Machupa-FrontBC

Machupa ni mfungaji hodari. Usemi huo pekee unatosha kumuelezea Athuman Iddi Machupa (pichani) mshambuliaji kijana ambaye kwa upande wa Tanzania, aliwika zaidi alipokuwa akichezea timu ya soka ya Simba maarufu kama “Watoto wa Msimbazi”.

Hivi leo Machupa anasakata kabumbu nchini Sweden akiwa na timu ya Vasalund IF.

Niliwasiliana na Machupa hivi karibuni na kumuuliza maswali machache. Haya hapa mahojiano yetu;

BC: Mpaka sasa mambo yanakwendaje hapo Sweden?Unachezea timu gani na ipo daraja la ngapi?

Machupa: Kwa upande wangu hapa Sweden maisha yanakwenda poa kaka.Ninachezea timu inayoitwa Vasalund IF ilikuwa katika ligi ya Superettan (ligi ya pili kwa ukubwa hapa Sweden) lakini kwa bahati mbaya tumeshuka daraja hadi la kwanza..

BC: Umeshakaa Sweden kwa muda wa kutosha sasa.Unapaonaje na zaidi unaonaje nafasi za kuendeleza soka lako?

Machupa: Kwa sasa kaka napeleka mwaka hapa na kwa upande wangu mi naona maisha ni mazuri na hata nafasi ya kusonga mbele kwangu ni kubwa mno.Nazidisha bidii katika kila kitu na inshallah nitafanikiwa zaidi na zaidi.


BC: Kama mgeni katika nchi ya watu,ni mambo gani ambayo ilibidi ukabiliane nayo kwanza? Hapa nazungumzia mambo kama vile lugha,vyakula nk

Machupa: Of coz lugha kaka ni ngumu. Lakini nashukuru jamaa wamenishughulikia masuala yote ya muhimu ikiwa ni pamoja sehemu ya kujifunza lugha yao.Na kuhusu chakula; kwa kusema ukweli ni kizuri tu. Hakina tofauti sana na cha nyumbani Tanzania kwa sababu najipikia mwenyewe chakula ninachojisikia kula.Hali ya hewa nayo ilikuwa changamoto lakini taratibu ninazoea.

Machupa-Jikoni“Hebu ngoja nicheki kama vitu vishaiva”

BC: Una ujumbe gani kwa vijana wengine wanaosakata soka nyumbani Tanzania?

Machupa: Ujumbe wangu kwa vijana wanaosakata soka na hususani waliopo nyumbani ni kwamba waheshimu soka kwani soka ni kazi kama zilivyo kazi zingine zozote.Ukiheshimu soka hakika utafanikiwa.

BC: Mwakani ni mwaka wa kombe la dunia.Safari hii kipute kipo Africa.Nini matarajio yako kwa nchi za Afrika?

Machupa: Ni changamoto kubwa kwa timu za Africa ambazo zimefanikiwa kuingia katika finali hizo. Tusubiri tuone kwa sababu nina uhakika watajiandaa vizuri. Nina uhakika hatutosikia madai ya posho. Nina imani watatuwakilisha vyema kabisa,sina wasiwasi na hilo. Ila nahisi Ghana watafanya vizuri. Nawa-support.

Machupa-ZoeziniMachupa akiwa mazoezini na timu yake.Anaonekana kulia katika picha akijaribu kutuliza mpira chini.

BC: Una lolote la kuongeza kwa mashabiki wako?

Machupa: Mashabiki ndio kila kitu.Nawapenda na ninawaheshimu sana na hakika bila wao hatuwezi songa kwa sababu wao ndio wanaotukosoa pale tunapokosea.I love all my fans popote walipo.

Feedback / Comments

5 Responses to ““VIJANA WAHESHIMU SOKA KAMA KAZI ZINGINE”-MACHUPA”

  1. Comment by BLACKMANNEN on November 24th, 2009 11:56 pm

    Mimi ninafurahi sana ninapowaona vijana wetu wakipata nafasi za kucheza mpira nchi za nje, kama tunavyowaona Machupa, Boban na Kaniki.

    Watanzania tumezoea kucheza mpira “MIDOMONI” mwetu. Sasa, Watanzania hawa watakaporudi nyumbani, watatusaidia sana kuibadirisha sura ya soka letu, kwa kuwa watapata elimu ya nje ya kucheza mpira wa kweli bila ya porojo nyingi.

    Pia kwa vile wanatufahamu vyema tulivyo na imani zetu za giza, katika mambo ya mpira. Nina hakika watatusaidia kutuondolea au kutushawishi tuachane na imani za aina hiyo.

    Ombi langu kubwa kwa “Wataalamu” wetu hawa, ni kwamba, wanapokuja nchi za watu waje na nia ya kujifunza kile kilichowaleta kwa manufaa yao na sisi Watanzania. Mishiko ya “nguvu”, wanayopewa katika mikataba yao na timu zinazowachukua, isiwafanye wawe na “macho miamia” kwa mali za watu, kwa vitu vyote ving’aavyo.

    Ni rahisi sana kujikuta ukinawishwa mpira au kitumbua chako kumwagiwa mchanga kama tulivyoona kwa jirani yetu kutoka Congo “Yannick Bapupa”. Mtego ulikuwa ni rahisi sana, na sasa kwake vyote alivyovipanga vimekuwa ni histora tu. Tujiheshimu.

    It’s Great To Be Black=Blackmannen

  2. Comment by mr degree on November 25th, 2009 3:26 pm

    hawa jamaa wakati wanaanza kucheza mpira walikua wakubwa kiumri kuliko mimi!kwa mfano jana nimeona boban ananadiwa kwenye mtandao wa klabu yake kama kijana mwenye kipaji kutoka Tanzania na ana miaka 22!nikajiuliza 22?jana nilitafakari sana kwa kweli, maana yeye alikua mkubwa kuliko mimilakini ghafla nimempita umri! labda wataalam wa masuala ya ukuaji wa binadamu wanisaidie mimi nina matatizo gani mpaka nakua haraka kiasi cha ku-overtake umri wa wakubwa zangu! any way kila la heri mzee machupa!

  3. Comment by Titi on July 22nd, 2010 6:19 am

    Ongera sana machupa,songa mbele usigeuke nyuma onyesha mfano na wengene watafuata kwani maisha ni kujituma na ni popote,litangaze jina la nchi yetu,miaka ya mbeleni na sisi tuwemo kwenye kombe la dunia mungu mkubwa.keep it up

  4. Comment by christopher on August 27th, 2010 3:35 am

    hongera sana machupa,niliyategemea hayo tokea wakati unachezea simba kwa kuwa uwezo wako ulukuwa juu.endelea juu na mungu akupe nguvu ili siku moja uwasaidie vijana wanaochipukia…………..nakumbuka sana goli ulilofunga wakati wa mechi ya yanga baada ya kukimbilia mpira ukiwa na salum swedi ukamfinya na kipiga kiki iliyozaa bao pekee kwa simba .

  5. Comment by Moses Mlengera on November 6th, 2010 1:32 pm

    Hongera Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kushinda nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa awamu ya pili.
    Mungu akujalie afya njema na nguvu tele ili uweze kuwatumikia watanzania kwa uwezo wako wote.
    KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

    Moses M. Mlengera
    Box 3003, Morogoro.
    mlengera@yahoo.com

Leave a Reply