
Mcheza golf maarufu ulimwenguni,Tiger Woods,kutoka nchini Marekani, ametangaza kupitia mtandao wake kwamba anachukua likizo isiyo na muda maalumu kutoka katika mchezo huo ili kujaribu kurekebisha mambo yake.
Katika siku za hivi karibuni,habari za Tiger Woods kupitia vyombo mbalimbali vya habari,amekuwa akihusishwa na habari mbalimbali za “ukosefu wa uaminifu” kwa ndoa na mke wake kwa kuwa na vimada mbalimbali.
Mpaka hivi sasa wanawake 13 wameshajitokeza na kudai walikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Tiger Woods wakati tayari bingwa huyo wa golf duniani akiwa ni mwanandoa kwa mwanamitindo kutoka Sweden, Elin Nordegren.Wengi miongoni mwa wasichana hao wamekuwa wakijitokeza na ushahidi wa kueleweka zikiwemo text messages,voicemails ,e-mails na hata risiti za malipo.
Mapema hivi leo,ziliibuka habari kwamba Tiger Woods amewahi hata kujihusisha kimapenzi na malaya wa kulipia ambapo inasemekana alitumia zaidi ya dola $60,000 kwa huduma hizo.
“Baada ya kufanya tafakuri ya kina,nimeamua kuchukua mapumziko. Nahitaji kuelekeza nguvu zangu katika kuwa mume,baba na mtu bora zaidi” amesema Tiger Woods.

Tiger na mkewe, Elin walioana miaka mitano iliyopita na wana watoto wawili;wa kwanza wa kike ambaye ana umri wa miaka miwili na wa kiume ambaye ana miezi kumi.Kuna habari kwamba Tiger Woods na mkewe wameamua kwenda nchini Sweden ili kurekebishia mambo yao huko. Mkewe ameripotiwa kununua jumba lenye thamani ya dola milioni 2 huko Sweden ambalo wadaku wanadai huenda ndio ikawa nyumba yao ya kuishi kwa hivi sasa.
Habari kwamba huenda Elin akaomba talaka kutoka kwa Tiger zimekanushwa na marafiki wa karibu wa wanandoa hao.
Feedback / Comments
One Response to “TIGER WOODS AAMUA KUPUMZIKA KUCHEZA GOLF”
Leave a Reply


sending...
mwanaume mwenya mafanikio ya juu kama Tiger sio ajabu kupata ripoti kwamba hana uaminifu katika ndoa yake. Hata huyu Elin ninamlaumu kwani anafikiria tiger ni malaika? ama alifikiri macho ya tiger haiwaoni wanawake wengine? infact inawezekana kwa vile tunawajua hawa wasichana wa eva na tamaa kubwa ya senti walionayo. ukifilisika unatupwa pembeni wakiwafukuza wanaoendesha magari ya kifahari. halafu sasa imagine kwamba kijana tunayezungumza juu yake ni mweusi aliye na mtambo wa kumfanya mwanamke yeyote kupata full satisfaction kitandani, tena ongezea juu ya hiyo kwamba ana umashuhuri wa kuingiza mipira shimoni bila kuhata. mwanamke yupi mweusi ama mweupe atamtupilia mbali eti yeye tayari ashaoa na ana watoto, hakuna. itatambulika baadaye kwamba kuna wanawake wengine zaidi ambao hawajajitokeza ambao walishavua suruali ili kumpea ngono huyu kijana aliyebarikiwa na senti ambayo hata wazungu wenyewe hawapati.