Mojawapo ya mambo ambayo viongozi mbalimbali wa dunia hupenda kufanya wanapokutana ni kupiga picha.Katika nchi za magharibi kitu hicho huitwa Photo Opps au photo opportunity.Picha moja ni sawa na maneno elfu moja.Viongozi hulitambua hilo.Huwa ni nafasi ya kuwaonyesha wananchi mambo mbalimbali kwa kutumia picha.Wanaposalimiana na kujitega kwa picha huku wakiwa wanatabasamu,mwananchi wa kawaida atatafsiri kitu hicho kama amani,upendo na urafiki miongoni mwa viongozi hao na hivyo inamaanisha kwamba nchi zao zipo katika urafiki fulani ambao una manufaa kwa nchi husika.Yaweza kuwa kweli na pia yaweza kuwa sio kweli.
Photo Opps ni masuala ya kihistoria.Yamekuwepo tangu enzi na enzi.Ni masuala ya kidiplomasia.Viongozi kushikana mikono(kwa ishara ya kusalimiana),kutabasamu huku wakiwa wameelekeza nyuso zao upande walipo wapiga picha,ni mambo yaliyozoeleka.
Tangu Rais wa Marekani,Barack Obama aweke historia ya kuwa Rais wa kwanza wa Marekani mwenye asili ya Afrika au mweusi na kutokana na jinsi yeye na mkewe Michelle Obama walivyoiteka dunia,hakuna kiongozi ambaye hutaka kubakia nyuma linapokuja suala la kupiga picha nao.Bila shaka utakumbuka jinsi viongozi wa G20 walivyokuwa wanahangaika kupiga picha na Obama kule nchini Ujerumani mapema mwaka huu.
Majuzi jijini New York na kule Pittsburgh hali ilikuwa ni hiyo hiyo.Viongozi wetu wa Afrika nao hawako nyuma katika suala la picha na kina Obama.Kina Obama nao bila shaka ni wapenzi wa masuala ya picha na kwa sababu wao ndio walikuwa wenyeji kidiplomasia iliwabidi.Hizi hapa ni baadhi ya picha wakiwa na viongozi mbalimbali wa Afrika akiwemo Rais wetu,Jakaya Mrisho Kikwete.

Rais Kikwete (katikati) akiwa na Rais Obama(kulia) na US First Lady,Michelle Obama.Bila shaka picha hii ingependeza zaidi kama Mama Salma Kikwete angekuwepo.Mtizamo binafsi.

Kutoka kulia kwenda kushoto,Rais Barack Obama,Waziri Mkuu wa Kenya,Raila Odinga,US First Lady,Michelle Obama na mke wa PM Odinga,Mama Ida Raila Odinga.

Kutoka kulia kwenda kushoto,Rais Obama,Rais wa Uganda,Yoweri Kaguta Museveni,US First Lady,Michelle Obama na Ugandan First Lady,Janet Museveni

Kutoka kulia kwenda kushoto,Rais Obama,Rais Paul Biya wa Cameroon,US First Lady,Michelle Obama na First wa Cameroon,Mrs.Chantal Biya.Tayari kumeshazuka maneno katika blogs mbalimbali hususani nchini Marekani kuhusu wig alilovaa Mrs.Chantal Biya.Soma hapa.
Kwa picha zaidi bonyeza hapa
Feedback / Comments
23 Responses to “WITH THE OBAMAS…”
Leave a Reply


sending...
Dah!!! Mke wa Rais wa Cameroun, ni bonge la “mshamba”, ni aibu tupu. Sina hata la kusema hapo.
Odinga alimtema lini mke wake wa kizungu? Au Odinga ana wake wawili? Naomba mnifahamishe kwa anayefahamu lolote kuhusu hilo.
This Is Black=Blackmannen
Hiyo MIGUU ya Mama Obama! Mweeh!
Hivi kwani huko maekani hakunaga zile dawa za WACHINA akaibust kidogo hiyo miguu yake?
Khaa!
Hapo naona Moderator umetupa mtihani mgumu,unataka tujiulize maswali magumu yasiyo na majibu.Unataka tuangalie hizo picha na kutoka na uchambuzi wa kwa nini Raisi wetu ndiye tu ameonekana peke.
Kweli kabisa Protocali ni muhimu sana, hasa kwa wenzetu,tena linapokuja suala la mwakilishi wa nchi.Sijui first lady wetu alikuwa wapi kwani kwenye shughuli kubwa hiyo kila mtu anakuwa na wa kwake.
Hilo pungufu laweza kuonekana dogo sana kwa mtu asiyejua,kwa mtu asiyeangalia kwa picha kubwa.Lakini kwa watu wenye zao, wanaichukulia hayo mazingira kwa masikitiko sana.Watanzania tunapenda kutake things for granted that why they costed us a lot,and we are going to pay the price for ever.
Obama anamuamini mr president wetu mbona kamuachia mtoto upande wake? shauri yake hatutabiriki sisi!
BC hamjambo!
mama wa cameroun kigoli nini.
BC Mambo wajameni,
huyo mama wa cameroun ananikumusha vigoli wa mlali morogoro wakitolewa kuchezwa ngoma.
Matty,upo wapi tupe shout
mwandiga umenifanya nicheke
du mr. obama vimiguu ni vyako au wamekutoa upside doun???????
sory not mr, itz mrs
Jamatini kaingia Golo
Dada zangu wa BC,
Siku zote mmekuwa mkimshambulia sana “shemeji” yangu Mama Mkapa, kwa vijiguu vyake ya aina ya fito.
Lakini yeye ni mchagga. Watu kutoka sehemu za uchaggani wengi wao wako hivyo kutokana na kupanda Mlima Kilimanjaro kupata majani ya ng’ombe.
Hali hiyo sio mbaya, maana ni uwajibikaji ndani ya nyumba, kwa wa mama wa sehemu hiyo.
Lakini tunapokutana na fito (miguu mwembamba mfano wa fito) za Mama Obama, na anapeta hapa bila ya maoni ya akina dada zangu wa Tanzania, inanipa mawazo mengi. Mko wapi leo hapa?
Ni “Mchokozi” tu ndiye aliyediriki kugusia swala la vijimiguu vya Michelle, wakati watu wote tunaviona hapa, lakini hakuna anayethubutu kukosoa kitu.
Kenya kuna Wakamba wenye mamiguu ya “Kihaya”, na hata baadhi ya Wajeluo wana mamiguu ya “Kijita”, sijui Bwana mdogo wetu Barack, alipotea vipi hapo, hadi kujikwaa kwenye fito hizo.
Lakini hata hivyo “Siri Ya Mtungi…!” au “Utamu wa Ndizi Umo Ndani ya Nguo Zake”. Heri na baraka zenu Obamas, uzuri wa mtu sio sura ni ndani ya roho yake.
This Is Black=Blackmannen
mimi naona miguu ya mrs obama ipo ok tu. no fat.
nyie wabongo acheni kusagia wenzenu.hata mseme nini hao ni wake wa marais. na miguu yenu minene mbona mmeishia kuolewa na wauza nazi? wenzenu walikuwa hivyo hivyo mkapa na obama wakawapenda, wakawachagua wakawaoa.kila mtu bahati yake na mvuto wake. mtaishia kusema miguu ya fito ya kichaga wenzenu wanapeta.Mafirst Lady. acheni wivu na comment zenu za kifala fala. ndoa iheshimiwe na watu wote.
Masikini Lady in red Ft “Mkorogo” & Wig!
Naomba kuuliza, Kikwe, Mu7 na Ondinga ni Uanajeshi au Uoga?
“Sahihisho” 2 Blackmannen.
Sio kweli kuwa upandaji wa milima na shughuli nyingine za Uchagani zinasababisha Jamii hiyo kuwa na “vimiguu” ni mambo ya Genes.
Kuna wadada wamezaliwa Dar(hakuna kupanda milima wala kusaka majani ya ng’ombe) na sio Wachaga lakini still wanavingoko na ving’isi(viazi)juu!
Naona Balozi Cisco tu ndio alikuwa anaweza kufuata protokali bila kumuogopa bosi!
BC,naaminia hapa wapo washua wanaosifia na kuponda ikibidi.
Nimeangalia global publisher na kumuona kanumba akiwa anahojiwa kule london katika kipindi cha ”sporah’ kama sijakosea. Jamani mnyonge mpeni haki yake lugha yake ni nzuri. Let us be honest.
Nilichokiona ni kuwa labda haelewi swali linataka nini[sio lugha].
Kanumba jifunze kuwa tabia njema ni silaha,na tabia mbaya ni mtaji wa maadui.
Wewe kuwa bongo celeb. sio ticket ya kufanya madudu bali opportunity ya kuonyesha discipline. Madongo yote kutoka sauzi si lugha yako,ni ”wabaya” wako walikuwa wanakuvizia.
Acha kusema hovyo na kuruka ruka na vigoli wa watu.
Nenda cameroun utaibuka na kigoli pooa kama cha prezida.
Nawakilisha
To my opinion, Mu7′s wife is the hottest of them all. Cameroonian’s 1st lady is the ugliest and Michele is the coolest, he he he. JK and Obama mmhhh its hard to pick…. tight race…
Dada Dina!
Sio kwamba silijui hilo unaloniambia, bali ni kuelewa hali halisi kuwa hapa BC unaongea na akina nani.
Maswala ya evolution, au nadharia za akina Darwin au Mendeleev, ukizileta hapa. Watu wengi utakuwa umewaweka njia panda.
Uwanja huu wa BC kuna safari za mamba ikiwa ni pamoja na “kenge”, ambao wakiwa ndio wengi zaidi ya mamba waliopo hapa.
Mara nyingi nimekua nikitoa coments za mwelekeo wa kisomi. Lakini ninajikuta maoni yangu yakiwa ndiyo kifunga mada za BC.
Katika kuthibitishia hiki nikisemacho, jaribuni kurudi nyuma kuyaangalia, katika maoni yangu mengi niliyoyatoa.
Dada Dina, maelezo niliyoyatoa hapo, ni mifano yetu ya kijamii, maelezo yasiyohitaji uthibitsho wa kisayansi. Ni jinsi ambavyo tunavyowaona wachagga wetu wakiwa na vijimiguu vya vijiti.
Kwa hiyo dada Dina, nimekuelewa vizuri sana kwa hayo mambo ya “Genetic”, upo sahihi.
It’s Great To Be Black=Blackmannen
Bila shaka Obama aliangalia ubongo wa mama huyu ulivyoelimika na jinsi unavyofanya kazi kiufasaha. Sidhani kama aliangalia miguu. Hilo sio swala muhimu sana kwenye relationship. Pengine angeangalia miguu, leo asingekuwa the first black President of U.S.A.
Wachagga na miguu yao mnayoisingizia ni design ya vijiti wako bomba na wana historia ndefuu kuchumi, wanapesa nammanisha na wazuri wa sura. Hapo Dar mnawasikiaje??
papaa Blackmannen mbona maumbile ya dada zetu wa kule kilimanjaro unayajua kiundani sana?????? kunani pale!!!!!!!!!!!!!!!!!! ukizingatia kule huwa wanavaa suruali za kiume halafu wanapiga kanga kwa juu. sasa hiyo miguu njiti umeiona wapi?? hebu tueleze zaidi hapo………………
huyo 1st mama wa cameroun mbona anaonekana kama demu wa market?
Papai,
Wachagga ni shemeji, wakwe na wake zangu. Wanangu ni mchanganyiko wa kichagga na usukuma.
Wasukuma wanawacheka wachagga kwa kulisha ng’ombe ndani ya boma, badala ya kuwapeleka mchungani. He he he he he he he!!!!!!
Wachagga, wanadai eti wanapesa, wakati msukuma anaona vipesa vyao hivyo ni vijisenti tuu kwa msukuma.
Sisi vijimilioni vya dola, tunaona ni vijisenti. Swala hili la vijisenti, sasa limekuwa swala la kitaifa.
Wazungu, Uingereza wananyonyoka nywele, kwa kuangalia kisheria, juu ya swala la vijisenti, wakati wao walidhani wametoa kitu kikubwa kwa “msukuma” yule, na yeye anaona ni vijisenti.
Yise banhu batale, mujagi “Subi” u onukta77.com/
This Is Black=Blackmannen