
Mpoki ana single mpya.Single ya kwanza.Na yeye ameamua kujaribu “muziki”.Anasema anatest zali kwa sababu anasikia muziki unalipa.Anawaomba watanzania mu-mkaribishe.
Wimbo unaitwa Shangazi.Imetengenezwa ndani ya Fishcrab Studio na Producer Lamar. Kuna maneno ambayo nimeyasikia mtaani.Maneno yenyewe ni kwamba wimbo huu ni kama vile majibu ya wimbo wa Mjomba kutoka kwa Poet Mpoto Mrisho kwani Mjomba mara nyingi mwenzie ni Shangazi.Hebu usikilize hapa chini na kisha uniambie,je kuna uelekeo wowote kwa wimbo huu kuwa majibu kwa mjomba? Maudhui yake yanaonyesha hivyo? All in all, karibu Mpoki.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Ukitaka kusikiliza wimbo wa Mjomba kutoka kwa Mpoto Mrisho bonyeza hapa.
Feedback / Comments
24 Responses to ““SHANGAZI”-MPOKI”
Leave a Reply


sending...
Huu Hauwezi kuwa wimbo,jamaa aendelee tuu na maigizo au kukipigia kampeni ccm sio fani ya music
Nimeanza kucheka kabla sijasikia mashairi ya wimbo wake lakini jina la wimbo tayari nimeshapata ujumbe!….. kama tulivyodokezwa inaonyesha ni majibu ya Mjomba Mrisho Mpoto. Mimi binafsi nafurahi kuona wasanii wetu wanajaribu kuonyesha uwezo walionao kufikisha ujumbe kwetu! Haijarishi wanakosoa,wanafundisha au kuburudisha la msingi ujumbe ufike tu! Alichofanya Mpoki ndicho walichofanya wasanii wetu wengi wa bongo flava. Walianza kuachia track zao za kwanza yakiwa majibu ya track za wasanii waliotangulia na kwa bahati mbaya wengi kati ya wasanii wa aina hii nyimbo zao za kwanza huwa hazichezwi sana ktk redio kutokana na ubora wake! Lakini next time wakijaribu tena huwa wanafanikiwa sana! Wasanii wengi walianza hivyo hivyo! Kwa hiyo mimi binafsi naunga mkono kwa asilimia zote! ………. You’re welcome keep it up..
kaka umedhihirisha wewe ni mchekeshaji zaidi ya mwimbaji so kazi buti kwenye uchekeshaji zaidi maana hii nyimbo inachekesha zaidi…au ndio style nyingine ya comedy unakuja nayo mwaka huu? kama ndivyo nitakuelewa zaidi…!
Keep it up, mashahiri yako ni mazito. Mwanzo ngumu na utapata negative comments nyingi but wewe usijali. Najua haya mashairi umekaa na kutunga hujakurupuka na kuimba, amabao hawajaelewa wanasema na kucheka kwamba huwezi kuimba. mimi nimepeda beats, utulivu na mashairi. Big up endelea tu, watakubali baadae kazi yako
hahahhahahhahahhahhahahhahahhaha
uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii mbavu zangu yani nimecheka sana nilikuwa nausongo mkubwa wakuusikia huu wimbo wa shangazi nimecheka kiukweli tena peke yangu hadi naonekana chizi siongezi zaidi CR kesha sema kaka wewe ni mchekeshaji.
ACHA KUPOTEZA MUDA!STAY FOCUD ON COMEDY!!!
NENO LA KWANZA TU NIKAZIMA NA RADIO HAPO HAPO!!
Mpoki ujumbe umefika.. maudhui ya wimbo wako ni mazito. I hope Shangazi amepata somo tosha.. Shangazi inabidi aelewe uwepo wake kwenye baraza la mawaziri ni wa upendeleo kutoka kwa raisi ambaye jamii imeanza kujiuliza mengi juu ya utendaji wake wa kazi. Shangazi pia aelewe kushinda kwake kuwa mwenyekiti wa jumuia ya wanawake ni jibu tosha kwa watanzania wajiulizao kwa nini bado yuko kwenye baraza la mawaziri wakati akili zake ni nusu kilo. Mjomba nahitaji msaada wa kila kona vinginevyo atakuwa Mjomba wa kwanza kushikilia kiti kwa miaka mitano tu. Mjomba pia anaelewa msuguano utakaokuwapo wakati wa vikao vya chama chetu kitukufu hivyo anahitaji msaada wacheza mdundiko kama Shangazi ili wamsaidie kuiba kura ndani ya chama.. Watanzania hatuna wa kumlaumu kwa kuwa macho tunayo lakini tunayafumba… masikio yunayo lakini tunayaziba.. akili tunazo lakini hatuzitumii ipasavyo.. Mjomba kashaanza kampeni.. mara Mwanza, mara Shinyanga ni ajabu tangu mwaka uanze hajapaa kwenda zake kutalii ng’ambo kwa nini? kwa sababu huu ni mwaka wa kuwadanganya watanzania, mwaka wa uchaguzi mkuu..Mjomba bado anaota kurejea kwa kishindo
duh . mimi kwa upande wangu comments zangu naona comed iko ndani ya sanaa kwa model ya kipekee . keep it up karibu ndani ya fani mwanzo mgumu .
Mwimbo mzuri sana na unachekesha endelea Mpoki
Huyu shangazi mimi mbona naona kama kazungumziwa mtu? maana anasema shangazi anaropoka kuhusu ufisadi, mara anamwambia mama mdogo akapimwe akili, n.k hayo yote yanamhusu anna kilango malecela.
Huu ni mtazamo wangu maana Anna aliwahi kumwambia mama mdogo akapime akili katika vita dhidi ya ufisadi
Mpoki mi nakukubali mno ur the best. U alwayz rocks, do wat ur doin ma men, ingnore them harerz
sasa wewe mpoki unajaribu kuimba mziki au unajaribu kutumia nguvu ili utoke kimaisha .kama unataka kutoka basi kaka umeshatoka ki comedy au kama unataka kutumia nguvu kuingia anaga za watu sikunasihi kwani kila kitu na pahala pake huwezi kuchukua ringi la katapila kuendeshea baiskeli….ni bora ukawaachia watu wa fani hiyo kwani mziki ni jukumu usije ukawaharibia wasanii a mziki wa kizazi kipya kwa wakaambiwa kwamba asanii wakileo wanakurupuka likashuka soko lao njee.duuuuuuuuuuuuuuuu bongo bwana kila kitu mzukaaaaaaaaaaaaaa..
Wimbo unalipa endelea Mpoki.
kaka wa ukweli! unakubalika kijamii. huyo sijui mpoto hana lolote wala nini, kaka wewe wa ukweli. hizo ni salamu zangu kwako shangazi~!
Big up bro message delivery, keep it up.
WE KWANI ULIKUA UNAIMBA AU ULIKUA KATIKA KUWAKILISHA COMEDY? INAELEKEA WATU WENGINE
HAWAELEWI TENA ILI INOGE ZAIDI ILI BIDI
UONESHE HUJUI KABISAAA MASWALA YA MZIKI
ILA HUMOHUMO TWENDE KAZI WATAKOMA WENYEWE
INABIDI WAANDAE MBAVU ZA SPARE
HAWAKUKUBALI MBONA UKIONGEA WANACHEKA
AU NDO KUKUBALI KIAINA? I DON’T NO!
BIG UP ALL THE BEST
umeanza vizuri mzee, kaza buti,potezea majungu
kwa wasioelewa watafurahi nawatasema nyimbo nzur but kwa wat weny akilizao timam hujawaconvice kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa na wataona umeongea pumba sasa naona uzalendo umekushind kwa hiy tunamashamba matatu tutakuajir kutokana na experienc yako ya kuchekesh .nyimbo mbayaaaa naona waliosema zikiwa na vina hazina mana NDIO HIZIII
UNGEPITIA BONGO STARSACH SIJUI UNGETOKEA MLANGO GANI MDOGO WANGU.MWENZANGU NYIMBO IMECHACHA BADO KUTOA HARUFU TU….NYIMBO IMEFUTA MPAKA RECORD YAKO YA NYUMA UKO.MDEMBWEDO NDO HUUU SASA TUMEUSIKIA.LOOOOOOOOO
DONT GIV UP
aah,ndugu yangu,kama umeamua kufanya kazi we fanya tu,kwani hata nyimbo za wasanii wanaovuma kwa sasa kuna baadhi ya watu hawazipendi.sasa kazi kwako,kwani hii nyimbo kuna watu wanaoipenda na wasioipenda.binafsi napenda sana komedi,kwa hiyo bila ya kuingia ndani saana,mi nimependa komedi ya wimbo huu,na hata biti imetulia.si unajua tena baadhi yetu tulivyotekwa na nyimbo za mapenzi,lakini ukimlenga mtu kwa manufaa ya taifa!ooh, nyimbo mbaya,wakowapi wagosi wa kaya? kulikuwa na uongo gani kwenye nyimbo zao? na nyingi walikuwa wakiziwakilisha wa njia ya kikomedy.kila la kheri kwa kila mwenye niya ya kuingia kwenye fani.ila usijaribu,ingia kwa nguvu zote.nisipoteze muda,wacha niisikilize tena hii nyimbo.
karibu mpoki
kaka unatisha achana na hao wasenge hapo juu wanaochonga ambao hawapendi kuona maendeleo ya mtu akishine
mm nakukubali kinyama best
ora we ni wa ukwel,mi nakukubal mwanzo mwisho,uccklze maneno ya wa2,ohhh focus on comedy nop hao ni wapumbav 2