Habari kubwa iliyopo kurasa za mbele za vyombo vya habari ulimwenguni hivi leo ni kuhusu hotuba ya Rais wa Marekani,Barack Obama hapo jana usiku.Wenyewe wanaiita State Of The Union. Kama hukuiona,unaweza kuitazama hotuba nzima katika video hiyo hapo chini.
Kwa mtazamo wangu hotuba hii ni nzuri na ambayo viongozi mbalimbali duniani(hata katika nchi zetu za Afrika) wanaweza pia kuitumia kama kioo katika uongozi wao.Kuna mahali Obama alisema ukishachaguliwa kuwa kiongozi basi ufanye kweli kazi ya kuongoza(leadership) na kutengeneza kesho ya kizazi kijacho(next generation) na sio tu kwa sababu unataka kushinda uchaguzi ujao(next election). Alitia pia msisitizo wa kukumbuka kwamba upo hapo ulipo kwa sababu waliokutangulia,waliandaa mazingira mazuri kwa ajili yako.Bravo Obama!
Feedback / Comments
One Response to “IN CASE YOU DIDN’T WATCH OBAMA’S STATE OF THE UNION SPEECH…”
Leave a Reply


sending...
Amani kwenu wana-BC wote!……. speech ya OBAMA niliipata vipande vipande ingawa sijaipata kwa ukamilifu lkn sehemu ya vipande nilivyovipata namkubali sana mheshimiwa kwa hotuba zake nzuri! Obama kwa kweli mimi nasema ni bingwa wa hotuba sasa sina uhakika kama anayoyaeleza ktk hizi hotuba zake anayo uwezo wa kuyatekeleza? Kwa sababu Obama ana malengo makubwa sana ya kuusukuma uchumi wa Marekani na Dunia kwa ujumla lakini si uchumi tu! Bali kutengeneza mazingira mazuri yatakayopelekea kuwa na dunia yenye amani pande zote! Tumeona kwa muda mfupi takriban mwaka mmoja toka aingie ikulu tayari ameshafanya mikutano mikubwa ya kidunia yenye malengo makubwa kwa dunia nzima! Kwa ktk hotuba yake ile ya juzi tumeiona jinsi viongozi wote waliokuwepo pale wakimsikiliza jinsi walivyokuwa wanakubali kwa vichwa na kuinuka wote kwa pamoja na kupiga makofi wakiashiria dhahiri kwamba wanaunga mkono maneno ya kwa % zote! ila khofu yangu naona tayari ahadi zimeshakuwa nyingi sana si za Marekani bali za dunia! Je? Uwezo wa kutekeleza ahadi hizi upo kwa muda mfupi alionao? Hatari iliyopo ni kwamba muda alionao ukilinganisha na majukumu na ahadi alizotoa ni kubwa kwa kuwatumikia wamarekani na dunia kwa ujumla! Mtaka yote hukosa yote! Lakini hatumuombei hayo bali tunamtakia mafanikio mema kwa maslahi ya wamarekani na sisi wenyewe!….. Mungu ampe uwezo wa kufanikisha majukumu aliyonayo….. Amen!