86343355JM014_Grizz_PortraitMsimu wa 2009/10 wa ligi maarufu ya mpira wa kikapu ya nchini Marekani(NBA) unaanza hivi leo. Ni mwanzo wa mikikimikiki ya ushindani mkali ambao hutawala ligi hiyo.

Kwa watanzania wengi, macho na masikio yao,watayaelekeza kwa Hasheem Thabeet ambaye kwa mapana na marefu atakuwa sio tu anaitafutia timu yake ya Memphis Grizzlies ushindi,bali pia atakuwa akiipeperusha bendera ya nchi yake ya Tanzania kwa njia moja au nyingine.

Habari za Hasheem zitakuwa sio tu za uchezaji bali pia jinsi ambavyo ni “ndoto iliyotimia” kwa kijana kutoka nchi ya “ulimwengu wa tatu” kama ya Tanzania kufikia kiwango cha kucheza katika ligi ya NBA ambayo hata huko Marekani kwenyewe,vijana wengi hutamani sana kufanya hivyo.

Bila shaka jina la Tanzania litatajwa mara nyingi kuliko kawaida katika matangazo ya ligi hiyo.Ni kwa sababu ya Hasheem Thabeet,mtanzania wa kwanza kuchezea katika ligi hiyo.Haishangazi kuona kwamba watu wengi,wakiwemo viongozi wetu,wanajitahidi kuwa karibu zaidi na Hasheem Thabeet.Jina lake ni ishara ya ushindi.Ni lulu.

Ingawa Hasheem hayupo bado katika “First Five” ya timu yake ya Grizzlies Memphis,bila shaka atacheza kesho wakati timu yake itakapowakaribisha, Detroit Pistons (kutoka jijini Detroit,Michigan) mjini Memphis,Tennesse yalipo makao makuu ya Grizzlies Memphis.Watabiri wa mambo wanasema Hasheem tayari ameonyesha uwezo mkubwa wa kuzuia mirusho ya timu pinzani lakini wanashauri azidishe juhudi katika rebounding.Bila shaka anasikia na atazingatia ushauri huo na pia wa makocha wake.

BC inaungana na wote wanaomtakia kheri Hasheem.Tunaelewa kwamba mafanikio ya Hasheem ndio mwanzo wa mafanikio ya vijana wengine wengi wa kitanzania ambao naamini kabisa,endapo watapewa nafasi,wanaweza pia kufikia kiwango cha Hasheem.Kila la kheri HT.

Feedback / Comments

6 Responses to “NBA STARTS…ALL THE BEST HASHEEM”

  1. Comment by Sports Fan on October 28th, 2009 1:54 pm

    I didn’t cheer and still I don’t like Hasheem to play in Memphis, but it is so bad that no one can choose an organization during drafting. This team does not need Hasheem and he does not need it either. Marc Gasol (Paul Gasol’s brother)is far productive and more experienced than Hasheem, no coach would pick Thabeet to start in the roaster when you have people like Gasol. This means Hasheem will have to come off the bench for a long while, this means that he will be playing against the bench players of other teams. If it goes all season long; it means hasheem will lose some credit considering that the first season matters a lot to any rookie (Even the rookie of the year must have a definitive role in the team and must be a starter). All rookies who became influantial in the league they secured a starting spot from season one. Wadau this is just my views although I know Hasheem is very humbled, somewhere down the road he will have to be aggressive for a trade…he can reach a far more potential than coming off the bench!

  2. Comment by khamis on October 29th, 2009 7:27 pm

    Nakubaliana na wewe mdau hapo juu, kitu chengine ni kwamba angeenda timu yenye viterani ingemsadia sana kujifunza gemu hii,(kama blair kwenda pale spurs)
    pia huyu mdau bado anakazi kubwa sana ya kufanya kujiestablish katika NBA, jana nimecheki highlight ya gemu waliyocheza na Pistons, na statistics zake kusema kweli hazijaridhisha kabisa kwa mtu aliyecheza dakika karibia 15, he need to learn mapema na kuanza kufanya mambo, la sio hivo tutamsahau kwenye bench then He will be out for gud.
    Alafu mwambieni apunguze u blaza, he need to be a man, lots of kidz are following him.

  3. Comment by japha on October 30th, 2009 3:03 am

    wat we apriciate from hasheem is to have a chance at nba ligue it doesnt matter the club or let say team,coz if ur playin at nba ligue and u have the talent its easy to get big team.so keep it up and fly with tanzania flag men,we are all fans of u coz we know u from makongo school and we wish u all tha best.

  4. Comment by papai on October 30th, 2009 12:02 pm

    yeah mashkaji itabidi akaze boot, ndo challenges zenyewe hizo. kila kwenye mafanikio there is always price to pay, in way or another. na grizzlies wamesajili Allen Iverson kama guard ingawa ni majeruhi, so ni bahati kucheza na mtu kama iverson lakini challenge vilevile kwani kiwango chako kinatakiwa at least kisiwe na gap saana. ila mimi na naamini na watanzania wengi tunamuombea.

  5. Comment by MAKULILO, Jr. on November 1st, 2009 1:59 am

    Kila kitu ni challenge, hivyo wadau hapo juu sio mseme kuwa atashindwa kucheza huko Memphis. Hata akina Kobe wenyewe sio gemu rahisi kwao, wanakomaa kila siku na mazoezi na juhudi. Ukija hata kwenye soka, sio kwamba akina Christain Ronaldo, Kaka, Mesi, Zidane nk ndio kila kitu, nao kila siku wanakaza buti ili wafike mbali zaidi kwenye gemu.

    Tukubaliane na uwezo wa Hasheem Thabeet upo juu sana. Na wataalam wa timu yake wameona kuwa ni mtu muhimu ktk timu yao. Kuwepo kwa mtu mwingine wa kucheza namba hiyo haina maana kuwa hatakiwi. Mbona timu ya taifa ya Spain (Soka) inakua na viungo wengi sana kama Alonso, Sena, Xavi, Iniesta, Fabregas nk na wote wanachukuliwa ktk timu ya taifa. Kuanzia benchi au direct haina maana kiwango chako kibovu. Point ni kwamba ndani ya dakika utakazocheza utaifanyia nini timu yako ktk kuleta ushindi, hiocho ndio Hasheem anachotakiwa kufanya, na si suala la kuanza au kutoka benchi.

    MAKULILO, Jr.
    http://www.makulilo.blogspot.com
    San Diego, CA

  6. Comment by MUGA RAYMOND on November 6th, 2009 5:43 pm

    Mr Makulilo is right, thabeet is a skilled player, thats why he got a contract wit memphis glizzlies, i guess we shld encourage him 2 practise a little more harder 2 fit in the NBA league well, other than puttin negative coments toward him, knowin that we’re sowing misfortune 2 him, so is it jealous or somthin? Guys we gat 2 support our boy all the way, thats the bottom line.

Leave a Reply