MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

AJ UBAO 2Kwa jina anaitwa Athuman Juma Ubao au AJ Ubao au Father D, alizaliwa katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar-es-salaam,Tanzania.Nni mtoto wa pili katika familia ya Mzee Juma Ubao a.k.a King Makusa.

AJ anasema ametokea kwenye ukoo wa muziki kuanzia kwa babu yake hadi baba mzazi ambaye ni mkongwe wa muziki Tanzania na enzi zake alikuwa akienda kurekodi miziki Nairobi- Kenya akiwa na bendi yake, Six Manyara, kwani wakati huo hakukuwa na studio pale nyumbani Tanzania.

Lakini hivi sasa Mzee Ubao ameanzisha kundi liitwalo Wanne Cultural Group akiendeleza libeneke katika utamaduni wa Mtanzania.

Kwahiyo alianza muziki miaka mitano iliyopita akiwa katika kikundi kiitwacho “The Swahili” akiwa na mwenzake Herry Omary a.k.a Dirty Herry hapa Washington Dc. Anaendelea kusema “tulitoa albam moja ambayo haikupata mafanikio makubwa”.

Hapo basi ndipo alipoamua kubadili mwelekeo wake wa muziki kama mwimbaji na Rapper kwasababu anasema amejifunza kwamba siku hizi muziki wa R&B unategemea hiphop na hiphop nayo inategemea R&B kwahiyo unaweza ukavuta watu wote wa makundi hayo mawili kupenda muziki wako bila wasiwasi.

Hivi sasa nimeamua kuimba mwenyewe yaani “Solo” na kazi yangu ya kwanza inaitwa Haya ni Maisha Yangu (This is my Life) na sababu ya kuipa jina hili anasema ni kwamba anaongelea juu ya maisha yake na mambo magumu aliyopitia.

Albam hii itakuwa ni katika miondoko ya R&B na HipHop na imetengenezwa na prodyuza Akili Msola a.k.a Mtaalam anasema “tunategemea itakamilika mwanzoni mwa mwaka ujao. Na itakuwa na nyimbo maarufu kama Adabu Tupu, Macho, Feel The Music, Haya ni maisha yangu na nyingine nyingi itakuwa ni moto mtupu anaongeza AJ.

“Nataka muziki wangu uwe wa starehe na pia kuelimisha jamii na ndio maaana naimba kwa lugha mbili kiingereza na Kiswahili na pia ndoto yangu ni kuwa mmoja wa wasanii bora kutoka Daressalaam Tanzania anasema AJ kwa utulivu mkubwa.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video


Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

3 Responses to “INTRODUCING AJ UBAO”

  1. Comment by Kigina khamis on December 21st, 2009 8:39 pm

    hope u all fine

  2. Comment by Gally Zouler on December 22nd, 2009 11:15 am

    Pheeew! Pheeew! Phew ! wazo zima ni zuri -yaani kuimba both kiingereza na kiswahili .si haba umejitahidi.
    Ushauri: siku nyingine au ktk jaribio lingine tafuta mtu akusaidie siyo kubadilisha mashairi yako ya kiingereza lah! bali akusaidie uweze kuimba kiingereza kwa kiingereza na siyo kiingereza kwa kiswahili.Labda itapendeza mara mbili ya hapa ilivyopendeza.Ni jaribio zuri lakini
    NB. Usinelewe vibaya kuhusu ushauri wangu.Sina maana kwamba uimbe kama mzungu au lafudhi ya kizungu
    Gally Zouler

  3. Comment by Sakina Abdul on December 31st, 2009 3:16 pm

    Aj jitaidi uimbe siyo hook inakua the all song usinielewe vibaya ni kwa ushauri tu isitoshe umetokea kwenye family ya muziki

Leave a Reply