
Bila shaka unaitambua sura yake na bila shaka umewahi kumsoma au kusoma vitabu vyake. Anaitwa Ngugi wa Thiong’o. Ni miongoni mwa wanazuoni na waandishi ambao bara la Africa linajivunia kuwa nao.Je nikikupa nafasi ya kumuuliza swali Ngugi ungependa kumuuliza nini? Tuma swali lako kupitia sehemu ya maoni(comments) au kwa kutumia barua-pepe info at bongocelebrity dot com
Feedback / Comments
16 Responses to “UNA SWALI KWA NGUGI?”
Leave a Reply


sending...
Furaha kuweza kumuuliza mwandishi huyu mahiri wa vitabu.Swali langu ni ili;ninaweza pata wapi vitabu vyako(vya zamani na vipya)kwa sisi tunaoishi Marekani?jee?vipo ktk internet?
I really get reminded when I saw or even hear about a legend goes by the name Ngugi wa Thiong’o! Wht I am curious to know from him is if he still write down some series of new interesting books or he is now retire? And currently what exactly is he doing?
Gift Shine.
I have read a lot of books from Ngugi Wathiong’o. Your books are very impressive. Can You tell me just a little what motives led you to write those books which actually are fond of good stories, educative, hence full of criticim? on top of that are You still on line?
Namkubali sana Ngugi..swali ningependa kujua kulichomfanya kwenda kuishi uhamishoni ni nini hasa?
2.Aliporudi alivamiwa na mkewe kubakwa (POLE SANA) Je ufumbuzi wa hili umekuaje.
3.Vitabu vyake vingi vili based upande wa ukoloni sasa hivi ana mpya gani?
Napenda kazi zake natamani kuandika vitabu kama yeye ila nina wasiwasi na pia naogopa Tabaka fulani halitaki kukosolewa thus why siandiki.
The river between, kama sijakosea ndo mwandishi wake vile eeeh! I was too lazy to read i wish i read that story tho.One day when i go back home will do.
Jina la Ngugi wa Thiong’o sio geni masikioni mwangu. Yawezekana ni kutokana na mipishano yangu kwa kile nikipendacho na kile Mwandishi huyu Mahiri, akiandikacho au alichowahi kuandika hakikunifanya kusoma au hata kupitisha macho vitabu vyake.
Hali kama hiyo namwomba Mzee Ngugi, aichukulie kama ni moja ya changamoto kwake. Kwa sababu, ijapokuwa mtu huwezi kusoma vitabu vyote viandikwavyo, lakini unaweza kusoma japo kimoja kwa mwandishi mahiri kama huyu.
Kwa mfano, nakumbuka kusoma vitabu vilivyoandikwa ama kuganiwa na Mwalimu Nyerere, “1st and 2nd Scrambe” kwa upande wa siasa na upande wa kielimu niliwahi kusoma vitabu shuleni vya “Hekaya za Abunuwasi, Bulicheka na mke wake Elizabeta”. Sijavisahau.
Kwa sasa nimejikita kutoa maoni yangu katika Blogs mbalimbali mitandaoni, na mimi jina langu sio geni mitandaoni, lakini nazipendelea zaidi Blogs zitumiazo kiswahili. Kwa hiyo kama Ngugi wa Thiong’o atumia zaidi kiswahili katika uandishi wa vitabu vyake, nina hakika nitakutana naye uso kwa uso, nitavisoma.
Ombi langu kwake Ngugi wa Thiong’o, naomba aandike vitabu vya kisiasa. Kwa mfano shughuli mbalimbali alizokuwa akizifanya Baba Wa Taifa la Kenya Marehemu Jommo Kenyatta wakati wa uhai wake au habari zozote kuhusu Afrika yetu ambazo tungependa kuzijua sisi na vizazi vyetu vijazo.
Ulimwengu wa leo ni mdogo kutokana na tekinolojia tuliyo nayo. Habari tunazozisoma sasa hivi, haziishii mezani kwetu peke yetu, wengi wanazisoma. Kazi bado unayo Mzee Ngugi wa Thiong’o. Endelea kutuelisha Mzee.
It’s Great To Be Black=Blackmannen
Wow! I love a Grain Of Wheat! Your characters are really impressive in this novel especially the character of Mugo, Kihika, Karanja and Mumbi. My question to Ngugi are,What made you to be in exile? Is it true that your wife raped when you came back to Kenya and were you there when this happened?
Hi my Friend;I only wanted to know how many books have wrote to us as the readers of u’r books.How can u help young generation with the same talent like u’rs so that they inherity & perpatuate the the writings for the coming generations?
sijawahi kupenda vitabu vyake! so sina la kumuuliza na kama nikikutana naye nitamuangalia tuu basi!
Namkubali huyu mzee kwani ana kipaji halisi. Nimesoma kwenye website yake lakini sijaona mahali ambapo ameelezea kuhusu familia yake kwa ujumla..! ana watoto wangapi? wako wapi na wanafanya nini?
wewe mson unaogopa kuandika vitabu kisa unawasiwasi tabaka flani halitaki kukosolewa? usiogope wee andika mimi nitasoma najua utaandika vichekeshio tuu!na wasomaji wa vichekesho tupo wengi. andika tuu ondoa hofu wasomaji tupo wengi!
Ni miaka mingi toka kiandikwe kitabu cha “The River Between”, na mimi nimesoma kitabu hicho miaka kadhaa iliyopita. Naomba kuuliza muono wako juu ya mahusiano kati ya dini kuu tatu Uislam, Kikristu na Waebrania na tamaduni zetu za kiafrika, na hasa hizo mbili za kwanza.
Mimi nimesoma vitabu vyake nilivyokuwa Secondary i loved them. Pole sana na matatizo yaliomkumba alivyorudi kwao Kenya. Jamani kutoa critic kwa hizi serikali zetu ni noma sana unaweza kufanyiwa vitu vya ajabu sana. Swali langu kwake ni 1. Je siku hizi anaishi wapi?
2.Je kuna vitabu gani vipya ambavyo tunaweza kununua tukiwa ugaibuni?
3. Vitabu vya zamani je vinapatikana wapi?
4. Maisha yake kwa ujumla atuambea kwa sasa anafanya shughuli gani apart from writting books?
SWALI KWA NGUGI…TUTAPATA WAPI VITABU VYAKE KWA WAKAZI WA ARUSHA NA DAR ES SALAAM NA JE ANA MATOLEO MAPYA?
umenikumbusha mbali sana…kwa mbali makuyu na kameno,inaonekana kama vile simba aliyelala, katikati yao kuna ziwa, ziwa la kutibu(kwa wale waliokwenda kutahiriwa na mambo kama hayo) yaani hakika ,umenikumbusha mbali sana..kijana wako Waiyaki na mdingi wake Chege haha! wewe upo ulikuwa makini…nilipenda sana kusoma vitabu vyako,hasa hicho cha the river between.swali langu ni kuwa,pamoja na kuwa wewe ni mwandishi makini,je kuna mwandishi yeyote aliyekuwa akikupa msukumo wa kusoma vitabu vyake?
What made some Kenyan, if not all, hate you so much that you have been forced to live in exile. What have you done to them. It is very unusual to hate a country man to such extent.
Otherwise i enjoyed reading your novels.
Likwe