ROGERS MTAGWA ULINGONI TENA MWEZI UJAO

Mtagwa

BONDIA Mtanzania anayeishi nchini Marekani Rogers Mtagwa anatarajia kupanda ulingoni Januari 23 mwakani kupambana na Yuriorkis Gamboa, pambano la raundi 12 litakalofanyika jijini New York.

Pambano hilo la ubingwa linalotambuliwa na HBO litakuwa la uzito wa Feather, ambako mabondia hao wanaendelea kujifua kwa ajili ya shughuli hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Marekani zinaleza kuwa Mtagwa ana rekodi ya kushiriki mapambano 26 na kushinda 13 kwa pointi, kupoteza mawili na kushinda kwa KO 18.

Mpinzani wake Gamboa amecheza mapambano 16 na kushinda kwa KO 14, mawili kwa pointi na hajapoteza hata pambano moja.

Aidha, mbali ya pambano hilo pia kutakuwa na pambano la uzito kama huo ambalo litamshirikisha Juan Manuel Lopez atakayezichapa na Steven Luevano.

Pambano jingine linalotarajiwa kufanyika siku hiyo jijini Pasay nchini Philippines, Donnie Nietes atazipiga na Ivan Meneses.

Source:Tanzania Daima

Page 1 of 3 | Next page