KanumbaFrontKatika siku kama ya leo,miaka 26 iliyopita pale mkoani Shinyanga, alizaliwa kijana na kupewa jina la Steven. Hivi leo ni maarufu kama Steven Kanumba au kama mwenyewe anavyojiita wakati mwingine “The Great”. Kwa maana hiyo,leo ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Steven Charles Kanumba.Happy Birthday!

Kwa mtu yeyote ambaye anafuatilia maendeleo ya tasnia ya filamu nchini Tanzania,bila shaka atakubaliana na mimi nikisema kwamba Kanumba ni miongoni mwa waigizaji wa filamu(Film Actors) ambao ni maarufu zaidi nchini Tanzania. Leo hii ni vigumu kuiongelea sanaa ya filamu nchini bila kumhusisha Kanumba kwa njia moja ama nyingine.

Kwa hivyo,haishangazi sana kuona kwamba,katika mwaka uliopita jina lake lilikuwa takribani la kudumu katika vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo vya mtandaoni,mitaani nk. Bila shaka unakumbuka jinsi habari ya Kiingereza Vs Kiswahili ilivyozua mjadala wa kitaifa. Kila mtu akasema lake.

Baada ya mambo kama yale,mijadala kama ile,watu hupenda kujua what next? Nilimtafuta Steven Kanumba ili kujua machache kuhusu mipango yake ya mwaka huu.

Unajua Kanumba angependa kupata chakula cha mchana (lunch) na actors gani maarufu hapa ulimwenguni? Una habari kwamba katika Curriculum Vitae(CV) yake ameongeza cheo cha “Blogger”? Unajua ana malengo gani mwaka huu? Una habari kwamba Kanumba hivi sasa amedhamiria kuibua vipaji vingine katika ulimwengu wa uigizaji filamu? Fuatana nami;

BC: Mpaka sasa unalionaje soko la filamu nchini Tanzania? Kumekuwa na mabadiliko gani ya kimsingi ukilinganisha toka ulipoanza mpaka hivi leo?

SK: Soko limetanuka kiasi kwamba tunatambulika kimataifa. Pia hivi sasa makampuni ya kusambaza kazi zetu yameongezea ikiwemo na pesa kwa kiasi fulani tofauti na hapo mwanzo.Safari bado ni ndefu lakini angalau inatia moyo.

BC: Mwaka 2009 ndio tumeumaliza.Jina lako liligonga vyombo vya habari kwa mambo kadha wa kadha.Unaweza kusema umejifunza mambo gani katika mwaka ulioisha?

SK: Nimejifunza mengi lakini zaidi nimejua zaidi juu ya thamani kama msanii.

Kanumba na Richard

Kanumba(kulia) akiwa na Richard(Big Brother).Wote wameshiriki katika filamu za nchini Nigeria maarufu kama Nollywood.

BC: Nini mipango yako au kama wasemavyo katika kiingereza ‘your resolutions” kwa mwaka huu wa 2010?

SK: Mwaka huu kwangu sitoongea kitu zaidi ya kazi na nimeshaanza. Vitendo vitatawala zaidi.

BC: Nimesikia kwamba umefungua kampuni ya kusaka vipaji vya waigizaji.Unaweza kuniambia kidogo kuhusu kampuni hiyo na jinsi ambavyo vijana wanaweza kuwasiliana nawe kwa minajili hiyo?

SK: Kampuni inaitwa KATI CLASSIC lengo ni kusaidia wasanii ambao hawajawahi kuigiza kabisa katika TV lakini wana vipaji. Vijana ambao hawajui waanzie wapi.Zoezi la kusaka vipaji hivyo limeshaanza na interview zinafanyikia pale Lamada Hotel kila Jumapili.Wanakaribishwa.

Lovely Gamble

BC: Kama ungepewa nafasi ya kupata chakula cha jioni na actors watatu hapa duniani(waliopo hai) ungewachagua kina nani? Kwanini?

SK: Denzel Washington,Leonard DiCaprio na Ashwarai wa Bollywood..napenda kazi zao na ni watu ambao wameshika chart kwa mda mrefu jambo ambalo ni gumu sana kwa ma staa wengi hasa hapa TZ.

BC: Asante kaka.Kila la kheri katika kazi zako.

SK: Shukrani Jeff.Kazi njema na wewe pia.

Note: Ukitaka kuona Steve Kanumba anafanyaje katika ulimwengu wa blog,bonyeza hapa kumtembelea.

Feedback / Comments

42 Responses to ““MWAKA HUU SITOSEMA KITU,NI KAZI TU”-STEVEN KANUMBA”

  1. Comment by Nurdin Nuha Karamagi on January 8th, 2010 4:02 am

    nakutakia kila la kheri na mungu atkua nawe na kzi zako zitakua bab’kubwa kanumaba a.k.a the great

  2. Comment by jojo on January 8th, 2010 5:07 am

    kazi nzuri lakini ukitaka utambulike kimataifa lazima ujue ku communicate kimataifa

  3. Comment by yusam on January 8th, 2010 8:57 am

    unatisha mkubwa

  4. Comment by yusam on January 8th, 2010 9:02 am

    kaka wewe ni funika bovu umewafunika wote kwenye medani ya filamu yaaaaani we acha tu rayakupati kabisaaaaaaaaaaaaaaaa kwer wewe the great big up mkubwa

  5. Comment by lisa on January 8th, 2010 12:51 pm

    AANDAENI BASI MOVE ITAKAYOITWA BONGOWOOD AU DARLYWOOD

  6. Comment by Mickey Jones Amos on January 8th, 2010 1:49 pm

    “HAPPY BIRTHDAY STEVE KANUMBA”

    Mwenzetu ana kipaji cha kuzaliwa na kila akifanyacho katika kazi zake huleta matokeo mazuri ambayo ni maendeleo ya kuigwa na kizazi kijacho,lakini kama kawaida yetu watanzania huwa hatuna uwazi wa kumsifu mtu anayejaribu kuvuka mipaka kuitangaza nchi yetu badala yake huwa tunatafuta njia za maovu ya kashfa ambayo mara nyingi huwa ni njia fupi zinazoishia ukingoni.

    Hakuna umuhimu wa mawasiliano ya kimataifa au kiingereza cha hali ya juu kutambulika kimataifa,kuna waigizaji wengi ulimwenguni wapo “Hollywood”hata”Bollywood”
    wametambulika bila ya mawasiliano ya kimataifa au kiingereza cha hali ya juu.

    Kanumba alituwakilisha kwa juhudi zake zote kiingereza chake ni sawa na watanzania wengi,labda hawana njia ya kujitokeza kama alivyobahatika kujitokeza yeye,muhimu kazi yake inaonekana na inapendwa na wengi,
    juhudi zake kazini zinastahiri sifa zote kama muigizaji maarufu nchini.

    Nakutakia kila la kheri steve Kanumba
    Denmark

  7. Comment by radjabu mwinyi on January 8th, 2010 5:51 pm

    HAPPY BIRTHDAY STEVE KANUMBA
    MUNGU AKUJALI AKUPE MAISHA MAREFU

  8. Comment by Freddy Macha on January 8th, 2010 6:48 pm

    Ulilosema mdau wa Denmark muhimu kuhusu kupeana moyo Wabongo.
    Kusifiana ni muhimu sana hasa kwetu wa nchi changa zinazotambaa. Ndiyo maana wenzetu Wahindi, Wanaijeria, Wamexico na Wabrazili sasa hivi wanaongoza dimba la sinema mpya (“World Cinema”) duniani.
    Hawa wenzetu husaidiana, hushirikiana, huungana na kuserereka pamoja. Tunayo desturi ya kutabasamu tukiona jicho la mwenzetu lina tongo; lakini akiwa anamumunya lawalawa; akijitahidi kurusha tiara, tunamtemea makohozi.
    Zidumu jitihada za maendeleo ya wasanii na Wanabongo wote!
    Happy Birthday, Stephen Kanumba.

  9. Comment by Kadoggo on January 9th, 2010 12:03 am

    Happy Birthday kaka Kanumba, kwa kweli tunakufagilia sana Mtanzania mwenzetu kwa bidii zako katika filamu zako zote kwa kweli ni nzuri, wakati mwingine nikizitizama nadhani kama vile ni kweli kumbe ni hadithi tu, kweli kaka uko juu. Mungu akuzidishie uwezo zaidi na zaidi.
    HONGERA STEVE KANUMBA.

    USA

  10. Comment by meshack simon on January 9th, 2010 1:45 am

    Siku zote mti mzuri ndio unaopigwa mawe kaka,so kaza buti.Tupo watu ambao tuna kuunga mkono kwa kununua kazi zako na kwa maombi pia,mimi nakuombea mafanikio makubwa zaidi Mungu akutangulie.

    Masasi-mtwara

  11. Comment by Annie Steve on January 9th, 2010 2:07 am

    Hey! Steve,
    Waseme wanavyosema, wachonge wanavyochonga ukweli unabaki pale pale kuwa wewe ni “SUPER STAR WA TZ. Waect filam bila wewe haitamaniki kuangalia, ukiwemo kwenye filam fulani mtu anatamani airudie kuiangalia tu bila kuchoka, Good, U a SUPER STAR, watu wanakukubali wanaochonga wivu wao tu. Ushauri: Wanavyozidi kuchonga na wewe kaza buti kusaka ufanisi bora zaidi.

  12. Comment by Joy maeda on January 9th, 2010 3:33 am

    HAPPY BIRTHDAY STEVE KANUMBA. MAY GOD BLESS U IN ALL UR PLANNING FOR THIS YEAR 2010.UR SO CREATIVE AND I CONGATULATE U FOR THAT.AS A TANZANIAN I WOULD LIKE TO SAY BIG UP FOR ALL U HAVE DONE

    TANZANIA DSM

  13. Comment by RAMAIYA SONJI/NANCY on January 9th, 2010 6:07 am

    “HAPPY BIRTHDAY” KANUMBA

    HONGERA SANA STEPHEN KANUMBA KWA KUKUKUMBUKA SIKU YAKO YA KUZALIWA MUNGU AKUPE MAISHA MAREFU. MTEGEMEE MUNGU KWA KILA JAMBO.

  14. Comment by Mangalili A.M on January 9th, 2010 3:52 pm

    Happy birthday to u! We appreciate ur talent and indeed we enjoy watching ur movies. Keep it up and God bless u.

    SWEDEN

  15. Comment by usa on January 9th, 2010 6:07 pm

    hongera steven aka the great unafanya kazi nzuri ila inawezekana kupatan movie zako huku usa? tafuta wadau wawe wanauza tunazihutaji

  16. Comment by usa on January 9th, 2010 6:08 pm

    hongera kwa kazi nzuri, hivi huku ua tutapataje movie zako?

  17. Comment by Baraka on January 10th, 2010 8:28 am

    Happy birthdy Kanumba

  18. Comment by salome on January 11th, 2010 2:47 am

    Jitahidi kazi kubwa mbele

  19. Comment by MG on January 11th, 2010 4:25 am

    Kanumba mimi nakubali sana kazi yako. Ila pia usipuuze ushauri wa watu kuhusiana na kujua lugha kwasababu sio kwamba wanakutakia mabaya. Sawa wengine wa Bollywood na Nolyywood wanaweza wakawa hawajui lugha ila wamefanikiwa lakini si vibaya wewe ukaja kivingnine kwamba ukajifunza lugha kwa ufasaha.

    Mi nakutakia mafanikio sana mdogo wangu.Natamani siku moja nikuone face to face.

    Halafu pia swali la uzushi tu,unajisikiaje pale unaona move kwa juu imeandikwa kwa Kiingereza halafu ndani ukakuta ni Kiitaliano!!?? tafakari

  20. Comment by eva on January 11th, 2010 5:44 am

    hongera kaka, mungu akusimamie sku zote, unafanya kazi nzuri sana keep it up bro.

  21. Comment by genov on January 11th, 2010 7:15 am

    kazana kjana mchuma usikuache huo! mwombe mungu nae akupe afya njema katika kazi zako za kila siku. ila ningekushauri pia uende darasani zaidi bro!othewise uko vizuri

  22. Comment by Mallya on January 11th, 2010 7:51 am

    HAPPY BIRTHDAY!!!!!!!!!!!!!!

    Kanumba kumbe wewe ni kinda sana, miaka 26 ila unaonekana bonge la mkaka, hongera sana, na pia una kipaji ila ni kwanini mnatoa move kila mwezi tulia hata baada ya mwaka ila mnatoa kitu cha uhakika, ushauri wangu huo, otherwise big-up!!!!!!!!

  23. Comment by Perez on January 13th, 2010 1:34 pm

    Mungu akubariki na kukutangulia. Mtake msaada popote pale unapokwama.
    Good Lucky mwaka 2010

  24. Comment by fabo yusuph on January 14th, 2010 3:56 am

    nakuamini na ninakukubali sana cha umuhimu nikumuomba mungu akufikishe mbali inshallah fabo from sweden

  25. Comment by steven kanumba on January 14th, 2010 1:54 pm

    Asanteni nyote kwa upendo wa dhati Mungu awabariki sana..amen.

  26. Comment by faraji kabuta on January 16th, 2010 6:13 am

    marais kama karume ndio wanatakiwa kuongoza dunia hasa afrika maana c warafi wa madaraka

  27. Comment by faraji kabuta on January 16th, 2010 6:15 am

    pinda upo juu wakipatikana viongozi mia moja kama wewe bac tanzania tunaondokana na umaskini

  28. Comment by esther wilbert on January 16th, 2010 6:17 am

    wawaa pinda big up sana!!!

  29. Comment by WILLO on January 16th, 2010 12:28 pm

    pinda utakufa maskini kama kanumba .kwa kucheza muvi asizojua mantiki yake kama kawawa., na alicheza muvi kibao hata ya muhogo mchungu /watoto wake tunapigao box swiden,..bongo ukipata sehemu vuna on spot.///hakuna mbongo mwenye machungu na nchi yake ZAIDI YA KIKWETE,,,wengine wote tupo kwa ajili y KUKEJELI VIONGOZI ./na ni wengi hao ,..ona wanavyojaribu kumsinga Ngereja,…changamka bob

  30. Comment by NYIRABU on January 26th, 2010 12:21 pm

    Kanumba my Brother wewe ni muimbaji mzuri sana wa nyimbo za Gospel.Mungu kakupa kipaji hicho kwamakusudi ili Baadae ujekumuimbia mbinguni.
    But naomba my brother steven mkumbuke mungu sana popote uwapo kazini,unapo lala,hata utembeapo maana adui wapo wengisana so praise the loard everyday because ur 1st of ur life.Ok GOD BLESS U,BYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!.

  31. Comment by hakimu on March 16th, 2010 8:17 am

    nakupa big sana kaka, uko juu zaidi ya actors wote tz, tunasubiri vitu vikubwa kutoka kwako ili viweze kufunika wengine wote akiwemo anayejiita the most great.

  32. Comment by emmanuel on May 16th, 2010 12:13 pm

    kaka jita hidi na Mungu akusaidie usiwe na kiburi mana kiburi ndio kinacho muharibu mtu wapenzi wa kazi yako wana taka waku one ukiwa simple sio mjivuno ila una kipaji kaka.

  33. Comment by john kas wa congo drc akiwa china on July 25th, 2010 12:58 pm

    congo, tunasubiri na hamu kubwa vitendo vyako filamu zako zinafatwa ama kutazamwa sana kwetu
    nashukuru kazi zako.

  34. Comment by Winnie Mueni on October 2nd, 2010 3:54 am

    Kazi nzuri kaka, lakini fanya juu chini uwatembelee wanakenya na uwafunze mengi juu ya KU ACT FILAMU.

  35. Comment by kemmy on February 9th, 2011 3:47 am

    HAPPY BIRTH DAY CHAMPION MUNGU AKUKUZE NAMUFANIKIO YAZIDI HONGERA IWISH YOU A LONG LIFE AND ACHIVE THE MASSIVE SUCSES

  36. Comment by Upendo on March 10th, 2011 8:10 am

    Hi! Kanumba
    Hope ur doing well,

    Napenda kuchukua nafasi hii kwanza kabisa kukupongeza kwa kazi zako nzuri unazofanya. kwakweli upo Juu Sana, wewe ni msanii wangu bora wa kiume hapa Tanzania japo wapo na wngne ila nikipewa nafasi ya kuchagua one of them is u Kanumba big up sana.

    Napenda pia chukua nafsi hii kutaka kujua kitu ambacho nilikiona Clouds Tv, sio siri kilinisuprise sana mpaka nakajisikia vibaya kama kweli kwa muonekano wako unaweza ukawa na roho mbya kiasi cha kuto kumsaport ndugu yako!

    Ni kuhusu yule kaka alijitambulisha kwa jina anaitwa Stephano Kanumba ambaye amesema ni Last born wenu is it Kanumba? km wewe ni msanii mkubwa kiasi hiki kwa nini usimsaport nduguyo na yeye akafikia ndoto zake.
    unaja nini mimi ni mkristo tena nimeokaka naipenda Biblia na kuisoma sana kuna mstari unasema upendo unaanzia nyumbani, sasa kama kuna watu unawasaidia na wanatoka na isitoshe una kampuni yako kwanini usifanye kwa nduguyo? au yule kaka sio ndugu yako? na km ni ndugu yako kwanini usimsaport jamani na yeye akafikia malengo.

    Nionavyo mimi ni ile hali ya wewe kuwa msanii mkubwa halafu nduguyo anahangaika kutoka. Kama kuna uwezekano msaidie. Japo kuwa yawezekana ni mambo ya kifamilia ila sisi ni wadau wa kazi zako na pia wewe ni kioo cha jamii my brother.

    km utaupenda ushauri wangu nitashukuru kama huto upenda basi. asante kazi njema

  37. Comment by bongocelebrity on March 10th, 2011 12:40 pm

    Upendo.
    Tutajaribu kumpata Kanumba kuhusu suala hili.Stay tuned.Asante.

  38. Comment by shukuru on March 29th, 2011 2:06 pm

    kanumba unajuwa tunakupenda saana sasa unaweza kutuambia utaowa lini? ou mchumba wako nani?

  39. Comment by gladness on April 9th, 2011 3:48 am

    mm naona uwe unacheza na hao watoto tu.Sihivyo visichana vinavyouza sura na kwenda uchi.kama li anti silipendi? bola dada johari anajiheshimu.sijui kwann hupendi kumtumia? kumbuka kakuvumisha! JOHARI NJIA PANDA Mpaka sasa inabamba.

  40. Comment by hamisi nyale on September 27th, 2011 7:40 am

    happy birthday mseya. wishh u all da best. am 1 of ua fans 4rom msa kenya

  41. Comment by Hamisi Bora a.k.a Kaka Boraxz on October 29th, 2011 5:24 am

    Hi Da Great, Hongera kwa bidii yako na kazi nzuri ila usimusahau Mola wako nakumuasi kwakua sasa ni bonge la star. Makinika wala usiwe na kibri kwa wasanii wa chini. Congratulations, Mombasa upo juu. By:- Hamisi Bora a.k.a Kaka Boraxz-Mombasani.

  42. Comment by jacque on February 3rd, 2012 9:20 am

    kaka uko juu sana, naikubali kazi yako

Leave a Reply