DJ mkongwe na maarufu nchini Tanzania,DJ Young Kim, amefariki dunia. Kwa mujibu wa blog ya Issa Michuzi, DJ Kim amefariki dunia akiwa katika hospitali moja ya binafsi inayojishughulisha zaidi na tiba za magonjwa ya moyo iliyopo Manzese jijini Dar-es-salaam.
DJ Young Kim ni miongoni mwa DJs waliochangia sana maendeleo ya disco na mashindano ya kucheza muziki(disco) ambapo ndipo yalipoibuka majina maarufu katika muziki kama vile Black Moses(RIP),Ommy Sidney,Othman DigaDiga na wengine wengi.
Pia kwa wale ambao wanafuatilia chimbuko la muziki ambao leo hii tunauita wa kizazi kipya,mchango wa DJ Kim kupitia mashindano ya Yo Rap Bonanza ,ulikuwa ni chachu muhimu katika mwanzo au mwendelezo wa muziki wa hip hop nchini Tanzania.Pumzika kwa amani DJ Young Kim.
Feedback / Comments
7 Responses to “DJ YOUNG KIM AMEFARIKI!”
Leave a Reply


sending...
hakika sisi ni wa mwenyezi mungu na hakika kwa mwenyezi mungu sote tutarejea. mwenyezi mungu ailaze roho ya marehem mahali pema peponi.mungu awape uvumilivu mke,mama wa marehem na watoto wake aamin.
RIP brother,najua ulikuwa unafurahia maendeleo ya vijana katika sanaa,lakini bwana ametwaa,sisi ni nani tumbishuie?
Pole sana Mariam mungu akupe nguvu wewe na wanao.
rest in peace
joachim aka dj young kim
Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi tutakukumbuka sana Dj Young Kim.Amen.
Nakuombea kwa Mwenyezi Mungu shemeji yangu roho yako aiweke mahali pema peponi.Na akupunguzie adhabu ya kaburi.Ni njia yetu sote hiyo.
Brother Mungu akulaze mahali peponi akuondoleye hazabu za kaburi na sisi piya vijana wa Bujumbura tunawapa pole familiya ya marehemu na wazazi wake sote niko turejeyapo na piya Kazi yake Mungu haina makosa amin.