SAJNA-PIC-4BC

Mojawapo ya mambo ambayo huwa nayapenda katika uendeshaji mzima wa BC ni pamoja na kumtambulisha msanii mpya,nyimbo mpya,makundi ya wasanii nk.Binafsi naamini sana katika sanaa kama njia mojawapo muafaka kabisa katika kufikisha ujumbe kwa jamii na hivyo kuwa chachu katika kuleta maendeleo ya kijamii,kisiasa na hata kiuchumi.

Tizama kwa mfano elimu inayotolewa kwa njia ya maigizo,nyimbo au enzi zile kupitia ngonjera(nasikia siku hizi ngonjera hakuna tena mashuleni,ni ushamba eti!).Mpaka leo nikikumbuka kisa cha sungura kukatazwa kutumia maji ya kisimani,nakumbuka kuhusu wajibu wa kuwajibika na kushirikiana!Si unakumbuka enzi za kina Mahoka?Naam hiyo ndio kazi ya sanaa.

Lakini pamoja na kuwa kioo cha jamii,sio mara nyingi ukakuta msanii akifanya kazi zake kutokana na matukio ya kweli katika maisha yake na akawa wazi kwamba anachokifanya kinatokana na uzoefu binafsi wa maisha yake.Wengi tumeumbwa ili kuwanyooshea tu vidole wenzetu.Yule kafanya vile,huyu kasema vile na mambo kama hayo.

Msanii mpya kutoka jijini Mwanza anayekwenda kwa jina la Sajna(pichani)yeye ni miongoni mwa wachache.Anakuja kwa kishindo na kisa cha kweli. Sajna ambaye ana umri wa miaka 18 tu huku bado akiwa shuleni(form II),amekuja na wimbo unaoitwa NADHIFA. Wimbo huu ni true story ambayo imemtokea yeye mwenyewe. Kila alichokiimba katika wimbo huu ni cha kweli na kinamhusu yeye na familia yake. Kwa ufupi amemuimba dada yake wa damu ambaye alitoweka nyumbani kwao bila taarifa miaka kadhaa iliyopita.Wimbo umetengenezwa na producer Sam Timber.Msikilize na mkaribishe Sajna.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.



Feedback / Comments

One Response to “INTRODUCING SAJNA;WIMBO WAKE NI KISA CHA KWELI!”

  1. Comment by E.R.K on February 2nd, 2010 4:31 am

    BIG UP MTU WANGU HOW ABOUT MWANZA
    KIFUPI MWANA SIJUI MAENDELEO YAKO
    KWA SASA ILA SINGLE YAKO IKO BOMBA
    SANA SAJNA NGOMA IMETULIA FANYA
    MPANGO UPATE MZAMINI KAZI UNAWEZA
    UNAUWEZO WA KUFANYA VIKALI ZAIDI
    TATIZO SAPORT WISH U ALL THE BEST

Leave a Reply