When the news surfaced that, Hasheem Thabeet, is headed to the Development League (D-League), the reaction among Tanzanians especially the users of social networks such as Facebook and blogs were overwhelming. I guess the big question in lots of folk’s minds was; what is a D-League? Does it suggest that he is no longer going to be playing in the usual NBA league? Well, it depends on a lot of things. You can read more about the D-League and its implications or benefits to Hasheem career by clicking here and also here.
The social networks such as Facebook and blogs were immediately stuffed with comments and opinions. Some were wishing him a “quick comeback “to the NBA, while some couldn’t hesitate to throw jabs on him in the sentiment of “we told you”.
I guess the news was “worth the talk”, because not only Hasheem is the first Tanzanian ever to play in the NBA, but also the highest draft pick ever to go to the D-League. Thabeet, who has played sparingly in his rookie season, averaging 2.5 points in 10.3 minutes over 50 games, has been optioned to the Dakota Wizards. He made his debut yesterday when Dakota Wizards played Erie Bayhawks. Dakota Wizards won 108-103.
Before his debut in the D-League, I had caught up with Hasheem with only one question in my mind; about his reaction following the demotion to the D-League. This is how it went;
BC: Hasheem, what is your reaction to this whole thing of moving to the D-League?
HASHEEM THABEET: My reaction about D-League…Uhmmm… well I’m excited to participate in the D-League. I’m looking forward to playing and maximizing this opportunity to be on court and use the skills that I have developed thus far rather than to be on the bench.
Right now the key for me is consistency court time as I am still learning the Pro Game. I know Coach Hollins has my best interest at heart so I’m happy with his decision which I believe is to make sure that I stay active.
Now I know this is the time for the haters and all the doubters to talk and say whatever they have because they have been waiting to bring me down for a minute. So it’s my downtime and I promise I’m not backing back. It’s a new saga that has started. Plus I’m still be getting the same cheque… it’s not like they are not gonna pay me the usual. So I’m still good and soon I’ll be back!!! And oh by the way, I’m only going there for 6 games. So I will be back sooner than they are thinking.
**BC would like to wish Hasheem all the best in the D-League and eventually his return to the NBA.

Kila ifikapo tarehe 13 August, yeye hukumbuka na kusheherekea siku yake ya kuzaliwa. Alipozaliwa pale jijini Mwanza,kaskazini mwa Tanzania wazazi wake walimpa jina la Fareed. Leo hii kwa wengi anatambulika kama Fid Q.
Kama ambavyo umeshasikia,leo hii,tarehe 25 Feb 2010, album yake inayokwenda kwa jina Propaganda inaingia mtaani.Kwa hiyo leo ukizunguka mitaani,usishangae kukutana na mtu kabeba CD mpya ya Fid Q au ukasikia sauti yake kwenye gari,magari,usafiri wa umma.Jambo moja muhimu unaloweza kufanya ni kujipatia nakala yako halisi.Hakuna njia nzuri zaidi ya kuunga mkono juhudi za wasanii zaidi ya hiyo!
Hivi karibuni nilipata nafasi ya kuzungumza machache na Fid Q kuhusu ujio wa albamu hii ya Propaganda,muungano wa wasanii wa bongo fleva na pia suala zima la nyimbo nyingi za bongo fleva kuwa na maudhui ya mapenzi zaidi ya kitu kingine chochote.Kwanini ameiita album yake Propaganda? Anamaanisha nini? Je unajua Fid Q ana mtazamo gani kuhusu muungano wa wasanii?Je anasemaje kuhusu mchango wa vyombo vya habari katika maendeleo au kifo cha muziki wa kizazi kipya? Fuatana nami katika mahojiano yafuatayo;
BC: Kwanza hongera kwa album mpya.Labda kwa ujumla tu,album hii umeitengenezea katika studio zipi,itakuwa na nyimbo ngapi na umewashirikisha wasanii gani wengine?
Fid Q: Asante sana kaka.Album hii nimeifanya katika studio 3 tofauti.Nimefanya kwa MJ Records, Tongwe Records na kwa Lamar.Nimewashirikisha wasanii kama AY, NCHA KALI, MZEE ZORRO, JUMA NATURE,QJ, NYLON WA MANZESE CREW, BI KIDUDE na wengine kibao bila kuwasahau MATONYA na MZUNGU KICHAA.
BC: Kwanini umeiita Propaganda?Kuna ujumbe wowote maalumu kutokana na jina la album? 
Posti hii nilitakiwa kuipandisha jana lakini sikufanikiwa maana jana nilifunga kiroho na kifikra ili kumkumbuka Malcom X, mpigania haki za watu weusi kule Marikani. Malcom X alizaliwa na kupewa jina la Malcom Little kisha akaamua kubadili “Little” na kuweka “X” kwa kile alichodai kuwa jina la awali lilikuwa ni la kikoloni na lenye nia ya kuiba utu wake. “X” inasimama kama “Aliyepotea/Asiye na Jina” ikimaanisha Mwafrika aliyepoteza utambulisho wake baada ya kutekwa na kupelekwa utumwani kule Marikani.
Nimeona niweke posti hii ili tuelewe kwamba isingekuwa Malcom X na wengine waliotangulia kama Martin Luther King Jr., Mama Rosa Parks, au mapambano ya kuwakomboa watumwa ya Reli ya Ardhini” (Undeground Railroad) yaliyoongozwa na mwanamke mweusi Harieth Turbman, pengine Marekani ya leo isingekuwa na Rais Mweusi tunayemfahamu na kumshabikia, Barack Obama.
Malcom X alizaliwa katika familia yenye maisha duni na akiwa na umri wa miaka 13, baba yake ambaye alikuwa mpigania haki za watu weusi pia aliuawa na wazungu wabaguzi waliojulikana kama Ku Klux Klan (KKK), na mama yake alikuwa amefungiwa katika hospitali ya wagonjwa wa akili. Hivyo Malcom akaanza maisha ya kujitegemea akitumia wizi wa mifukoni kama njia ya kujipatia kipato.
Mwaka 1946 Malcom alifungwa jela kutokana na wizi. Akiwa Jela, Malcom ambaye hakuwahi kusoma vitabu akajikuta akiwa msomaji mkubwa wa vitabu ambavyo vilimwongezea maarifa aliyokuja kuyatumia baadae katika mapambano dhidi ya ubaguzi wa watu weupe kwa watu weusi. 
Bila shaka utakubaliana na mimi nikisema kwamba ni vigumu kuongelea wachora katuni maarufu katika Afrika ya Mashariki bila kumtaja Godfrey “Gado” Mwampembwa.Katuni za Gado sio tu ni maarufu bali pia zimewahi kuamsha hisia kali za wahusika. Si unakumbuka jinsi ilivyokuwa Gado alipowachora waandishi wa habari wa kwetu kwamba wanalamba viatu vya mheshimiwa? Unakumbuka jinsi mjadala ule ulivyokuwa?
Godfrey” Gado” Mwampembwa,mzaliwa wa Tanzania ambaye pia ndugu wa kuzaliwa wa Robert Mwampembwa(yule mchoraji wa katuni maarufu ya Bi.Mkora) hufanyia kazi zake nchini Kenya. Yeye ni Political Cartoonist wa magazeti ya Nation ya nchini humo.
Hivi karibuni aliongea na CNN kuhusu kazi zake na hususani kazi zake wakati “watani zetu wa jadi” walipoamua kuangushiana dhahma kufuatia uchaguzi mkuu wa nchini kwao miaka michache iliyopita.Hayo hapo mahojiano yake.
Hii ni kutoka kwa DJ Fetty.Wimbo ninaoupenda zaidi ni wa kwanza hapo kutoka kwa kijana anayeitwa Roma.Wimbo ni Mr.President.Mtembelee DJ Fetty kwa kubonyeza hapa.
Waswahili tunao msemo usemao, Siku njema huonekana asubuhi. Ni msemo wa kale ambao tafsiri yake halisi inaweza kutofautiana baina ya mtumiaji mmoja kwenda mwingine. Huo ndio utamu wa lugha na misemo ya kwetu. Tunaweza kutofautiana lakini wote tukawa sahihi, angalau kwa mapana yake.
Pamoja na tofauti kadhaa zinazoweza kujitokeza katika tafsiri, nina uhakika kwamba wengi tutaelemea katika tafsiri rahisi ambayo ni kwamba unavyoianza siku ndivyo utakavyoimaliza. Hisia na vitendo vyako unapoianza siku yako vina mengi ya kusema kuhusu itakavyokwenda na itavyofikia ukingoni.
Ukiamka na kujihisi mchovu,ukaichukia siku hata kabla haijaanza,ni wazi kwamba utakuwa umejiweka mwenyewe kwenye mtego wa kuwa na siku mbaya! Hutofanikisha malengo yako.Kazini unapokwenda mambo yanaweza kwenda mrama.Kwanini? Umeiandaa vibaya siku yako.Ikitokea mwenzako fulani iwe kazini au shuleni akakuambia mbona leo unaonekana kama unaumwa au umechoka(hata kama anakutania tu) ndio kabisaaa anakuwa amekumaliza.
Kwa upande mwingine, siku njema huonekana asubuhi unaweza kuwa msemo unaoonyesha nguvu ya utabiri tuliyonayo sisi kama wanadamu.Tunazo hisia.Unaweza kuhisi kwamba kitu fulani unachokifanya au unachoacha kukifanya kinaweza kuwa na matokeo yasiyopendeza. Kila mmoja wetu anazo nguvu za utabiri.Tofauti ni jinsi tunavyozitumia,kuziamini au kuzifanyia kazi.
Bahati nzuri ni kwamba binadamu tumepewa uwezo mkubwa wa kunyumbulisha dunia na mambo mbalimbali.Sasa ufanyeje ili uianze siku vizuri? Wataalamu mbalimbali wa mambo ya saikolojia na utabibu wanakubaliana kwamba ukiianza siku yako mapema, itakuwa nzuri! Kuanza siku mapema, kwa mapana na marefu kunajumuisha kuamka mapema na kuwaza vyema.
Leo nimeamua kuongelea umuhimu wa kuamka mapema kwani kama nilivyotangulia kusema hapo juu,wataalamu wengi wanakubaliana kwamba kuamka mapema ni msingi wa kuwa na siku nzuri,maisha mazuri na kubwa zaidi,afya nzuri.Watu wengi ambao tunawaita “waliofanikiwa maishani” na hata matajiri wakubwa hapa duniani,wanalo jambo moja linalofanana. Katika kuwafuatilia(kupitia makala za magazetini,vitabuni na hata mahojiano yao katika televisheni) wote wanakiri jambo moja.Wote ni wa kwanza kudamka(early birds). Kwanini?Bila shaka kuna sababu.
Pengine baada ya kusoma kichwa cha habari umeshajiuliza; kwanini niamke mapema? Sababu ya Kwanza ni kwamba unapoamka mapema, unapata muda mzuri wa kujiweka sawa,kuipanga siku yako vyema. Imeshawahi kukutokea ukakurupuka usingizini na kukuta muda umeshakwenda na umechelewa kwenda unapotakiwa kwenda iwe ni kazini,shuleni au kwingineko? Umeshaona jinsi mpangilio wako wa mambo unavyokwenda kombo? Unapofika ofisini kwa mfano, unakuwa hata kuamka vizuri hujaamka bado na kila mtu anakutolea macho kwa sababu hata nywele hukukumbuka kuchana? Ungeamka mapema,ukaipanga siku yako vyema yote hayo yasingekukuta.
Faida ya pili ni kuweza kutumia ukimya wa asubuhi. Umeshawahi kudamka asubuhi ukaona jinsi palivyo na utulivu wa aina yake? Amini usiamini,ukiutumia ukimya huo wa asubuhi kuwaza na kupanga mambo yako,ni wazi kwamba utafanikiwa zaidi. Akili ya binadamu imetengenezwa ifanye vizuri zaidi panapokuwa na utulivu. Wenzetu wa magharibi ndio maana wakaja na msemo wa Silence is Golden.
Tatu,wataalamu wa afya wanasisitiza sana kuhusu kifungua kinywa(breakfast). Huo ndio mlo muhimu zaidi katika siku. Ni wazi kwamba ukiamka mapema, utapata muda mzuri wa kuandaa na kisha kupata kifungua kinywa kwa utaratibu unaofaa bila papara kitu ambacho ni muhimu kwa afya yako. 

Pamoja na ushabiki wote wa soka nchini ambao siku hizi umejikita sio tu katika timu za Yanga na Simba bali pia timu mbalimbali zinazoshiriki ligi kuu ya nchini Uingereza(English Premier League), bado wengi tunakubaliana kwamba hakuna tukio la soka ulimwenguni linaloshinda mashindano ya kugombea Kombe la Dunia la Soka( Soccer World Cup).
Ubishi na ushindani wa Arsenal, Chelsea, Manchester United, Liverpool, Newcastle nk unapofikia ukingoni,macho na masikio huelekezwa katika Kombe la Dunia. Pale ndipo penye msisimko wa aina yake.Vipaji visivyo vya kawaida huonekana pale. Ndoto hutimizwa pale na pia ndoto huyeyuka au kuota mbawa na kupaa kama vile afanyavyo mwewe baada ya kukidakua kifaranga.
Kama unavyojua,mwaka huu kipute kipo barani kwetu. Hii ni mara ya kwanza kwa bara la Afrika kupewa nafasi ya kuandaa kombe la dunia. Ni mwaka ambao una matumaini mapya kwani ukitazama kwa makini,bara la Afrika lina wasakata kabumbu mahiri sana wanaocheza katika vilabu mbalimbali ulimwenguni hususani barani Ulaya.Mimi sina timu huko Ulaya;ila Real Madrid na Arsenal wakifungwa huwa sijisikii raha! Utaniita mshabiki?
Sasa kama ilivyo kwa matukio mengi makubwa ya michezo duniani,muziki huwa haukosi.Kunakuwa na wimbo maalumu kwa ajili ya mashindano(tournament’s official song). Kombe la dunia pia.Kwa mwaka huu, wimbo Waving Flags (kwa Kiswahili rahisi naweza kusema Kupeperusha Bendera) kutoka kwa mwanamuziki Knaan .Huu ndio World Cup 2010 Official Song.
Knaan ni mzaliwa wa Somalia. Kwa sasa makazi yake ni Toronto,Canada. Ni miongoni mwa wanamuziki wenye asili ya Afrika wanaofanya vizuri sana katika anga za muziki ulimwenguni. Bonyeza hapa ili kutembelea tovuti yake na pia hapa ili kusoma zaidi kuhusu historia yake.
Haya sasa,wimbo huo.Tupeperushe bendera.Je Afrika tutatoka kimasomaso huko Kusini mwa bara letu? Imebaki miezi michache.Usikilize wimbo Waving Flags hapo chini
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Picha na habari kwa hisani ya GetMziki.Watembelee kusikia pia Remix ya wimbo huu.
Baada ya kimya cha takribani miezi mitatu tangu alipokumbwa na kashfa mfululizo juu ya mahusiano yake na “vimwana” nje ya ndoa yake,mcheza golf maarufu ulimwenguni,Tiger Woods, anatarajiwa kuonekana hadharani na kuzungumza na waandishi wa habari juu ya sakata lake.
Kwa mujibu wa wakala wake,Mark Steinberg, mchezaji huyo ataongea na kundi dogo tu la waandishi wa habari siku ya Ijumaa kutokea katika clubhouse ya TPC Sawgrass huko Ponte Vedra Beach jimboni Florida,yalipo makao makuu ya PGA Tour.
Tiger anatarajiwa kuongelea juu ya yaliyojiri,mipango yake ya sasa na baadaye na pia anatarajiwa kuomba msamaha(kwa kinywa chake mwenyewe) juu ya tabia zake. Tayari kuna hisia kwamba Tiger Woods ameamua kujitokeza na kuongea na waandishi wa habari siku hiyo,saa hizo, sio tu kwa sababu anataka kurudi uwanjani,bali pia kwa sababu anataka kuwakomoa waliokuwa wadhamini wake(Accenture) kwani katika muda huo kutakuwa na shindano lililodhaminiwa na Accenture liitwalo Accenture Match Play Championship kutokea Arizona.
Kwa kuongea na waandishi wa habari katika muda huo,matarajio ni kwamba macho na masikio(attention) vitaelekezwa kwake Tiger.Accenture walikuwa wadhamini wa kwanza kutangaza kumtema Tiger Woods mara tu sakata lake lilipoibuka.
Je hiyo ndio kusema Tiger Woods ameamua kurudi tena uwanjani baada ya hapo awali kutangaza kupitia mtandao wake kwamba anapumzika kucheza golf?

Ukumbi umefurika,watu wananyanyua na kushusha mikono.Wanaimba na kucheza.Wengi wamevalia nguo nyekundu.Siku ya siku ni Valentine’s Day au Siku ya Wapendanao.Kila mtu na wake. Ni siku ya kumuonyesha mwenzako kwamba unampenda.Kama alikuwa haamini huenda leo akaamini.Mwanamuziki aliyepo jukwaani ni TID.Mahali ni Platinum Club,Mikocheni.
Ghafla muziki unazimwa.TID anasema kuna kitu anataka sema.Waungwana wakatulia ili kumsikiliza.Anaanza kuongea “Wapendwa, muda umewadia,nataka kuuaga ukapela.Nataka kuoa”. Watu kimyaa, minong’ono ya chini kwa chini,shauku ya kutaka kujua na kusikiliza zaidi!
Kwa mujibu wa John Bukuku wa Full Shangwe,kilichofuata ni TID kumtambulisha mchumba.Anaitwa Kinana(pichani). TID akapiga goti na kutamka “Will You Marry Me”? Binti akakubali.TID and Kinana are engaged.
Hongera TID.Maisha ni hatua.Tunasubiri harusi.Kila la kheri.
Picha na chanzo cha habari:Full Shangwe.

Mimi sio mtaalamu wa Kiswahili.Ukweli huo ndio unanifanya niwe tayari kujifunza.Ndio sababu ya kuuliza swali lililopo katika kichwa cha habari hapo juu.Najaribu kujifunza.
Unapowaweka viongozi hao watatu pichani(wote,katika nyakati tofauti,waliwahi kushika wadhifa wa Waziri Mkuu wa Tanzania) ni sahihi kuwaita wote kuwa ni Waziri au Mawaziri wastaafu? Nauliza swali hili zaidi nikiwa nimemlenga Mheshimiwa Edward Lowassa (Mbunge wa Monduli) ambaye kwa mujibu wa kumbukumbu yangu,alijiuzulu wadhifa wa Uwaziri Mkuu mara baada ya sakata la Richmond kumkalia vibaya.Je kujiuzulu kule kunamaanisha kwamba ni sahihi hivi leo kumuita Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa?


sending...