Huwa najitahidi sana kwenda na wakati. Huwa napenda kutambua misamiati,misemo na vijineno vipya vinavyoibuka na kuanza kutumiwa mtaani.Lugha zote ulimwengu hukua kutokana na kuingia kwa misamiati na misemo mipya.Muziki,ukiwemo huu tunaouita wa “kizazi kipya” bila shaka unachangia sana katika kukua kwa lugha.Pamoja na jitihada zangu za kwenda na wakati,hutokea nikapigwa chenga.Nikawa sielewi na kubaki nikijiuliza maswali..
Leo niliposikiliza wimbo mpya kutoka kwa Dully Skyes,ghafla nikawa nimeachwa solemba.Nikatoka patupu.Wimbo unaitwa Shikide.Swali likanijia,Shikide ni nini? Kutokana na maneno yaliyomo katika wimbo wenyewe,yaelekea Shikide ni style ya kucheza.Nilipojaribu kumuuliza “mama watoto” kama yeye amelinyaka neno la Shikide au style ya Shikide alichoweza kuniambia ni kwamba labda tusubiri kuona video ya wimbo huu na ndio tutaelewa shikide ni nini.
Lakini kwa sababu BC ni uwanja mpana na penye wengi haliharibiki jambo,nimeona ni vyema kuwauliza wanaoweza kuwa wanajua zaidi.Shikide ni nini? Kwa upande wa wimbo wenyewe,Dully Sykes ambaye alipoanza muziki alikubali kuitwa “Mr.Misifa” anaonyesha tena kwamba bado yupo.
Style ya Dully Sykes haijabadilika sana tokea enzi zile alipoanza na kutamba sana na nyimbo kama vile Ladies Free,Julieta,Nyambizi(huu ulitamba na kuzua utata pia),Historia ya kweli n.k.Msikilize hapa.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Feedback / Comments
6 Responses to ““SHIKIDE”-DULLY SYKES”
Leave a Reply


sending...
LETENI RAHA VIJANA HAPA AUSTRALIA NA SHIKA DEMU MWIMBO.musik mzuri,ntamani niwe kijana kama duli sykes.mark
shikidee maana yake ni shikidee!!!!!!!!!!!!!!! usichoelewa wewe ni ki2 gani???
keep it rolling dully.
NIITE RICHARD JULIUS MAKENJI WA TTC TARME MARA.NIMEINYAKA HIYO KIJANA NINAKUKUBALI KIVYOTEVYOTE SI UNAJUA KIMASTYLE BONGO HII HAWAKUFATI.SHIKIDE LIKOMZUKA SAAAAAAANA.JINSI GANI UNAONESHA UBUNIFU WA HALI YA JUU KTK GEMU<KAZA BUTI SANAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA.HI 2 SIR MAKENJI AKIWA UNIV DODOMA.
Niaajeeeeee m2mzm we ni noma mi naakufaagilia ilekinoma kuhussu iyongoma ikojuuu ccjaona wakugusa levo zako kaka pamoko saaaaaaaaaaanaaaaaaaaaaa
Nimependa wimbo ambao uliuimba wakati unahojiwa na Dulla wa eatv katika kipindi cha planet bongo, keep it up men