
Rais wa Zanzibar Dr Karume ametangaza kutogombea tena uraisi katika uchaguzi ujao mwakani kwa kuwa katiba ya Zanzibar haimruhusu yeye kufanya hivyo.
Raisi ameyasema hayo hapo jana kwenye hotuba yake Kwenye sherehe za Miaka 46 ya Mapinduzi Zanzibar zilizofanyika kwenye viwanja vya Gombani Pemba ambazo zilihudhuriwa na na viongozi mbalimbali wa chama na serikali akiwemo Rais Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Mstaafu Benjamini William Mkapa,Rais Mstaafu Mzee Alhaj Hassan Mwinyi,Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda,Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa,Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi Cuf Sheif Sharrif Hamad pamoja na Lipumba,Waziri Kiongozi wa serikali ya mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa Nahodha na Wakuu wa Majeshi na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama.
Je unadhani nini itakuwa ni hatma ya Chama Cha Mapinduzi huko Zanzibar? Wakati wa CUF umewadia?Nani atamrithi Karume?
Source: Charaz
Feedback / Comments
One Response to “KARUME KUTOGOMBEA TENA;KATIBA HAIMRUHUSU”
Leave a Reply


sending...
Nahisi CCM wakafanya mbinu zilezile za uchaguzi zilizofanyika 2005 ili walazimishe kuwepo Serikali ya Mseto 2010. Bado CCM hawaiamini CUF kushika serikali wenyewe maana watawafanya kitu mbaya mno. Ni kweli Serikali imejitahidi sana kufumba macho na kuwabana wana-CUF zanz lakini nahisi harufu ya damu itakuwepo Maana kwa spirit ya Mapinduzi ile ile mapanga yanaweza pita tena maana kizazi cha mapinduzi bado kipo. Hata hivyo, matatizo ya Zanzibar hayatamalizwa na Uwepo wa CUF madarakani. Maana bado Pemba na Unguja si wamoja. Kuna uwezekano wa Shamsa Vuai kuongoza Zanz, na Maalim akawa Waziri Kiongozi.