MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

TigerMcheza golf maarufu,Tiger Woods,33 amepata ajali na kuumia karibu na nyumbani kwake huko Windermere,Florida. Tiger alikuwa akiendesha gari lake aina ya 2009 Cadillac SUV ambapo aligonga fire hydrant kabla ya kuuvaa mti uliokuwa pembeni.Ilikuwa mida ya saa nane na dakika ishirini na tano alfajiri. Ilibidi mke wake atumie golf club kupasua kioo cha nyuma cha gari la Tiger ili kumtoa. Mke wake alisikia mlio wa ajali kwani na kukimbilia nje kwani ajali ilitokea karibu kabisa na nyumbani kwa star huyo wa mchezo wa golf duniani.

Hata hivyo tofauti na habari zilizokuwa zimeenea hapo mwanzo,Tiger hakuumia sana katika ajali hiyo mbali ya kupata michubuko kadhaa usoni. Ametibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani kwake. Tovuti yake imeielezea ajali ya Tiger kuwa “ndogo”.

Historia ya Tiger Woods katika michezo ni miongoni mwa historia zenye mvuto wa aina yake.Kwa mujibu wa tovuti yake,ameshashinda zaidi ya mashindano 93. Aliweka historia ya kuwa kijana mdogo zaidi kushinda taji maarufu la Masters.Alikuwa na umri wa miaka 21. Tiger amesomea Chuo Kikuu cha Stanford.Alifundishwa kucheza mchezo wa golf na baba yake mzazi,Earl.Baba yake alikuwa mwanajeshi,mmarekani mweusi wakati mama yake ana asili ya Thailand.Mwaka jana Tiger Woods alitajwa kuwa mwanamichezo aliyelipwa zaidi akiwa amekusanya jumla ya dola milioni 110 kutoka katika michezo na matangazo ya biashara.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

4 Responses to “TIGER WOODS APATA AJALI NA KUUMIA”

  1. Comment by hombiz on November 28th, 2009 2:13 am

    Pole Mr. Hoods!

    Ulikuwa unaelekea wapi majira ya saa nane na dakika ishirini na tano za usiku! Hii ajali ina utata Mr. Woods. Nasikitika kusema hivyo lakini hivyo ndivyo ninavyodhani!

  2. Comment by eva moses on November 28th, 2009 1:31 pm

    per TMZ, his wife caused all the injuries on him…they were having a fight so he decided to leave the house.

  3. Comment by Simon Kitururu on November 29th, 2009 12:22 pm

    Mmmh!

  4. Comment by mr degree on November 30th, 2009 12:15 pm

    anadai yeye sio mwafrika ingawa rangi yake inamsuta! sidhani kama anastahili kupewa pole kwa chochote kibaya kitakachomtokea!

Leave a Reply