
Nina imani kwamba hujawasahau Wagosi wa Kaya.Naam ni wale wale vijana kutoka Tanga ambao miaka ileee waliingia kwenye anga za muziki kwa kishindo pale walipohoji “Tanga Kunani Pale”?
Tangu pale Wagosi wa Kaya wakawa wamejikita katika ile aina ya muziki wa kizazi kipya ambao mimi hupenda kuuita “conscious” kwa maana ya kwamba unalenga kwa undani kile kinachoendelea katika jamii.Ukipenda uite “muziki tambuzi”.
Baada ya kuwa kimya kwa miaka kadhaa(hata wao wanakiri katika wimbo huu kwamba walikuwa kimya kwa muda mrefu) wamerudi.Na mara hii wamerudi wakiwa na timing ya aina yake.Wanagusia uchaguzi,siasa na mambo kama hayo. Kama unavyojua,mwaka huu,watanzania watajipanga foleni ili kuchagua tena viongozi.Demokrasia.Wao wanasema ni Maumivu ya Miaka 10!
Wasikilize Wagosi wa Kaya kwa kubonyeza player hapo chini.Sikiliza kwa makini ujumbe kwani kwa maoni yangu,kidogo sauti ya beats ni ya juu kuliko za wanaoghani.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Picha kwa hisani ya outhere.de.
Feedback / Comments
3 Responses to ““MAUMIVU YA MIAKA”-WAGOSI WA KAYA”
Leave a Reply


sending...
Ee bwana hawa jamaa nawakubali.Vichwa.Karibuni tena wagosi
Jamaa wanajua maana ya muziki. Si kila mtu anaweza kupata nafasi ya kusimama jukwaani na kukosoa sera na uongozi mbaya bila kukutana na mkono mrefu wa dola. Lakini kupitia muziki unaweza kufikisha ujumbe kwa hadhira kubwa ndani ya muda mfupi. Ukitaka kujua thamni ya muziki katika mapinduzi basi angalia namna makaburu, madikteta na wanyonyaji wengine wanavyohaha kudhibiti nyimbo za kimapinduzi. Hongera sana Wagosi.
hawa wanamme wamesimama music wao si wezi download free lazima ni nunue tape cos nataka waendelee kuexist foreva, kiukweli ni kwamba nyie muziki mnaujua na mnapo kua nje ya gem mda mrefu mnatukata stim cos matatizo najua mengi tu yakuongelea haya na wapa na jingine la wanjeshi waonevu tungieni vesi basi nayo, kuna nyumba ya banki kuu mkuu wao kaiba tnayo pia vesi yake
thanx wagos