Kwa muda mrefu Tanzania tumekuwa na tatizo la kukosa waandishi wa vitabu. Waliotakiwa kuandika wamekuwa wakilalama kwamba hata wakiandika hakuna wasomaji achilia mbali wanunuaji wa vitabu. Bila shaka aliyetoa “utani wa ukweli” kwamba ukitaka kuficha kitu na mtu mweusi asikione,basi kifiche kwenye kitabu,alikuwa ameiangalia Tanzania pia.
Tatizo hilo linaelekea kupata ufumbuzi. Pengine inatokana na mabadiliko ya kidunia ya sayansi,tekinolojia na mawasiliano au ni wakati tu umefika wa Tanzania nayo kuzinduka na kuamua kuingia kwenye ramani ya watunzi na wasomaji wa vitabu.
Hivi karibuni,aliyewahi kuwa Gavana wa kwanza wa Benki Kuu nchini Tanzania,Edwin Mtei, ameandika kitabu. Kitabu kinaitwa From Goatherd to Governor ambacho kwa tafsiri ya moja kwa moja ya Kiswahili ni Kutoka Mchunga Mbuzi mpaka kuwa Gavana. Ni kitabu kuhusu maisha yake kikiwa na mengi kuhusu uhusiano wake na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye kama wengi tunavyojua,hawakuelewana katika mambo mbalimbali ya sera za kiuchumi.Ukitaka kukinunua kitabu cha Edwin Mtei bonyeza hapa.

Mbali ya Edwin Mtei, aliyewahi kuwa Miss Tanzania 1999,Hoyce Temu naye ametoa kitabu chake.Kinaitwa Nayakumbuka Yote.Mbali ya kuongelea kuhusu maisha yake,kitabu cha Hoyce ni muongozo mzuri kwa wasichana ambao wanataka kuingia au tayari wamo katika sanaa ya mitindo na urembo.Kinacho kipengele cha “Maswali na Majibu” kuhusu sanaa ya urembo.Kukipata kitabu hiki bonyeza hapa.
Hoyce Temu wakati wa uzinduzi wa “Nayakumbuka Yote”
Huu ni mfano na muelekeo mzuri kwa nchi yetu na kwa wapenzi wa kujisomea. Bila shaka hatutaishia kwa Mtei na Temu bali katika siku za karibuni tutaona wengine wakijitokeza na kuandika. Utamaduni huu ni miongoni mwa tamaduni ambazo mimi binafsi naona zinafaa kuiga.Wenzetu ni mabingwa wa kuandika na kujisomea.Hongera Mtei.Hongera Hoyce.
Vitabu vyote vimetolewa chini ya usimamizi wa kampuni ya Mkuki na Nyota.

Je,imeshawahi kukutokea ukampenda mtu halafu yeye hakupendi na mbaya zaidi analichukulia penzi lako kama kichekesho au kitu kisicho na maana? Na inakuwaje mwenzako anapokuchukulia kama “daladala” kwa maana ya kwamba ni kitu huru kwa kila mtu kupanda na kushuka apendavyo au atakapo?
Hayo yamo kwenye wimbo wa Maunda Zorro ambaye bila shaka hivi sasa ni miongoni mwa wasanii wa kike wa muziki wa kizazi kipya wanaofanya vizuri.Maunda yupo katika ziara ndefu ya Fiesta ambayo hivi karibuni itatua jijini Dar-es-salaam.
Usikilize Daladala kwa kubonyeza player hapo chini.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Msimu wa 2009/10 wa ligi maarufu ya mpira wa kikapu ya nchini Marekani(NBA) unaanza hivi leo. Ni mwanzo wa mikikimikiki ya ushindani mkali ambao hutawala ligi hiyo.
Kwa watanzania wengi, macho na masikio yao,watayaelekeza kwa Hasheem Thabeet ambaye kwa mapana na marefu atakuwa sio tu anaitafutia timu yake ya Memphis Grizzlies ushindi,bali pia atakuwa akiipeperusha bendera ya nchi yake ya Tanzania kwa njia moja au nyingine.
Habari za Hasheem zitakuwa sio tu za uchezaji bali pia jinsi ambavyo ni “ndoto iliyotimia” kwa kijana kutoka nchi ya “ulimwengu wa tatu” kama ya Tanzania kufikia kiwango cha kucheza katika ligi ya NBA ambayo hata huko Marekani kwenyewe,vijana wengi hutamani sana kufanya hivyo.
Bila shaka jina la Tanzania litatajwa mara nyingi kuliko kawaida katika matangazo ya ligi hiyo.Ni kwa sababu ya Hasheem Thabeet,mtanzania wa kwanza kuchezea katika ligi hiyo.Haishangazi kuona kwamba watu wengi,wakiwemo viongozi wetu,wanajitahidi kuwa karibu zaidi na Hasheem Thabeet.Jina lake ni ishara ya ushindi.Ni lulu.
Ingawa Hasheem hayupo bado katika “First Five” ya timu yake ya Grizzlies Memphis,bila shaka atacheza kesho wakati timu yake itakapowakaribisha, Detroit Pistons (kutoka jijini Detroit,Michigan) mjini Memphis,Tennesse yalipo makao makuu ya Grizzlies Memphis.Watabiri wa mambo wanasema Hasheem tayari ameonyesha uwezo mkubwa wa kuzuia mirusho ya timu pinzani lakini wanashauri azidishe juhudi katika rebounding.Bila shaka anasikia na atazingatia ushauri huo na pia wa makocha wake.
BC inaungana na wote wanaomtakia kheri Hasheem.Tunaelewa kwamba mafanikio ya Hasheem ndio mwanzo wa mafanikio ya vijana wengine wengi wa kitanzania ambao naamini kabisa,endapo watapewa nafasi,wanaweza pia kufikia kiwango cha Hasheem.Kila la kheri HT.

Hakuna ubishi kwamba miongoni mwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya walio na kipaji cha uimbaji ni Marlaw.Tangu alipoanza safari yake katika ulimwengu wa muziki amekuwa hawaangushi mashabiki wake kila atoapo wimbo mpya.
Baada ya kutoa kile kibao cha Pip Pip(Missing You My Baby) ambacho kilizua mjadala mkubwa kuliko kawaida,hivi karibuni ameibuka na kitu “Bidii“.
Sina uhakika kama wataalamu wa mtiririko wa mashairi watasemaje safari hii lakini naamini kwamba wimbo wa Bidii ni mojawapo ya zile nyimbo ambazo tunaweza kuziita ‘zenye ujumbe’.Maisha yanataka bidii.Lazima ujitahidi endapo mafanikio ni ndoto yako.
Msikilize Marlaw katika wimbo huu,Bidii.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

If you are into fashion,you gotta watch Sheria Ngowi.Click Here.
Kama unafuatilia ratiba za shughuli za starehe hususani zinazowashirikisha vijana,basi bila shaka hivi sasa utakuwa unafuatilia ratiba nzima ya matamasha ambayo yanakwenda kwa jina la Fiesta.Kuna mtu kaniambia kwamba ukitaka kujua vijana wa Tanzania wanaupokea vipi muziki wa kizazi kipya basi huhitaji kuhangaika mitaani ukidadisi bali kuhudhuria tu matamasha ya Fiesta.Wiki tunayoicha Fiesta ilikuwa Tanga(waja leo waondoka leo).Mambo huko yalikuwa kama yanavyoonekana katika picha hizi.
Ukitaka kuona picha na picha zaidi za matamasha mbalimbali ya Fiesta,mtembelee Ahmad Michuzi,ambaye pamoja na kuwa mhusika wa karibu wa Fiesta,bali ni blogger ambaye anafanya kazi ya nguvu ili kuhakikisha kwamba kila mtu anapata japo nafasi ya kujua kilichojiri katika Fiesta.Bonyeza hapa.

Prof.Jay(Joseph Haule) akiwajibika kuwapa burudani kamili wakazi wa Tanga

Albert Mangwair,one of the best hip hop artist of the land.It’s Fiesta Time

Kutoka La Familia,Chid Benz na Chiku wakiwajibika jukwaani.


Kwanza naomba nianze kwa kusema;Asante kwa uvumilivu wako wakati BC ilipokuwa matengenezoni kwa siku kadhaa.Kilichokuwa kinafanyika ni kurekebisha links zote za tangu BC ianze zaidi ya miaka miwili iliyopita sasa.Baada ya hapo ilikuwa ni kuhifadhi upya(back-up) nyaraka zote zilizomo humu.Pia kilichofanyika ni kuhakikisha kwamba BC inaendelea kufunguka bila shida.Kama kwa njia moja au nyingine,unapata shida kuifungua BC,tafadhali tujulishe kupitia bongocelebrity at gmail dot com au info at bongocelebrity dot com.Asante
Utakumbuka kwamba BC ilianzishwa ili kutimiza lengo la kuweka habari zetu,za super stars wetu mtandaoni na hivyo kwa njia moja ama nyingine,kuweka mtandaoni historia yetu.Kwa kiasi fulani tunaendelea kufanikiwa katika hilo.Yote hiyo ni kwa sababu yako wewe msomaji,mtembeleaji na mchangiaji wa BC.Asante sana.
Kama uliimiss BC,we missed you too.Shukrani kwa baadhi yenu mliotutumia barua pepe za kheri na kutiana moyo.Leo hii hata sijui tuanzie wapi.Kwa siku kadhaa tu mengi yametokea,tumepitwa.Hatuna budi kujitahidi kukimbia kama vile tupo kwenye mbio za marathon ili twende sambamba na BC iendelee kuwa BC.
Mojawapo ya matukio muhimu yaliyotokea wakati tukiwa off ni kupatikana kwa mshindi mpya wa shindano linalozidi kujijengea umaarufu mwaka baada ya mwaka la Bongo Star Search kwa upande wa muziki.Kijana aliyeibuka mshindi anaitwa Pascal Cassian anayetokea jijini Mwanza,kaskazini mwa Tanzania.
Kwa mujibu wa wafuatiliaji wa shindano hili lililo chini ya usimamizi wa Rita Paulsen maarufu kama “Madam Rita”,Pascal alistahili kushinda.Alikuwa na upekee katika kuimba jambo ambalo ndilo wanalolizingatia zaidi waamuzi(judges) wa shindano hilo.Pamoja na ukweli huo,kama binadamu,Pascal ana mapungufu yake kisanii.Amepewa ushauri wa bure kupitia ukurasa huu hapa.
Je nini maoni yako kuhusu lilivyokuwa shindano la mwaka huu la BSS?Pascal alistahili kushinda?
Photo/Abdallah Mrisho

Mpenzi msomaji/mtembeleaji wa BC,
BC itakuwa chini ya matengenezo kwa siku mbili tatu zijazo.Kwa bahati mbaya,matengenezo hayo yatasababisha kutokuwepo kwa habari(posts) mpya katika muda huo wa matengenezo.Pamoja na hayo,maoni yako katika posts zilizopo yanakaribishwa na yataendelea kuwekwa hewani kama kawaida. Unakaribishwa pia kuzitizama posts mbalimbali zilizopita,yakiwemo mahojiano mbalimbali kwa kutembelea ukurasa wa “Archives”.
Matengenezo ni muhimu ili kuhakikisha kwamba BC inaendelea kupatikana kirahisi na kuwafikia watu wengi zaidi.Matengenezo haya hayatoathiri muonekano wa BC kwa namna yeyote ile kwa sasa.
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Asanteni.
Jeff Msangi kwa niaba ya wana-BC wote.
Nilipoteta naye kwa kina miezi michache iliyopita, Joseph Mbilinyi aka Sugu au pia maarufu kama Mr.II,alitoa ahadi muhimu kwa mashabiki wake.Alisema yupo studio jijini New York akirekodi albamu yake ya kumi ambayo ameipa jina la VETO.Alikuwa anakumbusha ukweli kwamba msanii hawezi kustaafu bali hupumzika tu kwa muda fulani. Sanaa huwa ipo kwenye damu.Ni vigumu kuikacha.Hakuna ambaye ameweza kuthubutu akafanikiwa.
Ahadi ni deni.Kama alivyoahidi hivi majuzi Sugu ameitimiza kwa kuanza kuachia nyimbo zitakazosheheni katika albamu hiyo.Miongoni mwa nyimbo hizo ni ule uitwao Hold On akiwa amemshirikisha mshikaji anayekwenda kwa jina la Andre.
Sasa kama wewe ni mshabiki wa Sugu au umewahi kukutana na mshabiki wa Sugu,bila shaka utakubaliana nami ninaposema Sugu anabakia kuwa mshirika muhimu katika lile kundi la wasanii wa muziki wa kizazi kipya ambao huwaza,hutafakari,kusanii na kusahihisha kabla hajakubaliana na kile anachotaka kukiongolea katika wimbo wake.Kwa bahati mbaya wasanii wa kundi hili wanabakia kuwa wachache. Utitiri wa wasanii wapya haujawa suluhisho la tatizo sugu la ukosefu wa wasanii wanaitizama jamii kwa umakini wa hali ya juu.Kwa maneno mengine,nyimbo zake zimejaa ujumbe.Zinailenga jamii na kuongelea kile ambacho yeye,kama msanii,anakiona katika jamii. Unaweza usiupende kuucheza lakini bila shaka,kama hujali kuambiwa ukweli,basi utapenda kuusikiliza.
Katika wimbo huu,Sugu anagusia maisha na watu.Mahusiano ya wanajamii.Jinsi ambavyo umdhaniaye anaweza kuwa siye na kinyume chake.Msikilize hapa Sugu. Wimbo unaitwa Hold On.Kazi nzuri Sugu
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

