MADARAKA NYERERE’S BLOG

Nimekuwa katika vuguvugu la habari na mawasiliano kwa njia ya blog kwa muda sasa.Kila siku huwa napitia blogs zaidi ya 500! Huwa natumia huduma ya www.bloglines.com. Ukiandika kitu basi naambiwa umeandika na hivyo napita na kusoma.Ukiwa hujaandika,basi siku hiyo napata muda wa kuperuzi au kutafuta blogs zingine,kuziingiza kwenye orodha yangu ya bloglines.Siku inakuwa imekwenda au naendelea na kazi zingine.

Leo nikiwa katika pitia pitia yangu mtandaoni,nimekutana na blog ya Madaraka Nyerere,mtoto wa Hayati Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Cha kwanza kilichonijia kichwani ni hasira fulani.Iweje siku zote hizi sikujua kuhusu blog ya Madaraka? Haikutangazwa au ilikuwaje? Hasira zangu ziliyeyuka kama vile barafu inapopigwa na jua baada ya kuanza kuipitia blog yake.Imesheheni habari kemkem.Madaraka ni mwandishi mzuri.Simulizi zake ni nyepesi kama pamba lakini maudhui yake ni mazito kuliko yale mawe yanaouzunguka mji wa Mwanza.

Bonyeza hapa ili kuitembelea blog hiyo. Nikisema mkaribishe nitakuwa nakosea kwani amekuwepo kwa muda sasa.Bravo Madaraka.

Pichani juu ni Madaraka Nyerere(kulia) akiwa na Jaffar Amin,mtoto wa Iddi Amini aliyewahi kuwa Rais wa Uganda. Soma zaidi kuhusu mkutano wao.

Page 1 of 3 | Next page