
Hamis Ramadhan,maarufu kama H-Baba(pichani) yawezekana sio jina geni kwako.Huyu ni miongoni mwa wanamuzuki waliojikita katika mtindo ujulikanao kama TAKEU(Mr.Nice ndiye anasemekana kuwa mwanzilishi wake).
Ambacho unaweza kuwa hukijui ni kuhusu “imani” aliyonayo. Hivi karibuni H-Baba alinukuliwa na chombo kimoja cha habari akisema kwamba amelogwa na mmoja wa wasanii wenzake kitu ambacho anadai ndicho kilichosababisha mambo yake kwenda ‘kombo” katika siku za karibuni.
Kwa masikitiko na upole,H-Baba amenukuliwa akisema “Unajuwa mtu ataniona mimi kama naongopa lakini ukweli ni kuwa nilichezewa ila nilikuwa sijui nimekuja kugundua baada ya kupita pita kwenye tiba.Nilianza kujihisi hivyo mara baada ya kugombana na watu wengi sana nikiwa sijielewi”
H Baba anakiri kwamba hivi sasa ameshapona kutoka katika matatizo yaliyokuwa yakimsumbua baada ya kupata tiba toka kwa wataalamu wa miti shamba.
Bila kumtaja wazi huyo ‘mchawi” wake H-Baba alizidi kusema ” Unajuwa ni ukweli kabisa waswahili hawakukosea walivyosema kikulacho kinguoni mwako, kwani yote hayo yalikuwa yakifanywa na mtu wa karibu kabisa tena rafiki yangu mkubwa”.
Mfano mmojawapo wa matatizo yake,anasema “Matatizo mengi yalitokana na Irene(Uwoya), unajua watu wengi hawakupenda niwe na Irene, kwahiyo ili kunikomoa ikabidi waniroge, mimi na Irene tukawa hatuelewani, tunagombana mpaka tukaachana,”
Je,unaamini kwamba ni kweli yawezekana H-Baba amefanyiwa anachodai kufanyiwa au hii ni “publicity stunt”?
Feedback / Comments
7 Responses to “H-BABA:NI KWELI AMELOGWA?”
Leave a Reply


sending...
h baba ndo nini mbona mi sielewi???? iyo h baba inatumikaje ni dawa ya nini na nimara ngapi kwa siku?/???? na je imethibitiswa kweli na wizara husika?????
Hbaba hujarogwa bwanaaa, ebu jaribu kumwamini Mungu.hamna aliye zaidi yake
Halafu mnauliza kwanini watz hatuendelei? Karne ya 21 bado wakubwa kwa wadogo wanamini kurogwa. Tena na huu ni mwaka wa uchaguzi, wengi wameshaanza kuogea maji ya maiti. Wakitoka huko kwanini wasiwe mafisadi? What a sad country!!!
Labda nianze na nukuu yake Saadi aliyesema “Nothing is so good for an ignorant man as silence; and if he was sensible of this he would not be ignorant.”
Sasa hapa tatizo kubwa ni kuwa KAJILOGA KUDHANI KALOGWA. Yaani kama angekaa kimya na kuamua kuwaza na kuwazua, basi angegundua namna ya kujipanga upya. Ni kwanini kila msanii nyumbani akishindwa kuwa m’bunifu na kufanikiwa anakuja na kisingizio kuwa “kalogwa”?
Wanajiloga wao kwa kwenda kwa waganga. Kwani alitegemea aende kwa mganga kisha aambiwe kuwa hajalogwa? Ina maana ama alikuwa ameshahisi kulogwa (kwa hiyo asingekubali maokeo mengine ya aina yoyote) ama alikuwa tayari kuloga na ndio maana akaenda kwa waganga.
All in all, YEYE NI SEHEMU YA ULOGAJI KWA KUWA ALIKWENDA KUSAKA MLOGAJI WAKE KWA WALOGAJI.
Blessings
huyu mimi namuona kadata kabisa ona hiyo staili yake ya nywele si ya mtu mzima huyo
this is rubbish….hana hoja huyu….aishie…
kwa kweli inaelekea irene alimuingia sana na alivyopigwa chini kisaikolojia imemletea hitilafu hizo anazozusha, hakula uchawi ni msongo wa mawazo tu yy ajipange na mziki asitafute visingizio