MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

KabweDAVID Kafulila, mwanachama mpya wa NCCR-Mageuzi, ambaye amekuwa akitumia uhusiano wake binafsi na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, kama kete ya kisiasa katika ugomvi wake na uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), amesema Zitto ni mzushi.

Kafulila, ambaye alikuwa Ofisa Habari wa CHADEMA kabla hajavuliwa cheo hicho na kukimbilia NCCR-Mageuzi, alisema hayo jana Dar es Salaam, wakati akijibu taarifa kuwa mbunge huyo amekanusha kumsaidia magari matatu ya kufanyia harakati za kujijenga kisiasa mkoani Kigoma baada ya kujiunga na NCCR-Mageuzi.

Msukumo wa Kafulila kumshutumu Zitto umetokana na tetesi kwamba amekuwa anatumia barua pepe ya mbunge huyo kusambaza taarifa zinazoleta chokochoko katika CHADEMA, kwa kuwa anajua neno siri la anuani ya barua pepe ya mbunge huyo ambaye amekuwa anamtumia kama msaidizi wake katika masuala mengi walipokuwa CHADEMA.Bonyeza hapa kwa habari kamili.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

7 Responses to “KAFULILA ADAI ZITTO KABWE NI MZUSHI”

  1. Comment by mr degree on December 4th, 2009 3:09 pm

    mwenyekiti wa NCCR mageuzi James mbatia amesema ni kweli zito ametoa magari hayo kwa kafulila! sasa wanabisha nini chadema!CHADEMA lazima wakubali ukweli kwamba wanayumba! na wasitafute mchawi wachawi ni wao wenyewe.siasa zao za kibaguzi na kupendeleana zitawafanya wampoteze hata huyo ZITO! wajirekebishe haraka! sisi CCM tunataka kupambana na wapinzani wenye nguvu, tumechoka kushinda kwa kishindo!

  2. Comment by papai on December 5th, 2009 4:20 am

    jamani mimi naipenda chadema ila nahisi hawatafika mbali kwa sababu ya ubaguzi wao na utapeli wa baadhi ya viongozi wao kama zito. kama wanataka kura za watanzania watoe sera zao za umoshi moshi, kama hawatabadilika basi wategemee kura za moshi tu. hata kule tarime wasitegemee wataendelea kushinda kwa kishindo kwa sababu wale mura huwa wanageuka kama wanaona chama hakina tija, na wakigeuka huwa wamegeuka, hawarudi nyuma.

  3. Comment by hombiz on December 6th, 2009 12:41 am

    Hizo ndio si hasa za bongo. UFISADI tuuuu kila kona. 80% ya watanzania wanateseka kutokana na siasa hizi mbovu za BONGO!

  4. Comment by Ray Ephraim Ndewingiya Njau on December 7th, 2009 11:19 am

    Matatizo ya Bongo kila mtu anataka kuingia kwenye uga wa kisiasa na kusahau kuwa siasa ni taaluma.Kutokana na hali hiyo matatizo yanapojitokeza huko ndani ya vyama husika mchakato wa usuluhishi haufuatwi na sasa kinachofuata ni kuhama kwa lengo la kujiimarisha kisiasa.Wakati hayo yakiendelea ni vema wanasiasa wetu wajitahidi kuwa makini sasa wakati wanapoamua kuwasilisha ujumbe kwa jamii kwa kuwa wanasiasa wanathari kubwa za kimtazamo ndani ya jamii husika.
    Ujumbe:”SIASA SIYO UGA WA KILA MTU”

  5. Comment by Dan on December 7th, 2009 5:47 pm

    Bc washenzi wakubwa mnabania maoni! manataka maoni ya upande mmoja tu so sad!Haya kaeni na mtandao wenu!

  6. Comment by OSCAR NDOSI on December 8th, 2009 6:36 am

    ZITTO NI MZURI NA ANAWEZA KUSIMAMIMIA MISINGI YA KATIBA NA SHERIA NA BADO NI MPEVU KATIKA SIASA KWA HIYO ILI AWEZE KUTEKELEZA MAMBO YENYE KULETA TIJA KWA TAIFA NA MAENDELEO KWA UJUMLA LAZIMA ATAFUTE CHAMA MBADALA AMBACHO KITAMPA NAFASI NA CHAMA HICHO SI KINGINE BALI CCM.

  7. Comment by Elinihaki charles on December 21st, 2009 10:53 am

    chadema watulie wasiue imaniyao kwa wananchi ambayo walisha jiwekea.migogoro inatatuliwa kwa maongezi si kufukuzana.

Leave a Reply