitu kuna madaktari na wasomi wengi tuu ambao wanajulikana ambao hata salamu ya kiingereza inawashinda na ni wasomi wakubwa.kwa ushauri wangu acha kasumba ya chuki na uwe mpenda haki si kusikiza maneno ya wajinga na kuyabeba bila kufanya uchambuzi yakinifu,au unafikiri ulivyokuwa ww na ss wote ni sawa?.

  19. Comment by hombiz on October 4th, 2009 3:20 am

    Ktk jitu zoba wewe Shekallaghe ni mmoja wapo. Hapa ulileta mada ya Afrika na ma-dikteta wake kama Ghadafi. Kwenye kuwa mimisikukubaliana na u-dikteta wao na sera zao zisizo na faida kwa Afrika, hilo likakusumbua sana. Labda wewe ungependa kuwa kibaraka wao sina hakika. Still hao ni madikteta na sifa yao hiyo itawafuata mpaka kaburini.

    Nikianzia na nchi ya Iran, ngoja ni update your knowledge kidogo. Kwa taarifa yako jeuri ya ilani kwa sasa, inatoka Urusi. Hawa urusi ndio wafadhili wakubwa wa siraha na vifaa vya kijeshi ktk nchi ile. Iran ina wataalamu wengi sana ambao wamesoma nje ya nchi ambazo Marekani ni mojawapo. Wanapomaliza masomo, wataalamu mbali mbali wanarudi nchini Iran na kutumikia nchi yao ktk fani mbali mbali.

    Pia ni vema ukafahamu kuwa ili nchi iitwe superpower, nilazima iwe ktk nafasi ya kuongoza mataifa mengine ktk mfumo wa kimataifa. Na ni lazim iwe na nguvu kubwa za kijeshi na kiuchumi pamoja na influence kwa mataifa mengine duniani. Pia lazima iwe na uwezo thabiti wa kutetea na kulinda influence zake duniani. Nchi hiyo pia ni lazima iwe na uwezo wa ziada ukilinganisha na nchi nyingine. Mtu yoyote anayefuatilia masuala ya siasa za kimataifa kiufasaha, hatashindwa kubaini kuwa nchi zilizokuwa super powers ni mbili ambazo ni Soviet Union na USA. Baada ya Soviet Union kusambaratika, U.S.A. ikabaki kuwa Superpower.

    Shekallaghe, ujinga wako bakia nao mwenyewe! How can you call Iran a superpower!? Labda kama unamaanisha superpower ya Middle East, hapo nitakuelewa. Nchi ya Korea, kilanja wao ni Urusi. Lakini bado haina hadhi ya kuitwa superpower for now!

    Halafu ulivyo mpuuzi zaidi, umeichanganya Israel ktk mfano wa nchi wewe unazoziita superpower zisizotegemea marekani. Nakupa homework ndogo tu nayo ni-”nenda kajifunze juu ya mahusiano ya U.S.A. na Israel baada ya hapo uje unieleze umejifunza nini juu ya mahusiano ya nchi hizi mbili.

    Shekallaghe, Burkina Faso na Ivory coast zilipata uhuru wake mwaka 1960 toka France ambao ni wazungu wanyonyaji pia.
    Mfumo wa elimu wa nchi hizo mbili una-infuenc kubwa ya wafaransa na lugha ni kifaransa. Nchi hizo mbili nazo hazijaendelea kama zilivyo nyingine za Afrika zilivyo na udikteta. Ni vema ufahamu kuwa raisi wa sasa wa Burkina Farso (Blaise Compaore), alichukua nchi kwa mapinduzi na kumuua aliyekuwa rais wa nchi hiyo ajulikanaye kama Thomas Sankara, October 15, 1987. Mauaji hayo yalikuwa ni maagizo toka France nchi nchi ya wazungu ambayo wewe Shekallaghe unadhani ni superpower.

    Shekallaghe, ni vema sasa ujue kuwa mandeleo ya Japani, hasa ya kiteknolojia, yametokana na fidia kubwa ya marekani kwa nchi hiyo, hasa kutokana na mauaji makubwa ya raia wema yaliyofanywa na jeshi la Marekani wakati wa vita vya pili vya dunia. Bomu lile lilikuwa ni la nuclear ambalo marekani inapinga kutengenezwa tena na nchi yoyote na kutumika duniani kwa mauaji ya kadamnasi ya watu hasa wasiokuwa na hatia.

    Mjinga, hujua kamba hajui, lakini mpumbavu hajui kwamba hajui.

    Wewe Shekallaghe, hujui kwamba hujui!

  20. Comment by shekallaghe on October 4th, 2009 9:23 pm

    we hata unachokiongea hukijui ila akili yako ya kitaahira inakutuma kwamba tangu mungu alivyoumba ulimwengu basi hakuna watu wenye akili na wa kuigwa kama wazungu kwa kuwa ni mabwana wa baba zako na babu zako.unajua hao wazungu unawaona ww n bora hiyo elimu yao wameipata kutoka wapi?au hao wamerekani unadhani nchi yao inaendeshwa na nani kama si wageni hasa waisraeli ndo wanaoiendesha marekani katika kila nyanja.unajifanya unajua historia ujinga mtupu uliojazwa kichwani mwako wa chuku,na ndio nyinyi mnaosema pia mtu wa kwanza kuvumbua africa ni mzungu wkt wazee wetu walikuwapo kabla ya kuja hao wazungu ila watu kama nyinyi ndo vibaraka wa mashetani.

  21. Comment by shekallaghe on October 4th, 2009 9:30 pm

    hapa si suala la kiingereza hapa ni suala la nani mjuzi.kwa mfano urusi lugha yao si kiingereza lkn kama ulivyosema wanawafundisha irani hilo ni kweli,israel wana lugha yao lakini wanawafundisha marekani fani mbali mbali kwa kuwa wao ndio waliokuwa wa kwanza kupelekewa elimu na mungu ya kila kitu.kwa hiyo unapojisifia kwamba chuo kikuu unasoma kiingereza baada ya lugha nyingine ujue kwamba hao wazungu wenyewe mambo mengi wameiga kutoka kwa watu wa vitabu.wazungu ni watu wenye fitna na wana kila njia ya kukurubuni wajinga kama nyinyi kukubali kila walisemalo ni sawa,ngoja nikuulize kwanza unajua kwanza chuo kikuu cha kwanza ulimwenguni kilikuwa nchi gani ulaya au uarabuni?.au hesabu za kwanza aljebra unajua ni nani muanzilishi?.we bana kalagabao na ujinga wako tuangalie mambo mengine.

  22. Comment by Bingo on October 5th, 2009 3:57 am

    I will never forget when gaddafi sent a plane full of commanders to bomb Tanzania during Tz Vs UG war. Since then I have never trusted him. I think I am tired of hearing about him, cause he is obviously a wild terrorist, ethically challenged and a crooked politician. I also saw a part of his speech on CNN, and I could tell from it that he is a piece of useless humanity, and he was un-intelligible when he was talking and was obviously as senile as a rat. Its sooo sad to see how is fooling Africans into thinking he is great, while the truth is, he wants to bossy Africa. He should go to hell and leave us alone, those days are over and we are lever than he realize.

  23. Comment by A on October 6th, 2009 8:10 am

    Hivi wewe unayejiita Hombiz umetokea wapi? Mbona waajabu hivyo? Nilini umesikia Gaddafi amejilimbikizia mali. Hata hayo mahema asingekuwa anatembia nayo. Binafsi naona ushabiki mwengine kama huu wa Hombiz nadiriki kuuita wakijinga. Naona nobora kuwa na kiongozi kama Gaddafi hata kama atakaa madarakani milele na rushwa isiwepo kama kulivyo Libya kuliko tanzania ambako kumejaa wezi wakubwa (mafisadi) kila kona ya nchi. JK amejitahidi lakini wapi, bado wapo tu kwani hata wengi wao wa hao waliomzunguka ni mafisadi.
    Ni wazungu haohao waliomwadika Mzee wetu Mandela kwenye kitabu cheusi kisa anapingana na ubaguzi wa rangi. Ni haohao waliokuwa wanamwona The late Mobuto seseseko kuwa nikiongozi mzuri huku waZaire now DRC wakiteseka. Ni haohao waliomwona Mzee Mgabe ni mzuri kwa kuachia mshamba na wazungu lakini pale alipoamka na kuona ataondoka duniani akiwaacha wazimbambwe hawa ardhi (watumwa) akaonekana afadhali hata ya kinyesi. Hivi wewe Hombiz ni wawapi? nauliza tena bila shaka mtanijibu.

  24. Comment by Hombiz on October 7th, 2009 3:01 pm

    BC kwa nini huko post comment yangu juu ya huyu mpuuzi shekallaghe!? Acha niwahabarishe wajinga wanaotetea uzembe wa hali ya juu.

    Jingine hilo lime-post comment ya mwisho hapo juu. Sijuwi kwanini halichukui muda kusoma ninachosema ili lielewe ninamaanisha nini ninapochambua mambo kiyakinifu. Lingekuwa linafuatilia comments zangu vizuri, bila shaka lisingediliki hata kuniuliza eti mimi Hombiz natoka wapi.
    Hayo yote uliyoyaandika hapo nilishayazungumzia siku za nyuma kiufasaha kabisa. Kayasome ujielimushe!

  25. Comment by Bingo on October 8th, 2009 8:00 am

    ha ha haa home business why are you sooo freakin’ angry??

  26. Comment by shekallaghe on October 9th, 2009 8:00 pm

    haya hombiz mjadala upo kwa dubu mkapa sasa,unajua nn hombiz hoja zako si yakinifu ni za kichizi ndo maana mtu yyte mwenye akili timamu na asiyekopy na kupaste kama ww usiyekua mchambuzi bali unakula bila kuchambua pumba hapati tababu kuona mapungufu yako uliyonayo.ww uliyofundishwa ni hayo hayo basi utafakari wala kujudge ukweli wa mambo.sidhani kama unavyodhani ww na mtazamo wangu ni zaidi ya mtazamo wako na si kwamba watu humu ndani wanakupinga kijinga kwa ushindani nah, humu hakuna mjinga wala mpumbavu kama unavyofikiria ww bwana mkubwa.kuna watu hawajaenda shule lkn wana degree na masters humu za mtaani,

  27. Comment by Hombiz on October 14th, 2009 2:20 pm

    Shekallaghe hata hiyo degree ya mtaani wewe huna. Elimu inaitwa ni elimu kweli kama itakufaa wewe na jamii iliyokuzunguka. Cha ajabu elimu yako unayoizungumzia, hata wewe mwenyewe haikufai. Sasa ni elimu gani hiyo!? Wewe ni galasa!

  28. Comment by BLACKMANNEN on October 14th, 2009 8:39 pm

    Hombiz,

    Hapa ni uthibitisho tosha wa “ukiwete” wako katika kutoa hoja zako sehemu zote.

    Unaona jinsi watu wanavyokushambulia. Badala ya kujifunza makosa yako, unajitahidi kutetea hoja zako UTUMBO kwa bidii zako zote.

    Uwe unakubali kushindwa, unapoona umeboronga. Hapo ndipo utakapoheshimiwa na wenzako hapa. Hatuko hapa kushindana.

    This Is Black=Blackmannen

  29. Comment by Hombiz on October 21st, 2009 7:33 pm

    Kilichonishinda kitu gani hapa wewe juha! Yaani wewe na ufinyu wako wa akili unadhani mimi nitasema oooooooh, kwakuwa wapuuzi hawa wengi wanamfia dikteta Gadaffi basi bora nami nimwage manyanga na kukubaliana nao. Pumbavu, hata mje 1000, speed yangu ni 120 ktk kutetea hoja za msingi zisizo na ushabiki wa kijinga. Watu wenye akili zao timamu, wananielewa nnachokiongea kila nnapomwaga hoja zenye ukweli na zisizo na woga au sifa za kinafiki.
    Usicheze na umeme wa radi, utageuzwa majivu!

  30. Comment by Keynez on October 31st, 2009 3:52 pm

    Kwanza, mimi hii ni mara yangu ya kwanza kuandika maoni kwenye website hii.

    Sasa, kuhusu Kanali Ghadhafi, ninaweza kukubaliana na baadhi waliosema kwamba ni muhimu kujiuliza kwa makini kama Mzungu ni mtu wa kumsikiliza linapokuja suala la morality (kwa haraka sina neno la kutafsiri kwa kiswahili, ubinadamu?). Hapa naongelea masuala ya rushwa, amani, uongozi, demokrasia n.k kwa sababu ukiangalia historia ya maraifa haya ya magharibi, ndani ya nchi zao, au katika uhusiano na nchi zingine utaona kuna kujichanganya na hypocricy kubwa. Mzungu ni mtu hatari sana. Mimi nimeishi nao, uwezo wao wa kufikiri ni mkubwa sana, lakini kinachosikitisha hawautumii vizuri, badala yake wanautumia kukandamiza watu wengine na kutake advantage kila wakipata nafasi, hii inajumuisha kudanganya na kuwachafua watu wengine, naongelea hivyo from personal experience na siyo mambo ya kusikia.

    Mimi nadhani in due time, inaweza kuwa miaka 20 kutoka sasa au miaka 1000, ukweli utakuja kujulikana. Waafrika ipo kwenye desturi na imani zetu kwamba kisasi si lazima kimtokee mtu akiwa hai, kinaweza kutokea hata vizazi vitatu vijavyo, nadhani mtakubaliana na mimi. Malcolm X na Reverend Wright alivyowaambia wamarekani kwamba ‘it’s a case of chicken coming home to roost’ waliwashambulia, lakini hiyo ni imani ya kiafrika, labda kweli hawaelewi, what goes around comes around.

    Hii issue ya kusema kiongozi fulani ni dikteta kwa kuwa eti amekaa madarakani miaka fuali ni ulimbukeni tu na kutoelewa mambo. Tanzania kesho tukiamua kuwa na Raisi wa maisha lakini tukawa tunachagua Waziri Mkuu kila miaka mitano kutakuwa na ubaya gani? Kama hakutakuwa na ubaya, nani amesema demokrasia pekee ni kuwa na uchaguzi wa raisi kila miaka 4? Afrika tunaweza kuamua kwa pamoja kuwa na Mfalme na system tofauti kabisa ya uongozi inayojali uwajibikaji, lakini unadhani Mmarekani atakubaliana nayo?

    Nina mengi ya kuelezea lakini nitaachia hapo kwa sasa.

  31. Comment by shekallaghe on November 1st, 2009 4:18 pm

    kweli waswahili wanamsemo mmoja unaosema sikio la kufu halisikii dawa.nadhani keynez utakuwa umemaliza kila kitu.na pia kuna msemo mwengine wanasema ushauri wa wengi ni ushauri wa mungu,mfano wa watu wanaompinga kadafi ni sawa kwao hata ukiwaambie sasa hivi rais ni kikwete wao watakuambia nah sio kikwete ni nyerere kama alivyo hombiz.

Leave a Reply