Kila siku huwa napokea hoja,mapendekezo,ushauri kutoka kwenu wasomaji wa BC.Pia huwa napokea maswali mbalimbali.Nikiwa na ufahamu mkubwa juu ya swali lililoulizwa huwa najibu.Ninapokuwa sina jibu,wajibu wangu ni kutafuta jibu ama kwa kuomba msaada kutoka kwenu wasomaji na wachangiaji wa BC au vinginevyo. Leo nimepokea swali ambalo sina jibu kwani swali hili limeelekezwa moja kwa moja kwa celebrities. Mwenzetu mmoja ameuliza swali lililopo hapo chini na mwisho ametoa ombi.
Ningefurahi sana kama angalau celebrity mmoja angejitolea kulijibu. Sio lazima ajibu kama mwakilishi wa celebrities wengine,bali yeye kama mtu binafsi. Asante Allen kwa swali zuri.
Napenda kuwapongeza sana kwa kazi nzuri mnayofanya. Nina swali dogo sana kwa hawa Bongo Celebrity kwamba mbona hatuwaoni wakiwa mstari wa mbele katika kuhakikisha nchi yetu inapunguza au kutokomeza kabisa vifo vya mama na mtoto vinavyotokana na uzazi.
Mwezi wa kumi na mbili mwaka jana tulishuhudia mwana Mitindo mashuhuri nchini Uingereza Naomi Campbel akifanya onyesho la mitindo pale Movenpick kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kupunguza vifo vya mama na mtoto dunia nzima. Wanamuziki wetu, wanamichezo , wanamitindo na hawa wengine tunaowaita Bongo Celebrity wako wapi katika kuhakikisha nchi yao inafikia malengo ya milenia namba 4 na tano ifikao 2015.
Hongera kwa Stara Thomas kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha nchi yetu inapunguza vifo vya mama na mtoto kwa kiasi kikubwa. Napenda kuwakumbusha kuwa Tanzania bila vifo vya mama na mtoto inawezekana.
Timu ya taifa ilipocheza na Ivory Cost fedha nyingi sana zilipatikana.
Wachezaji hawa ni matokeo ya kina mama hawa ambao leo wanakufa kutokana na matatizo ya ujauzito. Tunaweza kutumia timu yetu ya taifa kupunguza pia vifo hivi vya mama na mtoto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni miongoni mwa viongozi wakubwa duniani wanaohakikisha nchi zao zinapunguza vifo vya mama na mtoto.
Nawaombatuungane pamoja kwa kutumia vipaji Mungu alivyotupatia kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa tanzania kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa vipaji vyetu na umaarufu tulio nao katika jamii yetu.
Page 1 of 3 | Next page