Kama wewe ni mtizamaji au mpenzi wa sinema za kutoka nchini Nigeria,bila shaka umewahi kuwaona wachekeshaji wawili wajulikanao kama Aki na Ukwa.Wanasemekana ndio waigizaji wafupi kuliko wote nchini humo.Habari nzuri,kama wewe unapendezwa na vichekesho vya Aki na Ukwa ni kwamba wapo njiani kuja jijini Dar-es-salaam.
Kwa mujibu wa Gazeti la Mwanaspoti,wachekeshaji hao wanatarajiwa kufanya vitu vyao katika tamasha la watoto yatima, na wale wanaoishi katika mazingira magumu Februari 14 mwaka huu. Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika siku ya wapendanao(Valentine’s Day) katika viwanja vya TTCL, Kijitonyama jijini Dar es salaam.
Aki na Ukwa watakuwa nchini kwa lengo wa kucheza na kufurahi na watoto mbalimbali wahishio kwenye mazingira magumu.
Watasindikizwa na wasanii wengine wa ndani wanaotarajiwa kutumbuiza katika tamasha hilo ni pamoja na Ze Comedy, Q-Chief, Mr.Nice, Rose Mhando na Mrisho Mpoto. Kwa habari zaidi bonyeza hapa.
Feedback / Comments
3 Responses to “AKI AND UKWA ARE COMING TO DAR”
Leave a Reply


Ama kwa kweli vijana hawa Aki na Ukwa ni mashuhuri katika fani ya uigizaji.
Aki na Ukwa ni wasanii wakubwa nchini Nigeria pia ktk bara letu la Afrika! Mimi binafsi ni mpenzi sana wa hawa wasanii! Nimejaribu kufuatilia kwa karibu sana filamu zao ninazipenda sana! Wana uwezo mkubwa wa kuchekesha,kuelimisha na kukosoa kwa njia ya filamu zao! …….. They’re welcome …. I appreciate them!
Inafurahisha it sounds funny aki anavyofyonza halafu anaposema neno “non sence”!!!!!!