AFRICA NA CHINA:NANI ANAFAIDIKA?

china

Viongozi wengi wa Africa wapo jijini Cairo nchini Misri kuhudhuria kongamano kuhusu ushirikiano baina ya nchi zao na China.Rais wetu,Jakaya Kikwete,ni miongoni mwa viongozi wanaohudhuria kongamano hilo.

Sasa kama unavyojua,uhusiano wa China na nchi za Africa ikiwemo yetu ya Tanzania una historia ndefu.Kuna ambao wanasema China ndio nchi pekee duniani ambayo imekuwa “true darling” wa bara la Africa.Wanaosema hivyo wanaangalia vitu kama misaada kutoka China,unafuu wa kufanya biashara na China,masharti nafuu ya misaada na mambo kama hayo.

Lakini katika siku za karibuni,uhusiano baina ya nchi za Africa na China umekuwa ukiongelewa katika namna tofauti.Masuala ya biashara,masoko,misaada nk ndio yameshika hatamu badala ya habari za udugu na ujamaa zilizokuwepo enzi zile kina Nyerere na Mao walipokuwa wakipanda mbegu za ushirikiano wa China na Tanzania.Hapo ndipo suala la kujadili au kufanya tathmini za uhusiano au ushirikiano huu linapokuwa na umuhimu wa aina yake.

Mijadala mbalimbali inazuka kila kukicha.Swali lililopo katika kichwa cha habari hapo juu ndilo linasumbua.Nani anafaidika zaidi na mahusiano haya? Je China wanafaidika zaidi au Africa ikiwemo nchi yetu ya Tanzania ndio inafaidika? Na bila kuficha wala kukwepesha macho,mtanzania wa kawaida ndiye anayefaidika au zaidi na uhusiano huo au ni viongozi wetu?Naomba kufungua mjadala.

Pichani ni Rais Jakaya Kikwete akiwa na Rais wa Misri,Hosni Mubarak huko Misri ambapo Rais Kikwete yupo kuhudhuria Kongamano la Ushirikiano baina ya China na Africa.Picha na Freddy Maro-Ikulu)

Page 1 of 3 | Next page