MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

HBC

Wikiendi iliyopita,jiji la Dar-es-salaam liligubikwa na homa ya “Fiesta”.Kuna ambao wamesema kama hukuhudhuria haifai hata kuomba kusimuliwa ilivyokuwa kwani hakuna jinsi ya kusimulia!

Wengi walikuwa wakielezea jinsi mwanamuziki mkongwe wa hip hop kutoka nchini Marekani,Busta Rhymes, alivyoweza kukonga nyoyo za mashabiki wa muziki.Wanasema japokuwa jamaa alilikwaa jukwaa wakati mida imeshakwenda sana,aliweza kuonyesha thamani yake kwa kuwapeleka mbio mashabiki wa mwanamuziki huyo.

Mimi sikuwepo.Nafuata ushauri wa kutokuomba hata kusimuliwa sana mambo yalivyokuwa.Niliyoyasoma katika vyombo mbalimbali vya habari  yanatosha.Lakini donge nililonalo ni kutokuwepo kuwaona HBC(Hard Blasterz Crew) wakisimama tena jukwaani kwa pamoja.I would have loved that.HBC ni miongoni mwa makundi ambayo binafsi naamini kwa dhati kwamba yalichangia sana kuuweka muziki wa kizazi kipya hapo ulipo.Isitoshe nilibahatika kuwa mtu wa karibu kwa vijana hao wa HBC enzi hizo walipokuwa wanaanza kuiteka fani ya muziki wa kizazi kipya.

Napenda kuheshimu watu au vikundi vinavyoanzishwa na kisha kujenga msingi wa jambo fulani.HBC ni miongoni mwa makundi hayo.Swali ni je,HBC ndio wamerudiana na labda tutarajie albamu kutoka kwao? Najaribu kuwatafuta ili wajibu swali hilo hapo juu wenyewe. Makundi mengine ambayo yalikuwepo siku hiyo ni pamoja na Daz Nundaz…wale wazee wa Kaaamandaaa..unawakumbuka? Wateule pia walikuwepo…yaani Jafarai,Mchizi Mox bila kumsahau Jay Moe.

Wimbo waliouimba majuzi ni huu hapa unaoitwa Niamini.Sikiliza hapo chini.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Pichani kutoka kushoto ni Terry Msiagi(aka Baba Ray),William Shundi(Big Willy) na Joseph Haule(Professor Jay)

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

4 Responses to “NATAMANI NINGEKUWEPO!”

  1. Comment by Mike Mhagama on November 27th, 2009 1:15 pm

    Salute! Good Job BC…Huu ni moja kati ya ujio uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu.Bado Kwanza,GWM etc.

    Nice work.

  2. Comment by hombiz on November 28th, 2009 1:37 am

    Safi sana HBC! Ninyi ndio wasanii mlioleta mapinduzi rasmi na halisi ktk sanaa hii ya bongo flava.

    Nategemea makubwa toka kwenu.

    STAY FOCUSED!

  3. Comment by Peter charles on December 4th, 2009 6:16 am

    Dah! ebwana nimefurahi sana kuona kundi kama HBC limerudi tena kwenye game ebwana fanyeni kazi wanangu hbc ni crew ya kiutu uzima au sio wana nafurahi kumwona fanani,big wiily,prof jize dah najisikia amani sana now mziki unarudi sasa tusimamishe nguzo isiyumbe tena BIGAP!!..

  4. Comment by Akihito on December 19th, 2009 1:54 pm

    kudadeki!!
    hawa watu wangu wote…
    Terry na willy najua mnakumbuka sana tulivyokuwa tukiwakomesha kwenye mechi zetu pale upanga primary school.Jay,tangu tukiwa na kijana Emma (iliyokuwa mobitel Tanga) hadi maskani ya brooklyn…yeah, huu ni ujio ambao,mpenda bongo flava anafaa arukeruke kwa furaha..imetulia mno..tupo wote makamanda…!

Leave a Reply