eduKwa muda mrefu Tanzania tumekuwa na tatizo la kukosa waandishi wa vitabu. Waliotakiwa kuandika wamekuwa wakilalama kwamba hata wakiandika hakuna wasomaji achilia mbali wanunuaji wa vitabu. Bila shaka aliyetoa “utani wa ukweli” kwamba ukitaka kuficha kitu na mtu mweusi asikione,basi kifiche kwenye kitabu,alikuwa ameiangalia Tanzania pia.

Tatizo hilo linaelekea kupata ufumbuzi. Pengine inatokana na mabadiliko ya kidunia ya sayansi,tekinolojia  na mawasiliano au ni wakati tu umefika wa Tanzania nayo kuzinduka na kuamua kuingia kwenye ramani ya watunzi na wasomaji wa vitabu.

Hivi karibuni,aliyewahi kuwa Gavana wa kwanza wa  Benki Kuu nchini Tanzania,Edwin Mtei, ameandika kitabu. Kitabu kinaitwa From Goatherd to Governor ambacho kwa tafsiri ya moja kwa moja ya Kiswahili ni Kutoka Mchunga Mbuzi mpaka kuwa Gavana. Ni kitabu kuhusu maisha yake kikiwa na mengi kuhusu uhusiano wake na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye kama wengi tunavyojua,hawakuelewana katika mambo mbalimbali ya sera za kiuchumi.Ukitaka kukinunua kitabu cha Edwin Mtei bonyeza hapa.

governor

Mbali ya Edwin Mtei, aliyewahi kuwa Miss Tanzania 1999,Hoyce Temu naye ametoa kitabu chake.Kinaitwa Nayakumbuka Yote.Mbali ya kuongelea kuhusu maisha yake,kitabu cha Hoyce ni muongozo mzuri kwa wasichana ambao wanataka kuingia au tayari wamo katika sanaa ya mitindo na urembo.Kinacho kipengele cha “Maswali na Majibu” kuhusu sanaa ya urembo.Kukipata kitabu hiki bonyeza hapa.

hoycetHoyce Temu wakati wa uzinduzi wa “Nayakumbuka Yote”

Huu ni mfano na muelekeo mzuri kwa nchi yetu na kwa wapenzi wa kujisomea. Bila shaka hatutaishia kwa Mtei na Temu bali katika siku za karibuni tutaona  wengine wakijitokeza na kuandika. Utamaduni huu ni miongoni mwa tamaduni ambazo mimi binafsi naona zinafaa kuiga.Wenzetu ni mabingwa wa kuandika na kujisomea.Hongera Mtei.Hongera Hoyce.

Vitabu vyote vimetolewa chini ya usimamizi wa kampuni ya Mkuki na Nyota.

Feedback / Comments

16 Responses to “UMEWASOMA EDWIN MTEI NA HOYCE TEMU?”

  1. Comment by Kikwete on November 2nd, 2009 12:34 pm

    wachaga bwana!

  2. Comment by john mwaipopo on November 2nd, 2009 12:36 pm

    i think it is high time we get to know autobiographies of some tanzanians

  3. Comment by kamanzi on November 3rd, 2009 2:06 am

    Haki ya nani Kikwete umenichekesha mno. Umewaza nini mpaka kuwaza kabila? Katu sikuliona hilo hapo mwanzoni. Ila inapendeza kuwaona mamiss wa Tz wanaonekana kwa mazuri kwenye media kuliko wengine waliojaa makashfa mpaka wanatia kizunguzungu.

  4. Comment by beline beline on November 4th, 2009 2:41 am

    ningenda nikipate hicho kitabu cha Mr. Mtei halafu niapply hizo maprincipal zake, nikitegemea kutoka kimtindo

  5. Comment by Joseph Mbele on November 8th, 2009 1:07 am

    Papo hapo hivi karibuni kilitoka kitabu cha Simba wa Vita, Mzee Kawawa.

  6. Comment by Joseph Mbele on November 8th, 2009 1:09 am

    Papo hapo, hivi karibuni kilitoka kitabu cha Simba wa Vita, Mzee Kawawa.

  7. Comment by meku on November 9th, 2009 10:16 am

    Mzee Mtei safi sana kwa kuandika kitabu hiki na kwa kweli sisi vijana ni wakati wa kujua kutunza kumbukumbu zetu na, inapendeza mno.
    Let me say this – “Well done BRAIN HERO”

  8. Comment by Temu Emmanuel on November 11th, 2009 5:44 pm

    Big up siz!!

  9. Comment by Semy on November 13th, 2009 9:46 am

    looong tym gal!!qyt duu lol…so creative..sio kuwa na makashfa ya ajabu ambayo hayana faida sijui wanaona sifaa!!!keep it up mumyy

  10. Comment by tida cct on November 17th, 2009 7:16 am

    congrats you all, Mtei and Hoyce. What you did others may copy for their life. its good men!! Big up!

  11. Comment by joan on March 3rd, 2010 9:04 am

    wachaga wako juu sana hongereni

  12. Comment by eric on April 15th, 2010 2:38 pm

    hakuna haja ya kutaja ukabila kwa waTanzania. Kwani mnataka kutambika. Iwe kwa mazuri au mabaya ukabila tusiutaje. Tutukuze utanzania wetu

  13. Comment by fortunatus on December 10th, 2010 4:46 am

    keep on moving never com back

  14. Comment by MCHIWA on April 9th, 2011 9:02 am

    SAFI SANA HUO NDO UJASILIAMALI.VERYGOOD.

  15. Comment by MCHIWA WA IFM on April 9th, 2011 9:05 am

    ILIKE CREATIVE PEOPLE LIKE U.VERYGOOD,KEEP IT UP.

  16. Comment by Othiniel K. Temu on June 23rd, 2011 6:45 am

    pale mwanzo kabisa sikumuelewe Kikwete alichomaanisha lakini Wachagga bwana wacha waitwe wachagga BIG UP

Leave a Reply