Busta

Kwa wapenzi wa burudani,kujiachia,kujirusha na mambo kama hayo,Jumamosi ijayo inaweza kuwa siku kinara katika anga za burudani.Ni wakati wa tamasha la Fiesta ambalo mwaka huu limepewa jina la One-Luv na huku ikitarajiwa kwamba miongoni mwa wakongwe na wakali wa muziki wa Rap/Hip Hop kutoka nchini Marekani,Busta Rhymes,anatarajiwa kuwa miongoni mwa wasanii watakaovamia jukwaa kwa minajili ya kuporomosha burudani ya aina yake. Mambo yote hayo yanatarajiwa kujiri katika Viwanja vya Posta pale Kijitonyama.

Busta hivi sasa anatamba na wimbo wake wa Arab Money Remix ambao umezua maneno chungu mbovu kwamba ni wa kibaguzi,kebehi kwa nchi za kiarabu na mambo kama hayo.Katika wimbo huo Busta Rhymes amewashirikisha wakali wengine kama vile P.Diddy,T.Pain,Lil Wayne,Akon,Ron Browz na Swizz Beats.Unaweza kutizama video za wimbo huo katika YouTube. Nitafurahi kama waandishi wa habari watapata nafasi ya kumuuliza Busta Rhymes juu ya wimbo huo.Kwanini aliutunga?Anajisikiaje kuona kwamba umepokelewa tofauti tofauti?Please….

Je upo tayari kwa Fiesta?Kila la kheri.

Feedback / Comments

6 Responses to “BUSTA RHYMES NA FIESTA 2009-ONE LUV”

  1. Comment by ABA on November 18th, 2009 9:54 am

    mzuka sana clouds fm kutuletea huyu msanii hapa bongo

  2. Comment by mr degree on November 18th, 2009 12:06 pm

    hii tabia ya kuleta watu waliochanganyikiwa inatufundisha nini hasa jamani?

  3. Comment by Mr Kas on November 19th, 2009 6:40 am

    Clouds FM ni kazi nzuri sana kuleta wasani wa nje kwa mafunzo zaidi, @ Mr Degree nani alikwambia kuwa mshikaji amechanganyikiwa? hayo ni mawazo finyo tena potovu, kwani kwao wanamueshimu sana….its realy one luv..make sure i dont miss!!

  4. Comment by mr degree on November 19th, 2009 1:06 pm

    we Mr Kas,sasa busta we unamuona mzima? we kweli humjui Busta!

  5. Comment by Dullah on November 20th, 2009 1:35 am

    Mr Degree, we Busta unamjua duh! wabongo wengine wajingawajinga! kama MR Degree!

  6. Comment by Mustafa@voda mail.com on March 19th, 2010 1:41 pm

    Mambo vp wabongo

Leave a Reply