Mashabiki wa muziki,hususani wa R&B waliopo katika ukanda wa Afrika Mashariki na hususani jijini Kampala nchini Uganda,huenda kesho wakashuhudia onyesho ambalo hawajashuhudia ndani ya miaka kadhaa na huenda wasishuhudie katika miaka kadhaa ijayo.Hiyo ni ahadi,sio kutoka kwangu bali kutoka kwa mwanamuziki Robert Sylvester Kelly maarufu kama R.Kelly(pichani) kutoka nchini Marekani anayetarajiwa kufanya onyesho la aina yake hapo kesho jijini Kampala katika ukumbi wa Lugogo Cricket Oval.

Onyesho hilo ambalo limedhaminiwa na kampuni ya simu ya Zain,limepewa jina la “I Believe”.Hivi karibuni iliarifiwa kwamba kampuni ya Zain imetumbukiza zaidi ya $2.5 kwa ajili ya onyesho hilo kwani inasemekana kwamba kwa R.Kelly kukubali kufanya show yoyote nje ya Amerika Kaskazini basi $600,000 lazima ziwe mezani. Viingilio katika onyesho hilo ambalo tiketi zake zilishakwisha(sold out) wiki mbili zilizopita, vimepangwa kuwa Ushs 30,000(Silver) Ushs 125,000(Gold) na Ushs 250,000(Platinum). Hii ni mara ya kwanza kwa R.Kelly kufanya concert katika ukanda wa Afrika Mashariki. Na barani Afrika kwa ujumla mahali pengine ambapo amewahi kufanya onyesho ni Afrika Kusini tu.

R.Kelly ameahidi kuimba nyimbo zake zote ambazo amewahi kutamba nazo kama vile Bump n’Grind, I Believe I Can Fly,Gotham City,Ignition(Remix),The World’s Greatest,If I could turn back the hands of time, na nyinginezo tele bila kusahau hip-hopera yake ya Trapped In A Closet.

Sasa kwa wale ambao mmeshawahi kuhudhuria show yeyote ya R.Kelly,mnajua kwamba yeye hupenda mashabiki wanaokwenda naye sambamba.Hupenda kuwashirikisha hadhira(audience).Kazi kwenu.Jukwaani R.Kelly anatarajia kusindikizwa na wasanii wa Uganda Bebe Cool,Jose Chameleon,GNL,Peter Miles na Goodlyf ambao ni Radio na Weasel.Wote hao wamepigiwa kura na waganda wenyewe ili kupata nafasi hiyo.

Here is one my favourite from him; Step In The Name Of Love.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Habari kubwa iliyopo kurasa za mbele za vyombo vya habari ulimwenguni hivi leo ni kuhusu hotuba ya Rais wa Marekani,Barack Obama hapo jana usiku.Wenyewe wanaiita State Of The Union. Kama hukuiona,unaweza kuitazama hotuba nzima katika video hiyo hapo chini.

Kwa mtazamo wangu  hotuba hii ni nzuri na  ambayo viongozi mbalimbali duniani(hata katika nchi zetu za Afrika) wanaweza pia kuitumia kama kioo katika uongozi wao.Kuna mahali Obama alisema ukishachaguliwa kuwa kiongozi basi ufanye kweli kazi ya kuongoza(leadership) na kutengeneza kesho ya kizazi kijacho(next generation) na sio tu kwa sababu unataka kushinda uchaguzi ujao(next election). Alitia pia msisitizo wa kukumbuka kwamba upo hapo ulipo kwa sababu waliokutangulia,waliandaa mazingira mazuri kwa ajili yako.Bravo Obama!

Anaitwa Irene Sporah Njau, ni mtangazaji wa Kipindi cha Sporah Show ambacho kinazidi kujipatia umaarufu na mashabiki.Lakini Sporah ni nani,ametokea wapi,ana malengo gani na ni kwanini anafanya anachokifanya? Ili kupata majibu ya maswali hayo na mengineyo bonyeza hapa kutembelea Spoti Starehe ili kucheki mahojiano kamili.

Nimekuwa katika vuguvugu la habari na mawasiliano kwa njia ya blog kwa muda sasa.Kila siku huwa napitia blogs zaidi ya 500! Huwa natumia huduma ya www.bloglines.com. Ukiandika kitu basi naambiwa umeandika na hivyo napita na kusoma.Ukiwa hujaandika,basi siku hiyo napata muda wa kuperuzi au kutafuta blogs zingine,kuziingiza kwenye orodha yangu ya bloglines.Siku inakuwa imekwenda au naendelea na kazi zingine.

Leo nikiwa katika pitia pitia yangu mtandaoni,nimekutana na blog ya Madaraka Nyerere,mtoto wa Hayati Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Cha kwanza kilichonijia kichwani ni hasira fulani.Iweje siku zote hizi sikujua kuhusu blog ya Madaraka? Haikutangazwa au ilikuwaje? Hasira zangu ziliyeyuka kama vile barafu inapopigwa na jua baada ya kuanza kuipitia blog yake.Imesheheni habari kemkem.Madaraka ni mwandishi mzuri.Simulizi zake ni nyepesi kama pamba lakini maudhui yake ni mazito kuliko yale mawe yanaouzunguka mji wa Mwanza.

Bonyeza hapa ili kuitembelea blog hiyo. Nikisema mkaribishe nitakuwa nakosea kwani amekuwepo kwa muda sasa.Bravo Madaraka.

Pichani juu ni Madaraka Nyerere(kulia) akiwa na Jaffar Amin,mtoto wa Iddi Amini aliyewahi kuwa Rais wa Uganda. Soma zaidi kuhusu mkutano wao.

Mabingwa wa Ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani(mara nyingi hujiita World Champions) kwa mwaka wa 2009,L.A.Lakers,jana walitembelea White House.

Pichani ni manahodha wa L.A.Lakers,Kobe Bryant na Derick Fisher(mbele karibu na Rais Barack Obama) wakimkabidhi jezi na mpira. Rais Obama sio tu ni mpenzi mkubwa wa mpira wa kikapu bali ni mchezaji mzuri wa mchezo huo.Are you an L.A.Lakers fan?

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Nina imani kwamba hujawasahau Wagosi wa Kaya.Naam ni wale wale vijana kutoka Tanga ambao miaka ileee waliingia kwenye anga za muziki kwa kishindo  pale walipohoji “Tanga Kunani Pale”?

Tangu pale Wagosi wa Kaya wakawa wamejikita katika ile aina ya muziki wa kizazi kipya ambao mimi hupenda kuuita “conscious” kwa maana ya kwamba unalenga kwa undani kile kinachoendelea katika jamii.Ukipenda uite “muziki tambuzi”.

Baada ya kuwa kimya kwa miaka kadhaa(hata wao wanakiri katika wimbo huu kwamba walikuwa kimya kwa muda mrefu) wamerudi.Na mara hii wamerudi wakiwa na timing ya aina yake.Wanagusia uchaguzi,siasa na mambo kama hayo. Kama unavyojua,mwaka huu,watanzania watajipanga foleni ili kuchagua tena viongozi.Demokrasia.Wao wanasema ni Maumivu ya Miaka 10!

Wasikilize Wagosi wa Kaya kwa kubonyeza player hapo chini.Sikiliza kwa makini ujumbe kwani kwa maoni yangu,kidogo sauti ya beats ni ya juu kuliko za wanaoghani.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Picha kwa hisani ya outhere.de.

Natumaini kwamba hujambo na unaendelea na mapambano ya maisha kwa ujasiri,bila woga wala dalili za kukata tama.Hivyo ndivyo inavyotakiwa.Kumbuka kwamba penye nia pana njia.Jifunze jambo jipya kila siku.Usipoteze muda bure.

Uchumi wa dunia bado haujatengemaa.Bado habari za makampuni kufungwa,kupunguza wafanyakazi,kufilisika na mambo kama hayo,tunazisikia na tutaendelea kuzisikia.Hatujui lini uchumi utarudia hali yake ya kawaida au tuseme ilivyokuwa miaka kadhaa iliyopita.Hakuna anayejua kwa hakika.Hata Rais Obama hajui. Kilichobakia hivi sasa ni imani tu kwamba huenda kesho ikawa bora kuliko jana.Imani.

Kwa sababu ya kuyumba huko kwa uchumi,wengi wameshapoteza kazi zao na wengi zaidi wapo mbioni kupoteza.Lakini kupoteza kazi sio mwisho wa maisha.Kwa ufupi ukipoteza kazi uliyonayo hivi leo,huo ni mwanzo wa mbio za kutafuta kazi nyingine.

Kwa maana hiyo wengi wanaopoteza,kuachishwa au kuanza kutafuta kazi hivi leo,wanahitaji mbinu za kushinda mtihani wa usaili(interview). Leo nitaongelea jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya usaili,jinsi ya kujiongoza wakati wa usaili nk.

Kabla sijakuambia ninachotaka kukuambia,naomba nikwambie jambo moja la msingi.Ushindi katika jambo lolote hutokana na jinsi unavyojiamini.Kujiamini hata wakati wa usaili ni jambo la msingi na ambalo lazima ulizingatie.Lakini kumbuka kujiamini hakumaanishi kiburi,majivuno au maringo.Ninaposema kujiamini ninamaanisha kuwa na uhakika na unachokisema na kuonyesha kwamba una uhakika bila majigambo wala kiburi.

Umepata barua au simu kuhusu usaili.Zingatia yafuatayo;

  • Hakikisha umepata taarifa za kutosha: Mara nyingi upatapo barua au simu inayokuita kwenye usaili,mtu yeyote hujawa na furaha au msisimko wa ajabu.Ni ruksa kufurahi lakini kumbuka kuchukua taarifa muhimu(hususani kama habari hii inakujia kwa njia ya simu) kuhusu mahali utakapofanyiwa usaili(anuani,namba ya chumba,gorofa ya ngapi nk),muda na kama usaili huo utakuwa na watu zaidi ya mmoja au la.Taarifa kama hizo zitakusaidia katika kujiandaa.
  • Fanya uchunguzi kuhusu shirika/kampuni husika: Kabla ya kwenda kwenye usaili hakikisha kwamba umefanya uchunguzi wa kutosha kuhusu kampuni au shirika husika(research).Wanashughulika na nini,wateja wao ni kina nani,linamilikiwa na nani,lilianzishwa lini na kwa malengo gani.

    Kama unamjua mtu au rafiki ambaye aliwahi kufanya kazi katika shirika au kampuni hiyo,mtumie ili kupata taarifa za ndani zaidi.Ufahamu wako kuhusu kampuni au shirika utawaonyesha wanaokufanyia usaili shauku uliyonayo kuhusu kampuni/shirika. Kumbuka tu kutojifanya unajua kupita kiasi.Bakia kwenye kiwango kinachostahili. read more

Binti au mrembo unayemuona pichani anaitwa Lilian Mduda(21). Huyu ndiye mwakilishi wetu katika fainali za shindano la kumsaka Kisura wa Afrika kupitia Mnet(Mnet Face of Africa) zinatarajiwa kufanyikia jijini Lagos nchini Nigeria tarehe 6 Februari/2010. Jumla ya warembo 10 kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika ndio waliofanikiwa kuingia katika fainali hizo na kwa maana hiyo ndio wataochuana.

Warembo wengine waliofanikiwa kufikia fainali wanatoka katika nchi za Angola,Ethiopia,Ghana,Kenya,Mozambique,Nigeria,South Africa,Zambia na Zimbabwe.

Lilian Mduda ambaye ni mwanfunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam akisomea Biashara(B.Comm), amesema amejiandaa vyema kwa ajili ya shindano hilo na haoni mshiriki yeyote anayemtisha isipokuwa ni yeye mwenyewe anayeweza kujiwekea mazingira ya kushinda kwa kuzingatia yale yote atakayoelekezwa na kuyafanya kwa ufanisi ili aweze kufikia malengo yake katika fainali hizo.

Lilian anapenda kusoma novels zenye hadithi za kimapenzi na chakula akipendacho ni wali na maharage.Ndoto zake ni pamoja na kuweza kutembelea jiji la Paris siku moja.Pia anapenda mpira wa kikapu(basketball) na hupenda kusikiliza mziki na kujisomea.Kila la kheri Lilian.

Ukitaka kujua zaidi kuhusu Mnet Face of Africa na warembo wengine wanaoshiriki,bonyeza hapa.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Movie inaitwa Legion. Mungu amekosa imani na wanadamu.Anatuma malaika kuja kuiangamiza dunia. Starring Paul Bettany, Dennis Quaid,Lucas Black,Tyrese Gibson etc.Imeongozwa na Scott Stewart

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Movie inaitwa Extraordinary Measures: Ni kisa cha kweli kinachowahusu wazazi John na Ailleen Crowley ambao wanajitolea kudhamini utatutwaji wa tiba kwa ugonjwa wa nadra ambao unawateketeza watoto wao wawili.Movie nzuri sana hii kwa wazazi.Starring Harrison Ford,Brendan Fraser, Courtney B.Vance nk.Imeongozwa na Tom Vaughan

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page