Warembo wanaoshiriki katika mashindano ya kimataifa ya urembo ya Miss East Africa 2009 wataanza kuwasili nchini wiki hii(au wameshaanza kuwasili) tayari kwa mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika tarehe 18 mwezi wa 12 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Aidha, warembo watakaoiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo wanatarajiwa kutangazwa kesho kutwa baada ya kamati maalumu iliyopewa jukumu la kuratibu zoezi hilo kukamilisha kazi yake.
Mashindano ya Miss East Africa mwaka huu yanatarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake kutokana na Nchi zinazoshiriki mashindano hayo kuchagua warembo wenye viwango vya hali ya juu ili kuziwakilisha katika mashindano ya mwaka huu
Miss East Africa 2009 itashirikisha warembo kutoka katika Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, na Mauritius ambazo zote zimeshathibitisha ushiriki wao.
Mashindano hayo makubwa ya urembo kwa ukanda huu wa Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Limited ya jijini Dar es salaam.
Miongoni mwa makampuni yanayodhamini mashindano hayo kwa mwaka huu ni pamoja na Kunduchi Beach Hotel & Resort, EATV, Kings & Queens Worldwide, CMC Automobiles Limited na AKO Catering Services Ltd.
Hizi hapa chini ni picha,majina na umri wa baadhi ya washiriki wa mashindano hayo.

Rebecca Getachew (23) Ethiopia,
Asli Osman Mahamud(20)-Somalia
Fatma Abdilahi (18)-Somalia

Dalysha Nirena Doorga (21)-Mauritius

Tabitha(20)-Kenya

Queen Belle Monique (23)-Burundi
Feedback / Comments
5 Responses to “HERE COMES MISS EAST AFRICA!”
Leave a Reply


the chicks wako hot ila mbona sioni m-tz?
Jamani huku si kuoneyana sasa yupo wapi Miss TANGANYIAKA wetu nasi tujivunie??
this will be fantastic context better
ina maana nchi ya ethiopia, mauritius na somalia na zenyewe ni east africa? mbona mnataka kuvuruga watu vichwa…..
Hmm inaonekana kuna “samsin”behind..where is awa Tz malkia..im sure kawafunika wote…!!walioko wako fine,hawatishi kiviiile…ha ha haa