
Kombe la Dunia lipo ziarani nchini Tanzania. Ziara hiyo imezinduliwa rasmi leo jioni nchini Tanzania na Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Ziara ya kombe hilo katika sehemu mbalimbali duniani, ni ishara ya kuwapa fursa mashabiki mbalimbali wa soka ulimwenguni,nafasi ya kuliona kombe hilo “live” na hata kupiga nalo picha kwa kumbukumbu nk. Hizo zote ni miongoni mwa shughuli mbalimbali kuelekea South Africa 2010.
Wakati nikimuangalia Rais Kikwete akiwa amejawa na tabasamu wakati akilinyanyua kombe hilo na kulibusu,nilijiuliza, hivi itakuja tokea kweli siku moja Rais wa Tanzania(yeyote yule atakayekuwa madarakani) kulinyanyua Kombe la Dunia baada ya kulipokea toka mikononi mwa nahodha wa Taifa Stars baada ya kulitwaa?
Well…naamini kila kitu kinawezekana. Sina tu uhakika kama tuna mipango madhubuti(ya mbali au karibu) ya kutimiza ndoto hizo.Tusiishie tu kuliona kombe kwa mbali au kulinyanyua pale tusipostahili.
Picha/Yahya Charahani
Feedback / Comments
4 Responses to “ONE DAY YES…”
Leave a Reply


sending...
Yule Mwakilishi wa FIFA amemuabisha kweli Fest Ledi wetu pale alipomkataza kushika hilo kombe. Mweeh!
Kwani lina mwiko gani wa kumzuia mpaka Festi Ledi! Khaa!
Amemdhalilisha sana
hilo kombe lina thamani kuliko mtu ndo lisishikwe? mbona marais na wafalme wanashikana mikono? hili kombe lina nini cha ajabu? eti linashikwa na mtu mmoja tuu nchi nzima! kisa dhahabu? kwani sisi hatuna dhahabu hapa nchini? kuna haja ya kulipiga marufuku kuja nchin!
Binadamu yeyote mtu ukitaka uheshimiwe wewe na kitu chako wewe.
Ni kutokana na wewe mwenyewe na uwezo wako ulionao. Sio uwezo wako wa kipesa wala uwezo wa kimungu. Ni jinsi unavyojiheshimu wewe.
Ndiyo maana mimi na nchi yangu Tanzania, nina heshimiwa sana na hata kuogopewa na wazungu sehemu nilipo kwa jinsi ninavyojipenda mimi na weusi wangu na nchi yangu ninavyoipenda na kuithamini.
Kombe la dunia halina thamani kwa kuguswa ama kushikwa na mtu yeyote duniani, kwa sababu wao (viongozi) walilolitoa wameamua liheshimiwe kwa njia hiyo, ili lionekane kuwa lina thamani, na wengi wamelithamini.
Huu ni mfano mzuri sana kwa Watanzania wenzangu wanaoishi nchi za nje. Kujiheshimu wenyewe na kujipenda wenyewe na kuithamini nchi yao walikotoka ni kitu cha muhimu sana.
Jipendeni wenyewe jinsi mlivyo na rangi zenu. Ipende lugha na nchi yenu na kuithamini na hata kutamani kurudi nchini kwenu Tanzania, hata kama kuna shida gani.
Kombe la dunia, tunaonjeshwa na kutambiwa na wahusika, kwa kuonyeshwa jinsi wenzetu wanavyokuwa wanalipata na kulibusu sio kinadharia tu, bali kwa kuwa nalo kiukweli.
Festi ledi wetu, hana thamani kwa hao waliopanga kuliheshimu kombe hilo. Na wako tayari kumwaibisha yeyote anayevunja amri zao FIFA, walizoziweka kama walivyofanya kwa Mh. Kikwete. Mimi sikupendezwa na hilo.
Dhahabu ya kombe hilo la dunia yawezekana ni kutoka Buzwagi Kahama Shinyanga ama Nyarugusi Mwanza ama Mwadui Shinyanga, lakini kwa sababu, hatukulijenga sura yake lilivyo tu, haturuhusiwi kuligusa kombe hilo Watanzania, ila kupiga picha pekee.
Kwa imani yangu. Yote haya yasingetokea kwa kuwadhalilishwa Viongozi wetu na sisi Watanzania, kwa kitu kidogo kama kombe la dunia kinachowaehusha watu duniani na kuwasahaulisha ubinadamu wao iwapo sisi Watanzania kama tungekuwa tumejipenda wenyewe, kwa kudai, siku zilizopita, kuombwa samahani kwa kutawaliwa na hao Wakoloni.
Katika enzi za ukoloni kuna mengi yasiyokuwa mema tumetendewa. Kwanini Wakoloni hawa hawataki kutuomba msamaha? Na si hivyo tu, wakome kuendelea kutunyonya hata sasa hivi.
It’s Great To Be Black=Blackmannen
English man used to say that “usually charity begins at home” so by celebrating with just a visit of the FIFA world cup without win the trophy is not such a proud thing, what I think is to put effort from family level to the national wide to prepare our young players so that one day in future times we shall celebrate after wining at the final match.
Gift Shine