MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

Miongoni mwa matukio ya ki-muziki ambayo yataendelea kukumbukwa kwa muda mrefu ni pamoja na tukio la jumla ya wanamuziki 45 kukusanyika katika studio za Jim Henson za jijini Los Angeles mwaka 1985 na kutengeneza wimbo ulioitwa We Are The World ambao ulikuwa mahsusi kwa kuchangia fedha kwa ajili ya Afrika na hususani nchi ya Ethiopia ambayo ilikuwa imekumbwa na ukame wa kutisha kuanzia mwaka 1984-1985.Ulikuwa ni umoja na upendo wa aina yake waliouonyesha wanamuziki wale sio tu kwa bara la Afrika bali kwa taasisi nzima ya ubinadamu. Wanamuziki Lionel Richie na Michael Jackson(RIP) ndio walioandika wimbo ule ambao ulifanikiwa kuchangisha jumla ya dola milioni 30 zilizokwenda kusaidia waathirika wa ukame ule.

Katika kujaribu kurudia kile walichofanya superstars wa ulimwengu wa muziki takribani miaka 25 iliyopita, hapo juzi jumla ya wasanii 100 (wengi wao kutoka Marekani) ambao wanatamba hivi sasa katika muziki ulimwenguni,walikusanyika katika studio moja chini ya Producer yule yule aliyefyatua We Are The World ya mwaka 1985,Quincy Jones ili kuutengeneza upya wimbo wa We Are The World(remake of We Are The World). Lakini safari hii sio kwa ajili ya kuchangia Afrika bali ndugu zetu wa Haiti ambao kama unavyojua wiki chache zilizopita nchi yao ilipata tetemeko la ardhi ambalo linahofiwa kwamba lilichukua maisha ya jumla ya watu 200,000.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Original We Are The World.

Baadhi ya wanamuziki wenye majina makubwa ambao wamo katika We Are The World mpya ni pamoja na Wyclef Jean, Kanye West,Celine Dion,Jennifer Hudson,Miley Cyrus,Barbra Streisand,Tony Bennett,Jamie Foxx,Natalie Cole, Akon, Carlos Santana,Josh Groban,Justin Bieber(kijana wa miaka 15 raia wa Canada,alikuwa hajazaliwa huyu mwaka 1985), Snoop Dogg,Drake,LL Cool J na hata Rapper Lil Wayne ambaye anasema alidhani wanamtania alipoambiwa kwamba anahitajika “kuimba”.

Wengine ni kama vile Usher,Jonas Brothers,Pink, Gladys Knight,Wil.i.am,Brandy,Keri Hilson,Busta Rhymes,T-Pain,Robin Thicke,Trey Songz,Adam Levine,Tyrese na wengine kibao.Nitaendelea kuongeza majina ya washiriki wengine katika orodha hii kwa kumbukumbu ya vizazi vijavyo.

Janet Jackson(dada wa Michael Jackson) ambaye hakuwepo studio anatarajiwa kuimba sehemu ya marehemu kaka yake kabla ya kutolewa rasmi kwa video ya remake hii ya We Are The World ambayo inatarajiwa kuonyeshwa rasmi tarehe 12 mwezi huu katika kituo cha televisheni cha NBC cha nchini Marekani kwenda sambamba na ufunguzi wa michezo ya Olympics ya majira ya baridi(Winter Olympics) inayofanyikia huko Vancouver nchini Canada kwa mwaka huu. Video ya wimbo huu mpya imeongozwa na Director wa movie ya Crash(kama hujaiona fanya bidii uione),Paul Haggis.

Je unadhani kuna uwezekano wa wimbo huu uliotengenezwa upya,kuushinda ule wa zamani au kupata mafanikio zaidi ya original? Kuna watu wanasema ni vyema kwamba Lionel Richie na Quincy Jones wapo kusimamia na kuhakikisha kwamba the “1985 spirit ” inabakia pale pale lakini bila kuwepo kwa Michael Jackson ni pengo kubwa sana.Wewe unasemaje?

Photo/Kevin Mazur/wireimage.com. Kwa picha zaidi bonyeza hapa.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

One Response to “THE REMAKE OF “WE ARE THE WORLD””

  1. Comment by Nas on February 3rd, 2010 10:57 am

    Kwa maoni yangu sidhani kama hawa wanamuziki wa sasa wanaweza kufikia kiwango cha wale wa zamani.Wa zamani walikuwa wanafikiria kabla ya kuimba wakati hawa wa sasa wanaimba halafu ndio wanakaa kufikiri.Maoni yangu.

Leave a Reply