Mamilioni wamekuwa wakiangalia show yake. Kwa takribani miaka 25,jina la Oprah Winfrey limekuwa miongoni mwa majina yanayotambulika kwa urahisi zaidi duniani.
Ni miongoni mwa wanawake matajiri kupindukia na pia wenye uwezo mkubwa wa kubadilisha muelekeo wa takribani kitu chochote anachoamua kukiweka ubavuni mwake.Oprah akisema kitabu fulani ni kizuri,basi usishangae kikienda kuwa “best seller”.Akisema yeye nyumbani kwake anatumia aina fulani ya dawa kusafishia nyumba yake,ukienda madukani na kuambiwa zimekwisha,hutakiwi kushangaa.Ni Oprah factor.
Kuna imani kwamba yeye ni miongoni mwa watu muhimu sana kwa Rais wa Marekani,Barack Obama kwani alichangia kwa kiasi kikubwa ushindi wake kuelekea “Jumba Jeupe”.Oprah pia ni miongoni mwa watu maarufu wa kwanza kabisa kumkubali Obama na kusema wazi kwamba anataka jamaa agombee urais.Aliona mbali.
Sasa habari ni kwamba ameamua kuhitimisha au kusitisha show yake ifikapo tarehe 9 September mwaka 2011.Kwa maana hiyo bado kuna muda wa watu kuendelea kumfuatilia Oprah Winfrey ambaye bila shaka ni “mwana-mapinduzi” linapokuja suala la “Talk Shows”.Oprah anatarajiwa kutangaza rasmi uamuzi wake huo katika show itakayorushwa hewani hivi leo.
Je,fununu zinasema atafanya nini baada ya kuipa kisogo show yake? Unaweza kupata fununu hizo kwa kubonyeza hapa.
Feedback / Comments
Leave a Reply


sending...