Kama yupo msanii ambaye kwa sasa,kwa maoni yangu,ndiye balozi mzuri wa Afrika nchini Marekani,basi mwanamuziki huyo ni Akon.Huyu jamaa ni mwafrika kwanza kabla ya mambo mengine.Anaupenda uafrika na hafichi.Kila analolifanya anataka ijulikane wazi kwamba kwao ni Afrika.Mtizame katika wimbo huu wa hivi karibuni unaoitwa Oh Afrika.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Feedback / Comments

3 Responses to “OH AFRICA-AKON Ft KERI HILSON”

  1. Comment by Mzee wa Changamoto on February 10th, 2010 11:29 am

    Wimbo umetulia saana. Umebaki na ka-uafrika fulani na amefanya kazi saaana kutouweka katika mahadhi ya KANDA moja ya bara letu.
    Hauko ki-Mashariki, ki-Magharibi, ki-Kaskazini wala ki-Kusini.
    Mchanganyiko wa ujumbe, tukio kubwa lijalo Afrika (world cup) kutaja higest mountain (afrika mashariki) na atokako (magharibi) kumeufanya wimbo kuwa na UJUMLA wa Afrika.
    Natumai wataumia kama WIMBO WA KUFUNGULIA SHEREHE ZA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA.
    Kama alivyosema Da Mdogo Candy1, huu waweza kuwa “wimbo rasmi wa kombe la dunia”
    Kazi nzuri kwa hakika
    Blessings

  2. Comment by bongocelebrity on February 10th, 2010 1:14 pm

    Mzee wa Changamoto,
    Nakubaliana kabisa nanyi kwamba wimbo huu unaweza kuwa wimbo mzuri katika ufunguzi wa Kombe la Dunia kule South Africa.Labda ninachoweza kuongezea tu ni kwamba Akon anazidi kuthibitisha kwamba mafanikio yanawezekana ilhali mtu anabakia kuwa na identity yake.Hakuna haja ya kujaribu kujibadili kwa minajili ya kutamani mafanikio.

  3. Comment by mtanzania on February 18th, 2010 4:09 pm

    AMEJITAMBULISHA KUWA NI MWAFRIKA TOKA AFRIKA BAADA YA TU YA KUFANIKIWA NA KUWA JUU LAKINI TOKA ALIPOKUWA MTOTO HADI KABLA HAJATOKA ALIKUWA ANAFICHA KUWA KAMA KATOKA AFRIKA NA YEYE MWENYEWE AMEWAHI KUSEMA HIVYO KWENYE MAHOJIANO MENGI TU, NA ALISEMA HIVYO KWA VILE NI VIGUMU WA-AMERIKA KUKUPA SOKO AU SUPPORT MTU WA KUJA HASA TOKA BARA LA AFRIKA

Leave a Reply