
Tunapoelekea kuufunga mwaka 2009,yaelekea AY ameamua kwamba mwaka haushi bila kuonyesha kule anapojaribu kuelekea kisanii. Utakumbuka kwamba AY mwaka huu aliteuliwa kuwania tuzo za MTV Africa Music Awards na ndiye mwanamuziki ambaye amekuwa akipewa sifa na moyo zaidi kutoka kwa wasanii wengine wa kimataifa kama vile K9,Wyclef Jean,Akon na wengineo.
Safari hii anakuja na wimbo ambao ameuita Bed and Breakfast. Ni mchanganyiko kabambe wa Raga na Hip Hop. Wimbo umefanyika katika studio za B.Hitz Music Group chini ya Producer Hermy B huku mastering ikifanyika katika studio ya Ogopa Deejays ya nchini Kenya.
AY anasema video ya wimbo huu itafanyika mwezi huu ndani ya jiji la Johannesburg nchini South Africa chini ya kampuni ya Film Online ambayo ni miongoni mwa kampuni bora kabisa barani Africa katika utengenezaji wa videoz na mambo kama hayo.Miongoni mwa kazi walizowahi kuzifanya jamaa wa Film Online ni pamoja na Video Bora ya Mwaka ya MTV 2009 ya msanii S.A HHP.
Nilipoongea na AY hivi karibuni alinidokezea kwamba nia yake hivi sasa ni kuhakikisha kwamba Tanzania na wasanii wa kitanzania wanajikita na kuleta ushindani wa dhati katika soko la kimataifa la muziki na burudani kwa kwenda sambamba na wasanii wengine wanaofanya vizuri barani Africa kama vile kutoka nchi za South Africa,Nigeria etc.
Ukisikiliza wimbo wa Bed and Breakfast utagundua kwamba kuna kiitikio cha mwanadada fulani.Kwa bahati mbaya,mwanadada huyo hapendi kupewa credit zake kwa sababu zake binafsi.Kwa maana hiyo hatotajwa kwa sasa….labda baadaye. Pata burudani,sikiliza Bed and Breakfast.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Feedback / Comments
6 Responses to ““BED AND BREAKFAST”-AY”
Leave a Reply


nyimbo kali kaka
bt fupi sana
wkt wa2 wanataka radha zaid
Mmh been thinking hivi huyo gal sio huyu mrembo Jokate?heard kuna muda flani walitaka kufanya collabo flani so nadhani naguess right hapo,ila kuhusu nyimbo naona ya kawaida tu sio kwamba iko kali kivile!
AY hii nyimbo ni kali mhh,sikiliza kwenye stereo utajua huyu jamaa alikuwa studio.
Ni njema ni tamu. Bed&breakfast, isijekuwa issue Dar maana mhh…
Hiyo bed and breakfast karibu na mwisho wa nyimbo mbona ina-sound kama bread and breakses!
Nyimbo iko tamu sana hata sisi napenda sana hii, mimi itampa pesa huyo AY aimbie imbo ya Compaign hata Mwakyembe abroo kabisa.
Mimi iko penda sana hii kijana iko mpa pesa ya kagoda akafanye albam kule kwa obama.
Hii kitu imetulia. Keep it up!