Warembo wanaoshiriki katika mashindano ya kimataifa ya urembo ya Miss East Africa 2009 wataanza kuwasili nchini wiki hii(au wameshaanza kuwasili) tayari kwa mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika tarehe 18 mwezi wa 12 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.

Aidha, warembo watakaoiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo wanatarajiwa kutangazwa kesho kutwa baada ya kamati maalumu iliyopewa jukumu la kuratibu zoezi hilo kukamilisha kazi yake.

Mashindano ya Miss East Africa mwaka huu yanatarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake kutokana na Nchi zinazoshiriki mashindano hayo kuchagua warembo wenye viwango vya hali ya juu ili kuziwakilisha katika mashindano ya mwaka huu

Miss East Africa 2009 itashirikisha warembo kutoka katika Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, na Mauritius ambazo zote zimeshathibitisha ushiriki wao.

Mashindano hayo makubwa ya urembo kwa ukanda huu wa Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Limited ya jijini Dar es salaam.

Miongoni mwa makampuni yanayodhamini mashindano hayo kwa mwaka huu ni pamoja na Kunduchi Beach Hotel & Resort, EATV, Kings & Queens Worldwide, CMC Automobiles Limited na AKO Catering Services Ltd.

Hizi hapa chini ni picha,majina na umri wa baadhi ya washiriki wa mashindano hayo.

East1

Rebecca Getachew (23) Ethiopia,

East3

Asli Osman Mahamud(20)-Somalia

East4

Fatma Abdilahi (18)-Somalia

East5

Dalysha Nirena Doorga (21)-Mauritius

East7

Tabitha(20)-Kenya

East8

Queen Belle Monique (23)-Burundi


TigerMcheza golf maarufu,Tiger Woods,33 amepata ajali na kuumia karibu na nyumbani kwake huko Windermere,Florida. Tiger alikuwa akiendesha gari lake aina ya 2009 Cadillac SUV ambapo aligonga fire hydrant kabla ya kuuvaa mti uliokuwa pembeni.Ilikuwa mida ya saa nane na dakika ishirini na tano alfajiri. Ilibidi mke wake atumie golf club kupasua kioo cha nyuma cha gari la Tiger ili kumtoa. Mke wake alisikia mlio wa ajali kwani na kukimbilia nje kwani ajali ilitokea karibu kabisa na nyumbani kwa star huyo wa mchezo wa golf duniani.

Hata hivyo tofauti na habari zilizokuwa zimeenea hapo mwanzo,Tiger hakuumia sana katika ajali hiyo mbali ya kupata michubuko kadhaa usoni. Ametibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani kwake. Tovuti yake imeielezea ajali ya Tiger kuwa “ndogo”.

Historia ya Tiger Woods katika michezo ni miongoni mwa historia zenye mvuto wa aina yake.Kwa mujibu wa tovuti yake,ameshashinda zaidi ya mashindano 93. Aliweka historia ya kuwa kijana mdogo zaidi kushinda taji maarufu la Masters.Alikuwa na umri wa miaka 21. Tiger amesomea Chuo Kikuu cha Stanford.Alifundishwa kucheza mchezo wa golf na baba yake mzazi,Earl.Baba yake alikuwa mwanajeshi,mmarekani mweusi wakati mama yake ana asili ya Thailand.Mwaka jana Tiger Woods alitajwa kuwa mwanamichezo aliyelipwa zaidi akiwa amekusanya jumla ya dola milioni 110 kutoka katika michezo na matangazo ya biashara.

EvanderHolyfield

BINGWA wa zamani wa masumbwi katika uzito wa juu duniani, Evander Holyfield wa Marekani amepanga kwenda Uganda kuzichapa na Francois ‘White Buffalo’ Botha wa Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa waratibu wa pambano hilo la kimataifa, wababe hao watazichapa Januari 16, wakiwania mkanda wa dunia wa WBF.

Pambano hilo ambalo litavuta hisia za wengi, litapiganwa siku hiyo katika Uwanja wa Taifa wa Mandela, mjini Kampala, Uganda. Kwa habari zaidi,bonyeza hapa.

HBC

Wikiendi iliyopita,jiji la Dar-es-salaam liligubikwa na homa ya “Fiesta”.Kuna ambao wamesema kama hukuhudhuria haifai hata kuomba kusimuliwa ilivyokuwa kwani hakuna jinsi ya kusimulia!

Wengi walikuwa wakielezea jinsi mwanamuziki mkongwe wa hip hop kutoka nchini Marekani,Busta Rhymes, alivyoweza kukonga nyoyo za mashabiki wa muziki.Wanasema japokuwa jamaa alilikwaa jukwaa wakati mida imeshakwenda sana,aliweza kuonyesha thamani yake kwa kuwapeleka mbio mashabiki wa mwanamuziki huyo.

Mimi sikuwepo.Nafuata ushauri wa kutokuomba hata kusimuliwa sana mambo yalivyokuwa.Niliyoyasoma katika vyombo mbalimbali vya habari  yanatosha.Lakini donge nililonalo ni kutokuwepo kuwaona HBC(Hard Blasterz Crew) wakisimama tena jukwaani kwa pamoja.I would have loved that.HBC ni miongoni mwa makundi ambayo binafsi naamini kwa dhati kwamba yalichangia sana kuuweka muziki wa kizazi kipya hapo ulipo.Isitoshe nilibahatika kuwa mtu wa karibu kwa vijana hao wa HBC enzi hizo walipokuwa wanaanza kuiteka fani ya muziki wa kizazi kipya.

Napenda kuheshimu watu au vikundi vinavyoanzishwa na kisha kujenga msingi wa jambo fulani.HBC ni miongoni mwa makundi hayo.Swali ni je,HBC ndio wamerudiana na labda tutarajie albamu kutoka kwao? Najaribu kuwatafuta ili wajibu swali hilo hapo juu wenyewe. Makundi mengine ambayo yalikuwepo siku hiyo ni pamoja na Daz Nundaz…wale wazee wa Kaaamandaaa..unawakumbuka? Wateule pia walikuwepo…yaani Jafarai,Mchizi Mox bila kumsahau Jay Moe.

Wimbo waliouimba majuzi ni huu hapa unaoitwa Niamini.Sikiliza hapo chini.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Pichani kutoka kushoto ni Terry Msiagi(aka Baba Ray),William Shundi(Big Willy) na Joseph Haule(Professor Jay)

Nako2Nako

Sijawahi kupata nafasi ya kufanya nao mahojiano ili kujua kwa kina maana au chanzo cha jina Nako 2 Nako.Pamoja na hayo,wengi wanawakubali na kwa mambo mbalimbali,yakiwemo binafsi,wameshagonga vichwa vya habari mara kwa mara. Walianzia A-Town/City kabla ya kuweka kambi jijini Dar.

Hivi karibuni wamefyatua kitu kipya.Wimbo unaitwa Ndani ya Nyumba ambao kutokana na Producer wake,Hermy B(kutoka B’Hitz Music) ni wimbo wa kustarehesha zaidi kuliko kuelimisha au vitu kama hivyo.

Kitu ambacho kimekuwa kikinivutia kutoka Nako2Nako ni aina yao ya kughani.Ina utofauti fulani hivi ambao kimsingi ni muhimu.Nimewahi kusisitiza katika “kijiwe” fulani kwamba kama mtu anataka kupata mafanikio fulani katika chochote anachotaka kukifanya,ni muhimu akawa “mbunifu”.Kwenye muziki hali ni hiyo hiyo.Lazima utoke tofauti.La sivyo,watu watakusikiliza na kukuacha solemba haraka iwezekanavyo.Huna jipya.

Wasikilize Nako2Nako katika Ndani ya Nyumba

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Machupa-FrontBC

Machupa ni mfungaji hodari. Usemi huo pekee unatosha kumuelezea Athuman Iddi Machupa (pichani) mshambuliaji kijana ambaye kwa upande wa Tanzania, aliwika zaidi alipokuwa akichezea timu ya soka ya Simba maarufu kama “Watoto wa Msimbazi”.

Hivi leo Machupa anasakata kabumbu nchini Sweden akiwa na timu ya Vasalund IF.

Niliwasiliana na Machupa hivi karibuni na kumuuliza maswali machache. Haya hapa mahojiano yetu;

BC: Mpaka sasa mambo yanakwendaje hapo Sweden?Unachezea timu gani na ipo daraja la ngapi?

Machupa: Kwa upande wangu hapa Sweden maisha yanakwenda poa kaka.Ninachezea timu inayoitwa Vasalund IF ilikuwa katika ligi ya Superettan (ligi ya pili kwa ukubwa hapa Sweden) lakini kwa bahati mbaya tumeshuka daraja hadi la kwanza..

BC: Umeshakaa Sweden kwa muda wa kutosha sasa.Unapaonaje na zaidi unaonaje nafasi za kuendeleza soka lako?

Machupa: Kwa sasa kaka napeleka mwaka hapa na kwa upande wangu mi naona maisha ni mazuri na hata nafasi ya kusonga mbele kwangu ni kubwa mno.Nazidisha bidii katika kila kitu na inshallah nitafanikiwa zaidi na zaidi.


BC: Kama mgeni katika nchi ya watu,ni mambo gani ambayo ilibidi ukabiliane nayo kwanza? Hapa nazungumzia mambo kama vile lugha,vyakula nk

Machupa: Of coz lugha kaka ni ngumu. Lakini nashukuru jamaa wamenishughulikia masuala yote ya muhimu ikiwa ni pamoja sehemu ya kujifunza lugha yao.Na kuhusu chakula; kwa kusema ukweli ni kizuri tu. Hakina tofauti sana na cha nyumbani Tanzania kwa sababu najipikia mwenyewe chakula ninachojisikia kula.Hali ya hewa nayo ilikuwa changamoto lakini taratibu ninazoea.

Machupa-Jikoni“Hebu ngoja nicheki kama vitu vishaiva”

BC: Una ujumbe gani kwa vijana wengine wanaosakata soka nyumbani Tanzania?

Machupa: Ujumbe wangu kwa vijana wanaosakata soka na hususani waliopo nyumbani ni kwamba waheshimu soka kwani soka ni kazi kama zilivyo kazi zingine zozote.Ukiheshimu soka hakika utafanikiwa.

BC: Mwakani ni mwaka wa kombe la dunia.Safari hii kipute kipo Africa.Nini matarajio yako kwa nchi za Afrika?

Machupa: Ni changamoto kubwa kwa timu za Africa ambazo zimefanikiwa kuingia katika finali hizo. Tusubiri tuone kwa sababu nina uhakika watajiandaa vizuri. Nina uhakika hatutosikia madai ya posho. Nina imani watatuwakilisha vyema kabisa,sina wasiwasi na hilo. Ila nahisi Ghana watafanya vizuri. Nawa-support.

Machupa-ZoeziniMachupa akiwa mazoezini na timu yake.Anaonekana kulia katika picha akijaribu kutuliza mpira chini.

BC: Una lolote la kuongeza kwa mashabiki wako?

Machupa: Mashabiki ndio kila kitu.Nawapenda na ninawaheshimu sana na hakika bila wao hatuwezi songa kwa sababu wao ndio wanaotukosoa pale tunapokosea.I love all my fans popote walipo.

oprah-winfreyMamilioni wamekuwa wakiangalia show yake. Kwa takribani miaka 25,jina la Oprah Winfrey limekuwa miongoni mwa majina yanayotambulika kwa urahisi zaidi duniani.

Ni miongoni mwa wanawake matajiri kupindukia na pia wenye uwezo mkubwa wa kubadilisha muelekeo wa takribani kitu chochote anachoamua kukiweka ubavuni mwake.Oprah akisema kitabu fulani ni kizuri,basi usishangae kikienda kuwa “best seller”.Akisema yeye nyumbani kwake anatumia aina fulani ya dawa kusafishia nyumba yake,ukienda madukani na kuambiwa zimekwisha,hutakiwi kushangaa.Ni Oprah factor.

Kuna imani kwamba yeye ni miongoni mwa watu muhimu sana kwa Rais wa Marekani,Barack Obama kwani alichangia kwa kiasi kikubwa ushindi wake kuelekea “Jumba Jeupe”.Oprah pia ni miongoni mwa watu maarufu wa kwanza kabisa kumkubali Obama na kusema wazi kwamba anataka jamaa agombee urais.Aliona mbali.

Sasa habari ni kwamba ameamua kuhitimisha au kusitisha show yake ifikapo tarehe 9 September mwaka 2011.Kwa maana hiyo bado kuna muda wa watu kuendelea kumfuatilia Oprah Winfrey ambaye bila shaka ni “mwana-mapinduzi” linapokuja suala la “Talk Shows”.Oprah anatarajiwa kutangaza rasmi uamuzi wake huo katika show itakayorushwa hewani hivi leo.

Je,fununu zinasema atafanya nini baada ya kuipa kisogo show yake? Unaweza kupata fununu hizo kwa kubonyeza hapa.

World Cup

Kombe la Dunia lipo ziarani nchini Tanzania. Ziara hiyo imezinduliwa rasmi leo jioni nchini Tanzania na Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Ziara ya kombe hilo katika sehemu mbalimbali duniani, ni ishara ya kuwapa fursa mashabiki mbalimbali wa soka ulimwenguni,nafasi ya kuliona kombe hilo “live” na hata kupiga nalo picha kwa kumbukumbu nk. Hizo zote ni miongoni mwa shughuli mbalimbali kuelekea South Africa 2010.

Wakati nikimuangalia Rais Kikwete akiwa amejawa na tabasamu wakati akilinyanyua kombe hilo na kulibusu,nilijiuliza, hivi itakuja tokea kweli siku moja Rais wa Tanzania(yeyote yule atakayekuwa madarakani) kulinyanyua Kombe la Dunia baada ya kulipokea toka mikononi mwa nahodha wa Taifa Stars baada ya kulitwaa?

Well…naamini kila kitu kinawezekana. Sina tu uhakika kama tuna mipango madhubuti(ya mbali au karibu) ya kutimiza ndoto hizo.Tusiishie tu kuliona kombe kwa mbali au kulinyanyua pale tusipostahili.

Picha/Yahya Charahani

HasheemT

Just a couple of weeks ago, he started his career as an NBA player. But before long, he broke his jaw in an incident involving him and his teammate, Zach Randolph. He actually suffered a ridgeline fracture in his mandible- a bone in his lower jaw.

Since the incident, his fans and well wishers have been praying for his quick recovery while his critics have also used the same opportunity to nail him down or try to elevate him. It just depends on how one looks at criticism.

I recently caught up with him, whereby, he took time to talk about his health and also to answer some of what his critics have been saying. Here is how my mini-interview with him went down…

BC: A lot of your fans and supporters have been worried about you since the jaw-breaking incident. Can you briefly tell me and of course…your fans how are you doing now and whether you are back in training and all that?

Hasheem Thabeet: Niko powa kabisa… I’m doing great. I have been back to work/practice since Monday and I am looking forward to play tonight when we play against L.A Clippers. I am a tough kid and don’t like to sit on a bench. I wouldn’t miss a game if it was my choice. But this is a professional level and coaches go with what they have been having or players that have been there before me. For now I am an additional and don’t mind playing that role.

BC: Some critics have been saying that you are not or were not ready for NBA and all that. I am sure you have heard such comments and criticism. What is your reaction?

Hasheem Thabeet: I know people have been talking and saying that I am not ready and or I should not have been drafted by Memphis and therefore suggesting I should have joined another team where there are more veterans so as to learn more and stuff. My answer to them is that; that is not or can’t work for everybody. If you may recall, Memphis Grizzlies drafted Pau Gasol. He was young and almost by himself. But eventually he ended where he is now…with a ring (Lakers).

I look at the situation differently. They drafted me for a lot of different reasons such as potential, progress, presence and production. That is what pushes to me to go out there and learn and strive to be better every day. There is a good reason they pay me $4 M per year.

So while I thank everybody for their advises, comments and criticism and try to understand those who keep doubting me or just hating for no well founded reasons, I wish to inform everyone that I am definitely making a progress and that is why I am able to survive the everyday’s routines of practices and the league itself.

BC: Thank you very much Hasheem. Wish you all the best.

Hasheem Thabeet: Thanks Jeff

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page