123Kawawa

Mzee Rashid Mfaume Kawawa,amefariki! Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari zikiwemo blogs,Mzee Kawawa amefikwa na mauti katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili ambako alikuwa amelazwa.

Rashid Mfaume Kawawa alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza nchini Tanzania na baadaye kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi.Alizaliwa mwaka 1926 katika kijiji cha Matepwende Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Tanzania. Alianza elimu ya Msingi huko Liwale -Lindi mnamo 19411942 na kuendelea na masomo ya sekondari katika shule ya Dar es Salaam Secondary School.

Ni hivi karibuni tu Mzee Kawawa alizindua kitabu kinachoelezea maisha yake.

Kawawa12

Majuzi Rais Kikwete na mkewe Salma Kikwete,walikwenda Muhimbili kumuona Mzee Kawawa.Laiti wangelijua kwamba hawatomuona tena Mzee Kawawa akiwa hai!

Kwa mujibu wa ratiba ya mazishi ambayo imetolewa,Mzee Rashid Mfaume Kawawa anatarajia kuzikwa Jumamosi nyumbani kwake Madale nje kidogo ya jiji la Dar-es-salaam.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Mwili wa marehemu Mzee Rashid Mfaume Kawawa ukitolewa katika hospitali ya rufaa ya Muhimbili kwenda kuhifadhiwa katika hospitali ya jeshi ya Lugalo.Anayesikika akilia kwa uchungu ni mkewe Asina Kawawa.

KawawaEnzi

Rashid Mfaume Kawawa enzi za ujana wake.

KawawaMuungano

Utumishi wa Mzee Rashid Mfaume Kawawa kwa taifa letu ni wa siku nyingi.Pichani kulia anaonekana akishuhudia Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akichanganya michanga ya ardhi ya Tanganyika na Zanzibar kuashiria Muungano.Hiyo ilikuwa ni mwaka 1964

Feedback / Comments

Leave a Reply