MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

Miongoni mwa kesi na hukumu ambazo zimekuwa na mawazo au maoni yanayopishana sana katika historia ya hivi karibuni ya nchini Tanzania,ni pamoja na ile ya Nguza Viking, maarufu kama Babu Seya na wanawe watatu ambao ni Papii Kocha Nguza,Nguza Mbangu na Francis Nguza. Lipo kundi kubwa tu la raia ambao wanasema Babu Seya na wanawe walionewa(set-up) na pia lipo kundi lingine linalosema kwamba walipo(jela) ndipo wanapostahili kuwepo kwani wana hatia.Katika siku za karibuni,wanaosema kwamba Babu Seya na wanawe hawana makosa, wameongezeka zaidi.

Wakati maoni na mtizamo wa raia ukizidi kujiweka sawa,kesho ni kesho kwa Babu Seya na wanawe kwani mahakama ya Rufaa nchini Tanzania,kesho inatarajiwa kutoa hukumu dhidi ya rufaa dhidi ya hukumu ya awali ya wanamuziki hao ambao wanatetewa na mawakili wa kujitegemea Mabere Marando wa jijini Dar-es-salaam na Hamidu Mbwezeleni kutoka Zanzibar.

Je Babu Seya na wanawe wataachiwa huru hapo kesho?

Kwa undani zaidi wa kesi hii,hukumu za awali na mengineyo,bonyeza hapa

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

8 Responses to “BABU SEYA NA WANAWE KUACHIWA HURU HAPO KESHO?”

  1. Comment by ritta on February 10th, 2010 2:36 pm

    penye uongo ukweli hujitenga, watatoka tu sijawahi kuona hukumu ya familia nzima

  2. Comment by pangu pakavu on February 10th, 2010 2:58 pm

    itakuwa furaha iliyoje wakiachiliwa huru hapo kesho.wapenzi na wakereketwa tukeshe tukiomba ili tuweze kumuoa babu seya katika jukuwa la muziki.

  3. Comment by CHECHE on February 11th, 2010 2:23 am

    Nyumbani mambo ni ujanja ujanja.Utafungwa au utaonewa kwa kesi ya kupandikizwa.
    Niko na uhakika wa 85% watakuwa huru.
    Nanyi ndugu zetu wakigeni punguzeni usungura kwenye mali za watu

  4. Comment by mswahili on February 11th, 2010 2:37 am

    wewe hapo juu ni kuona na si kumuoa.

    BABU SEA TUPO PAMOJA KATIKA HILI TUNAKUOMBEA KESHO UWE HURU.
    KAMA ADHABU IMETOSHA JAMANI MBONA WATU WENGI WANAHATIA KAMA HIYO AU ZAIDI YA HIYO HAWAFUNGWI???????????????
    ANABAKA AU KULAWITI LAKINI BAADA YA MASAA KADHAA ANAKUWA HURU SHERIA KAMA NI MSUMENO MBONA HAIKATI KOTEKOTE?

  5. Comment by kokusima on February 11th, 2010 8:01 am

    wameachiwa wana wawili tu, babu seya na papi waweza kufia kule. tumuachie Mwenyezi Mungu.

  6. Comment by pangu pakavu on February 11th, 2010 2:57 pm

    wewe mswahili pamoja na uswahili wote huwezi hata kubaini kuwa kalamu ndiyo iliteleza.hapa muhimu ni kuwaombea tu dua hawa wanyonge wenzetu waachiliwe huru,kusahishiana baadaye

  7. Comment by BELLL on February 13th, 2010 6:22 am

    ILA KAMA WAMEONEWA KUNA HAJA YA KUMWOMBA MUNGU ASHUSHE HUKUMU. WATU WANA UJASIRI KWELI YAANI UNATESA MTU NA FAMILIA YAKE KIASI HICHO DUUUUUUUUUUUU I CANT IMAGINE

  8. Comment by rasto on February 16th, 2010 12:26 pm

    hukumu iliyotolewa haina mwanzo wala mwisho.hao majaji yamkini wanatekeleza wito tu.wewe uliona ama kusikia wapi mambo haya katika familia za kiafrika.mambo kama haya utayasikia tu ulaya.eti kalawiti pamoja na wanaye,mbona hakushtakiwa mkewe pia wakasote pamoja.inauma mno

Leave a Reply