Rais wa zamani wa Marekani,Bill Clinton na mke wake,Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani hivi sasa,Hillary Clinton, wapo njiani kupata “mkwe” hivi karibuni kwani mtoto wao pekee,Chelsea,amechumbiwa.
Chelsea amechumbiwa na rafiki yake,Marc Mezvinsky. Habari zinapasha kwamba kitendo hicho cha kuchumbiwa kilifanyika hivi karibuni wakati wa kusheherekea sikukuu ya Thanksgiving. Chelsea na Marc walikutana Washington,DC na baadaye kuendeleza urafiki wao walipokuwa wanasoma katika Chuo Kikuu cha Stanford. Marc ambaye hivi sasa ni Investment Banker ni mtoto wa aliyewahi kuwa Mwakilishi kupitia chama cha Democrat kutoka Iowa,Edward Mezvinsky na mkewe Margolies-Mezvinsky ambaye pia aliwahi kuwa Mwakilishi kupitia tiketi ya chama cha Democrat kutoka Pennyslvania.Wote wanaishi New York hivi sasa. Wanatarajiwa kufunga ndoa katika majira ya summer hapo mwakani.
Bila shaka yule jamaa kutoka Kenya aliyewahi kutangaza kwamba angependa kumuoa Chelsea atakuwa amehuzunika kupita kiasi.Usijali best,ndio maisha.
Feedback / Comments
One Response to “CLINTON KUPATA MKWE HIVI KARIBUNI!”
Leave a Reply


Yaa jamaa wanowana kwa kujuana majina suo kila mtu anaweza kuoa tu.