
Nchini Marekani leo ni People’s Choice Awards. Sasa kwa wale wadau wa masuala ya fashion,urembo,vivazi nk, naambiwa kinachowavutia zaidi ni Red Carpet. Pale ndipo utaona nani kavaa nini,imetengenezwa na nani nk.Kumbuka tu kwamba wavaaji wale ambao ni celebrities,huwa wamepewa nguo,hereni,viatu vile nk kwa minajili ya kuzinadi.
Bonyeza hapa ili kuangalia mambo yalivyokwenda kwenye Red Carpet.
Nilichokipenda zaidi katika awards za mwaka huu ni kwamba kwa mara ya kwanza People’s Choice Awards zinachangia mradi wa Maji Safi kwa ajili ya watoto.Kwa kiingereza mradi huo unaitwa Children Safe Drinking Water. Celebrities wanapanda Mlima Kilimanjaro(nakumbusha Mlima upo Tanzania!) kwa ajili ya kuchangisha fedha. Tizama zaidi kuhusu mradi huu kutoka kwenye tovuti maalumu ya mradi huo.
Pichani juu ni Queen Latifah ambaye ndiye alikuwa Host kwa mwaka huu. As usual,I think she did a good job!
Feedback / Comments
One Response to “PEOPLE’S CHOICE AWARDS:RED CARPET +CLEAN WATER”
Leave a Reply


Queen Latifa namkubali sana, lakini wewe mleta mada unapotuletea mada za “michosho” za aina ya kusaidiwa au kuletewa misaada Tanzania. Hapo ndipo tunakuwa wazito na “vilema” wa kuchangia mada yako.
Tanzania ya leo sio ya kulialia na kutafuta misaada na kuchangiwa michango kama vile, michango ya vilio au harusi, heri michango ya harusi.
Maana katika michango ya harusi kuna minuso ya nguvu na wakati mwingine, kwa bahati ya “mtende” unaweza kukutana hata na watu mashuhuri kama vile akina anko “Michuzi” wakisaka nwuzi za blogi zao, na ukafotoa foto nao.
Lakini misaada misaada kwa Tanzania, mmmmhhh hapana kaka, hatujasikia Marekani ikichangiwa misaada, baada ya kushindwa vita vyake huko Iraq au Afganistani.
Usisahau kutuwekea miziki ya Queen Latifa wikiendi hii.
This Is Black=Blackmannen