MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

EvanderHolyfield

BINGWA wa zamani wa masumbwi katika uzito wa juu duniani, Evander Holyfield wa Marekani amepanga kwenda Uganda kuzichapa na Francois ‘White Buffalo’ Botha wa Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa waratibu wa pambano hilo la kimataifa, wababe hao watazichapa Januari 16, wakiwania mkanda wa dunia wa WBF.

Pambano hilo ambalo litavuta hisia za wengi, litapiganwa siku hiyo katika Uwanja wa Taifa wa Mandela, mjini Kampala, Uganda. Kwa habari zaidi,bonyeza hapa.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

2 Responses to “EVANDER KUZICHAPA NCHINI UGANDA!”

  1. Comment by mr degree on November 27th, 2009 8:37 am

    ndondi zimepoteza muelekeo siku hizi. hazina msisimko kabisa! ndondi gani zinapiganwa na walokole?yaani ndondi zinahitaji mabondia wakorofi lakini siku hizi wapi, mabondia walokole ndio wanapigana! huu mchezo ni wa ugomvi sasa inakuaje watu wapole waucheze? yaani toka Tyson kupoteza muelekeo ndondi za uzito wa juu zimekosa muelekeo! hakuna hamasa kabisa tunahitaji watu wenye vurugu kwenye ndondi. yaaani wale wanaobaka au wanaotukana hovyo. hapo ndondi ndio zitakuwa na mvuto! waganda wangemleta Tyson au hutton labda kidogo watu tungesisimka lakini EVERNDER? ulokole na ndondi wapi na wapi?

  2. Comment by hombiz on November 28th, 2009 1:32 am

    Yaani wewe unayejiita Mr Degree uelewa wako unakufanya usadiki kuwa kubaka na kutukana hovyo ni sifa ya bondia bora!? Kwa nini unapenda kufuka!? Kuna Mabondia wengi ambao hawakubaka wala kutukana hovyo na walivuma zaidi ya Tyson. Do a research.

Leave a Reply