MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

Miezi saba baadaye,aliyekuwa daktari wa Mfalme wa Muziki wa Pop ulimwenguni,Michael Jackson, Dr.Conrad Murray ameshtakiwa rasmi kwa kifo cha mwanamuziki huyo maarufu ambaye katika maisha yake,aligusa wengi.Michael Jackson alifariki dunia tarehe 25 June mwaka jana akiwa na umri wa miaka 50.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, Dr.Murray ambaye alifikishwa mahakamani mchana huu huko Los Angeles,amekana shtaka lake na ameachiwa kwa dhamana ya dola 75,000. Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena tarehe 5 April.

Ndugu wa Michael Jackson,kaka zake Jermaine,Tito,Jackie na Randy ,dada yake LaToya na wazazi wake Joe na Katherine walikuwepo mahakamani kusikiliza kesi hiyo.

Hapo kabla Dr.Conrad Murray ambaye ni mzaliwa wa nchini Grenada,alikiri kwa polisi kwamba alimchoma Michael Jackson sindano ya dawa aina ya Anaesthetic Propofol kwa dhumuni la kumsaidia bingwa huyo wa Pop kulala.Alisema aliporudi tena chumbani alimkuta Michael akiwa hapumui.

Mchunguzi wa vifo wa Los Angeles alithibitisha baadaye kwamba dawa hizo ndizo zilizosababisha kifo cha Michael Jackson. Dr.Murray alikuwa ameajiriwa maalum kwa ajili ya kumuandaa Michael Jackson katika tour iliyokuwa ijulikane kama This Is It ambayo ilikuwa ianzie nchini Uingereza.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

2 Responses to “ALIYEKUWA DAKTARI WA MICHAEL JACKSON ASHTAKIWA KWA KIFO CHAKE”

  1. Comment by ritta on February 9th, 2010 2:25 pm

    tulimpenda sana michael jackson ila muumba wake kampenda zaidi, sipendi hata kukumbuka kwani pengo lake hakika halita zibika

  2. Comment by MOSI on February 10th, 2010 7:14 am

    YAANI PAMOJA NA UGONJWA WAKE KUWA WAZI MSULULU WA MADAWAA ALIYOTUMIA KWA MIAKA KUJITIBIA NA KUPUNGUZA MAUMIVU.,LEO HII ZAKE ZIMEFIKA SASA,ETI WAMSTAKI DAKTARI ALIYEKUWA ANAMSAIDIA,..
    KWELI NAWAAMBIENI HII KAZI SASA SIO WITO.,BONGO ONGEZENI HELA LA SIVYO NA SISI TUTAJICHUKULIA CHETU MAPEMA TUWAACHE WENETU WAKIWA SAFI MAANA
    SASA UDAKTARI WETU SASA JELA NI NJE NJE

Leave a Reply