
Mashabiki wa muziki,hususani wa R&B waliopo katika ukanda wa Afrika Mashariki na hususani jijini Kampala nchini Uganda,huenda kesho wakashuhudia onyesho ambalo hawajashuhudia ndani ya miaka kadhaa na huenda wasishuhudie katika miaka kadhaa ijayo.Hiyo ni ahadi,sio kutoka kwangu bali kutoka kwa mwanamuziki Robert Sylvester Kelly maarufu kama R.Kelly(pichani) kutoka nchini Marekani anayetarajiwa kufanya onyesho la aina yake hapo kesho jijini Kampala katika ukumbi wa Lugogo Cricket Oval.
Onyesho hilo ambalo limedhaminiwa na kampuni ya simu ya Zain,limepewa jina la “I Believe”.Hivi karibuni iliarifiwa kwamba kampuni ya Zain imetumbukiza zaidi ya $2.5 kwa ajili ya onyesho hilo kwani inasemekana kwamba kwa R.Kelly kukubali kufanya show yoyote nje ya Amerika Kaskazini basi $600,000 lazima ziwe mezani. Viingilio katika onyesho hilo ambalo tiketi zake zilishakwisha(sold out) wiki mbili zilizopita, vimepangwa kuwa Ushs 30,000(Silver) Ushs 125,000(Gold) na Ushs 250,000(Platinum). Hii ni mara ya kwanza kwa R.Kelly kufanya concert katika ukanda wa Afrika Mashariki. Na barani Afrika kwa ujumla mahali pengine ambapo amewahi kufanya onyesho ni Afrika Kusini tu.
R.Kelly ameahidi kuimba nyimbo zake zote ambazo amewahi kutamba nazo kama vile Bump n’Grind, I Believe I Can Fly,Gotham City,Ignition(Remix),The World’s Greatest,If I could turn back the hands of time, na nyinginezo tele bila kusahau hip-hopera yake ya Trapped In A Closet.
Sasa kwa wale ambao mmeshawahi kuhudhuria show yeyote ya R.Kelly,mnajua kwamba yeye hupenda mashabiki wanaokwenda naye sambamba.Hupenda kuwashirikisha hadhira(audience).Kazi kwenu.Jukwaani R.Kelly anatarajia kusindikizwa na wasanii wa Uganda Bebe Cool,Jose Chameleon,GNL,Peter Miles na Goodlyf ambao ni Radio na Weasel.Wote hao wamepigiwa kura na waganda wenyewe ili kupata nafasi hiyo.
Here is one my favourite from him; Step In The Name Of Love.
Feedback / Comments
2 Responses to “KESHO NI KESHO JIJINI KAMPALA:R.KELLY IS IN TOWN”
Leave a Reply


sending...
Duh! Bab kubwa………… R.Kelly ni msanii wa ki ukweli hasa! Si mbabaishaji yupo ktk game kitambo and still he performs at maximum level! He has released all kind of music! So you can get all flavor you like i dont have to mention them for any one who knows him he will agree with me! I real feel him! HE IS THE BEST.
Nassor!!!
Nakubaliana na wewe. Robert (R.Kelly) ni mkali hasa katika mabluzzz yake ya kimapenzi ni hatari sana.
Kitu alichokosea ni kwenda nchi isiyokuwa na wajuaji. Angetua “Bongo” angerudi na picha kamili ya Afrika kuwa ni kweli yeye mwenyewe asili yake kutoka Afrika. Hasa kutoka Tanzania.
Bongo kumekucha. Mtu asiyekuwa nacho ndiye anayelalamika maisha magumu. Lakini hata “Wamachinga” Bongo wanakula maisha ya uhakika. Kila sikukuu beach za Tanzania Dar es salaam, zimejaa watu wakitanua. Usidhani ni vibosile hao. Ni Chinga wetu wanatanua baada ya kazi.
Habari ndiyo hiyo, sina mengi kwa leo.
This Is Black=Blackmannen