KikweteJK

Kesho ni 9 Desemba.Bila shaka unaelewa umuhimu wa siku hiyo kwa nchi yetu.Kama historia ya nchi imekupitia kushoto,naomba nikukumbushe.Ni siku ya kukumbuka siku mkoloni alipoamua kukubali yaishe na kuirudisha nchi kwa wenye nchi yaani wananchi.Uhuru.

Sitaki kuhesabu ni miaka mingapi imepita tangu mwenge ule ulipopandishwa kileleni Kilimanjaro.Nina sababu zangu.

Wakati wa kumbukumbu kama hizi za Uhuru,kinachoendelea ni hotuba,ahadi za uongo na kweli na mambo kama hayo.Tunatakiana kheri pia.Kwa kipi?Sina uhakika.Hapo ndipo katika pitapita yangu mtandaoni,kwenye wavuti na blogs mbalimbali,nikakutana na ya Mubelwa akiwa pale Laurel,MD nchini Marekani.Yeye anasema,wakati anawatakia watanzania wote kila la kheri katika kusheherekea miaka— ya Uhuru,ana maswali 10 kwenda kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.Bonyeza hapa uyasome.

Mubelwa,sidhani kama atajibu.Hulka hiyo bado haipo.Ninachoweza kukuhakikishia ni kwamba atayasoma.Kama sio yeye basi “miongoni mwao”.

Feedback / Comments

5 Responses to “MASWALI 10 YA MUBELWA KWA JK”

  1. Comment by perfect stranger on December 8th, 2009 1:44 am

    na yeye mubelwa ameifanyia nini nchi hii toka amekuja hapa duniani? mchango wa kila mtu unahitajika katika kuendeleza nchi hii. watu wafanye kazi,watoe mawazo ya kujenga nchi n.k. sio kukosoa tuu kama nchi hii ameumbiwa kikwete peke yake. nchi yetu wote. sasa wee unauliza maswali tuu halafu unakaa kimya! hatuwezi kuendelea kamwe. tumekaa kukomoana komoana tuu. unafiki umetujaa!

  2. Comment by Gift Shine on December 8th, 2009 9:33 am

    Yes, as other Tanzanian I have to proud of being Tanzania simply because I like my country. Tomorrow we will have such a crucial moment in the history of our country.
    Hope every one as Tanzanian have to feel something very special,
    Much respect to our President, Hon. JK
    Tupo pamoja katika ujenzi wa Taifa letu.
    Gift Shine.

  3. Comment by kamanzi on December 8th, 2009 11:11 pm

    Wote nyie wawili ni wanafiki tu pamoja na huyo Bubelwa wenu. Hamuwezi kumwambia Bubelwa kaifanyia nini nchi wakati nchi inaendeshwa kifisadi. JF Kennedy aliweza kuwauliza hilo swali wamarekani kwasababu nchi ya marekani ilishaweka mazingira ambapo kila mmarekani angeweza kuendelea kama angekuwa ngangari na ndio maana kuna old adage inayosema “American dream”. Yani kwasababu ya mifumo mizuri ya kiuchumi marekani, kila mmarekani na hata immigrants wanaoenda huko wanaenda kutafuta hiyo ndoto ambayo ni mafanikio na baraka. Sasa Kikwete ameweka ndoto kwa watanzania? Amefanya nini katik miaka yake 4 ya utawala kwa ajili ya watanzania? Lipumba anamjibia kwamba tangu awe raisi amegeuka Vasco Da Gama mara leo anenda Jamaica kucheza reggae mara kesho anenda US kucheza hip hop na JZ and the list could go on. Kwaiyo wewe Gift na huyo perfect stranger acheni unafiki. nyie ndio mnaopiga kelele na kuandamana Maximo afukuzwe au Ridhia asiwe miss Tanzania wakati mafisadi kama akina Rostam hamuwaambii chochote wala kuwagomea. Wanafiki wahedi.

    Nikirudi kwako Bubwelwa. Wewe huna uwezo wa kusemea watanzania maana unaishi nje ya nchi. Hujui kuomba kazi na vigezo vyote halafu mtoto wa waziri mwenye digrii akapewa badala yako. Hujui kuomba scholarship halafu girlfriend wa waziri akapewa au mdogo wa girlfriend. Hujui kuomba mkopo ukanyimwa halafu akapewa mtu ambaye tayari anakesi ya EPA mahakamani. Hujui kufungwa bila kosa kama akina Babu Seya. hujui kuishi bila maji bombani na umeme wa mgao. Ningeweza kuendelea ila la msingi nakuonya, kama huishi Tanzania usijifanye waionea uchungu sana. Labda utueleze huwa unatuma shillingi ngapi kusaidia familia yako hapo tutakuelewa.

    Mungu ibariki Africa, Mungu ibariki Tanzania ila nawaombea kifo na magonjwa yasiyotibika wale wote wanaoinyonya nchi yangu nzuri.

  4. Comment by perfect stranger on December 11th, 2009 1:11 am

    kamanzi anasema!”Lipumba anamjibia kwamba tangu awe raisi amegeuka Vasco Da Gama mara leo anenda Jamaica kucheza reggae mara kesho anenda US kucheza hip hop na JZ and the list could go on. Kwaiyo wewe Gift na huyo perfect stranger acheni unafiki. nyie ndio mnaopiga kelele na kuandamana Maximo afukuzwe au Ridhia asiwe miss Tanzania wakati mafisadi kama akina Rostam hamuwaambii chochote wala kuwagomea. Wanafiki wahedi”. nafikirihujajibu swali nawe umeifanyia nini nchi hii? hizo hasira na chuki haziwezi kusaidia kitu! fanya kazi.pia unawaombea kifo na magonjwa yasiyotibika wale wote wanaoinyonya inchi! mi nakuombea wewe mtumwa ufe hata leo kwa akili yako hiyo huwezi kuissaidia nchi yetu. mungu ibariki tanzania na mlaani kamanzi! kwanza wee raia wa nchi hii au mkimbizi?

  5. Comment by kamanzi on December 13th, 2009 2:50 am

    Naam sasa nimefahamu wewe ni nani perfect stranger. Ungekuwa na integrity hata robo ungeweka jina lako la ukweli hapa jamvini. Unajua kwanini unaogopa kuweka? Ni kwasababu ninyi ndio kansa inayokula nchi yangu Tanzania. Anaongea mtunzi mmoja kuwa “mmeiba hadi vipofu wameona”. Laana isiyo sababu haimpati mtu ndugu yangu ndivyo Biblia inavyosema. Je unaamini Biblia au ufisadi umeshakutafuna mpaka unajiona Mungu?

    Wazazi wangu hawakunifundisha kutukana ndio maana siwei kukujibu kwa matusi. Ila nasema kwa kuinukuu Biblia tena kwamba “Mshahara wa dhambi ni MAUTI”. Sio mimi ni Biblia. Hakuna mwanzo usiokuwa na mwisho ndugu yangu. Alsema Adam Shafi katika kitabu chake cha KULI, “Yana mwisho haya”. Waliaibika akina Mobutu Seseseko, Imelda Malcos na Jean Bedel Bokasa iwe ninyi wanyonyaji wa Tanzania?

    Laana ya Mungu itakapoanza kukutafuna ndugu yangu perfect stranger pamoja na mafisadi wenzio wote kumbuka jina hili “KAMANZI”. Karibu kwetu Kigoma ndugu yangu. Karibu katika mji wenye lami yenye urefu wa kilometa 3 tu tangu uhuru na tena inamashimo. Itakuwa ajabu kwa mkimbizi kuwa na uchungu wa nchi kuliko wewe “mzawa” perfect stranger. Narudia kumbuka jina KAMANZI utakapioanza kulaanika maana naanza kukuombea laana kwa matusi yako. Mungu akubariki mpendwa!!!

Leave a Reply