Sijawahi kupata nafasi ya kufanya nao mahojiano ili kujua kwa kina maana au chanzo cha jina Nako 2 Nako.Pamoja na hayo,wengi wanawakubali na kwa mambo mbalimbali,yakiwemo binafsi,wameshagonga vichwa vya habari mara kwa mara. Walianzia A-Town/City kabla ya kuweka kambi jijini Dar.
Hivi karibuni wamefyatua kitu kipya.Wimbo unaitwa Ndani ya Nyumba ambao kutokana na Producer wake,Hermy B(kutoka B’Hitz Music) ni wimbo wa kustarehesha zaidi kuliko kuelimisha au vitu kama hivyo.
Kitu ambacho kimekuwa kikinivutia kutoka Nako2Nako ni aina yao ya kughani.Ina utofauti fulani hivi ambao kimsingi ni muhimu.Nimewahi kusisitiza katika “kijiwe” fulani kwamba kama mtu anataka kupata mafanikio fulani katika chochote anachotaka kukifanya,ni muhimu akawa “mbunifu”.Kwenye muziki hali ni hiyo hiyo.Lazima utoke tofauti.La sivyo,watu watakusikiliza na kukuacha solemba haraka iwezekanavyo.Huna jipya.
Wasikilize Nako2Nako katika Ndani ya Nyumba
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Feedback / Comments
6 Responses to ““NDANI YA NYUMBA”-NAKO 2 NAKO”
Leave a Reply


jamaa mkali sana na amekuja na identity yake inayomtofautisha na wengine katika hip hop! tatizo liko palepale jamani bangi! mtu unaona kabisa ana kipaji na kama akitulia anaweza kufika mbali katika muziki,lakini waapi bangi kwa kwenda mbele.ukiuza utaambiwa mbona wamarekani wanavuta na kazi wanafanya kama kawa!wanaiga kila kitu hao jamaa kutoka kwa wamarekani. kwa mtindo huu wa wasanii wa kibongo kukimbilia bangi na maunga sidhani kama watafika popote! wanaiga kila kitu hawa! jiga akivuta bangi naye atavuta tuu, akitembea na mademu wengi naye atatembea tu na mademu wengi, akiendesha gari kwa kasi naye ataendesha kwa kasi! ilifika mahali wakaanza kuiga mambo ya kuuana eti kisa TUPAC na BIGGIE waliuana. wakaanza kuchomana visu na kupuliziana sumu!mambo ya kuiga ndiyo yaliyopelekea vifo kina Stive 2k, dandu na john mjema!waache bangi na hayo maunga kama kweli wanataka kufika mbali, otherwise watakuwa wanapoteza muda tuu.kuendelea kufanya kazi nzuri kunahitaji utulivu wa akili sasa kama akili yenyewe ndio hiyo imejaa moshi wa unga na bangi,unategemea nini? wenzetu ulaya na marekani msanii anaweza akafanya starehe zake zote na bado akawa msanii mzuri, kwa kuwa wenyewe wanatungiwa nyimbo na kila kitu kinafanywa tuu studio.lakini hao bongo fleva ambao kila kitu wanafanya wenyewe kuanzia utunzi hadi kupangilia muziki studio, hawahitaji kuzikoroga akili zao kwa bangi wanatakiwa kuzituliza akili zao hasa. lazima ifike mahali waambiwe ukweli. tunaweza kuwaokoa hawa vijana wenye vipaji kwa kuwaambia ukweli tuu!habari ndio hiyo najua hamuwezi kukubali nnachosema kwa kuwa nyinyi ni wabishi sana na mnajua kila kitu!
Unayejiita Mr. Degree!
Vifo vya mtoto wa Dandu na John mjema vinahusikaje na mambo unayodai ni ya kuiga ya wasanii wa Bongo flava toka kwa wale wa marekani?
Marehemu mtoto wa dandu alifariki kwa ajali mbaya ya gari na John Mjema yasemekana alijiua. Sasa kuiga kunahusiana vipi na marehemu hawa. Hebu acha kuoanisha vitu visivyo na uhusiano. Waache marehemu hawa wapumzike kwa amani, amina.
Pia ni vema ukafahamu kuwa wasanii wa rap nchini marekani huandika mashairi yao wenyewe kama ambavyo wasanii wa bongo flava wanavyofanya.
Pia kwa sasa nawapongeza wasanii wengi wa bongo flava kwa kuanza kuweka utamaduni wa Tanzania ktk sanaa zao. Mfano mzuri ni mavazi yao ambayo yana picha mbali mbali za wasanii wa nyumbani, lugha kiswahili, picha za viongozi wa Afrika, n.k.
Mbali na hapo, nafurahi sana kuona muziki wao unazidi kukua kwa kasi ya ajabu. Hii inatokana na changamoto wanazopeana wao kwa wao ktk kukabiliana na vipaji vinavyoibuka na kuzidi kukuwa kila kukisha.
Hata hivyo, ktk swala la matumizi ya madawa ya kulevya na vilevi vingine, mimi ningewashauri wasanii wale wa bongo flava wanaofanya hivyo, waachane na tabia hiyo kwani ina madhara makubwa kwao na jamii inayowazunguka.
Good luck Nako 2 Nako ktk safari yenu ya sanaa ya BONGO.
mumngu awapumzishe kwa amani mjema na dandu! lakini ukweli lazima usemwe dandu alikua hawezi kuendesha gari kawa taratibu hata kidogo. hii sikuhadithiwa nimeshuhudia mara nyingi tuu akiendesha gari kama yuko mashindanoni! kuhusu mjema nae sijui unachomtetea kitu gani? hivi unadhani nina wivu na hao jamaa au? kama huna pointi kaa pembeni usitetee vitu visivyo na msingi hapa! asilimia zaidi ya 80 ya hao bongo fleva ni wavuta bangi wazuri na hawafichi wanaisifia kwenye nyimbo zao kila siku! wanaita majani, moshi, nyasi, cha arusha cha dodoma n.k! labda wewe umepitwa na wakati husikiklizi nyimbo zao lakini sisi tunaosikiliza tunaelewa wanaimba nini
Wewe Mr Degree huna mpando. Unachofanya hapa ni kutumia mdomo km mali yako bila kujua unachoongea. Hujaanza kufuka leo, bali toka kktambo. Baki kuwa zuzu.
haise mazeeee mko juu sanaaa
don leave u’r war with tz’s hiphop
dat’s all
oya mazee n2n ni kundi la kwanza e-afrika kwa kuwakilisha hiphop ganstar oru can said hiphop ganstar, hakuna msaani wa tz anaye mshinda izz wa wazi kwa kuleta swag kali e.g mzuka,hainakwere mkazuzu,mzufuka bilakusahahu nako2nako kila ngoma wanayotoa ni hit eg ndo zetu,bang ,bang remix,mchizi wangu,hatuwezi,najua clouds wameanza kubana kutokana na roams za mitaaa it means hawana misimamo as redio kula kina chosemekana haina maana kundi swaga zimeeisha not we thnx eatv for u’r support.bado tanaona makali ya nako2nako mfano mpango mzima ninew swaga kila kona show love ni mf.wa kuigwa na wasani bongo,bado junior nakos 2nakuja lemi say nako2nako we nation.